Rais Nyerere na Rais Magufuli walikataa, Rais Samia usikubali Misaada ya kuingilia Sovereignty yetu!

Shida yako kaka yangu, unauma na kupuliza. Wee jilipue uwe chawa kamili, unajichelewesha sana, umri na kazi.

Nchi ambayo kila kiongozi ni bilionea, itenge fedha kwaajili ya wananchi? Uchaguzi? Waache kugawana. Waliomba, mnaodanganywa ninyinyi kuwa fedha za ndani zitaendesha uchaguzi, sasa wameumbuliwa huko.
 

..Wazungu walikuwa wapi wakati wakati Watanzania wenzetu kama Ben Saanane, Azory Gwanda, Deus Soka, Kipanya, Ally Kibao, Mdude Nyagali, na wengine, wanauwawa?
 
We pascal unaishi kwa kuwa loyal tu hapa mjini mambo yako yanakwenda, then unaishauri nchi iwe maskini jeuri, halafu mambo yetu yaharibike, it's better to live in harmony with them, na kufanya kilicho bora kama nchi.
 
Wewe kweli hamnazo!

Miradi imesimama? Ndiyo, maana hela zetu zimechoka kubeba mzigo wa maneno mengi na vitendo sifuri.

Tuna gesi, tuna dhahabu, tuna ardhi, tuna vijana — lakini tukitaka hela lazima tukakope!

Kila mwaka bajeti inasomwa kama maombi ya sadaka. Wenye pesa wanatucheka, sisi tunajifariji kuwa "Tanzania ni tajiri!"
 
Wewe hata hii internet unayotumia kupiga kelele hapa ni kwa hisani ya watu wa Marekani.

Unaelewa hilo?
 
Ukilisoma hili andiko kwa kutuliza kichwa utagundua Manjaa anaiumbua serikali ya Mama. Ukisoma mstari baada ya mstari utagundua anaikosoa serikali kwa namna ya "kupendeza"
 
..Wazungu walikuwa wapi wakati wakati Watanzania wenzetu kama Ben Saanane, Azory Gwanda, Deus Soka, Kipanya, Ally Kibao, Mdude Nyagali, na wengine, wanauwawa?
maswala ya tanzania yatatatuliwa na watanzania full stop, na hawana usafi wa kuongelea kuhusu haki sehemu yoyote duniani kwa ushenzi wanaofanya kwa kuuwa watu kila siku na kulinda wahalifu kwa maslahi ya pesa
Juzi imegundulika kampuni ya blair inahusika na kupewa tender kuwahamisha wapalestina na kujenga nyumba za waisrael gaza , watu kama hawa ambao wanaua watu wazi wazi for monry wakae kimya
 
Vipi jakaya, Mwinyi na n’kapa?

Btw samia hawezi kukubali
 
Tukawa Maskini mpaka leo,Nyerere alileta umaskini sana Tanzania
 
Tena kwa kukataa mabadilko ambayo wananchi wanataka.Tuteseke kwa manufaa ya ccm. Bwana Mayala sijui anongea upuuzi gani?wanaodai mageuzi ni wananchi sio EU. Hawa wanaunga mkono tu. Tena wanasema tuenende na standard na sheria za kwetu sio za kwao kwao
 
P,huu ushauri usiwe tu ushauri mwingine utakao kuja kukuumiza kama uleeee,halafu siku moja ukaka kujuta tena.Ila uzuri wa ushauri umnaweza kuchukua ulio na manufaa ama ulio na manufaa zaidi tu.
 
Sasa wewe unataka kumwambia Leo hii aachane na Sera zake. Maana Nyerere na Magufuli hizo zakutotaka misaada ilikuwa kwenye damu zao , yaani toka siku ya kwanza za tawala zao, sasa sijui Dada afanye mabadilliko ya damu, ili huo muelekeo wake
 
Hivi kwa kufikilia tu usimami
Wasomi wengi huwa wanajitoa ufahamu,hivi utafananisha uzalendo wa kina Nyerere na hawa wapiga dili
 
Shida mkuu ni kwamba viongozi wetu muda mwingine si wasema kweli,kuna kile kipande cha barabara ya Morocco -Mwenge,(R.I.P JPM) alisema ni hela za sikukuu ya 9 December zimetumika lakini baadaye akaenda kuzindua na sponsor..... inawezekana tukasema hela ni zetu za GE lakini behind the scene ikawa tofauti.

NB:Nchi yetu kuwa ombaomba ni tatizo la kukosa viongozi wazalendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…