Mkuu haujajibu swali langu, ni hivi hilo bomu la nuclear alifyatua wao hawafii? na kama litawazuru kwanini watumie silaha ya mwisho, ni kwamba wamezidiwa
Mkuu sio lazima uone, ushuhudie ama uwepo sehemu ya tukio ndio unaweza kuchambua mstakabali mzima/wote wa jambo husika. Mfano: sisi sote hatupo uwanja wa Vita. Lakini mgogoro huu sisi sote tunaufahamu chimbuko lake na ulipoanza: Kiongozi wa Urusi alimwona na kumtaka Rais wa Ukrein nchi yake ni budi watii amri na maagizo yake kitu ambacho aliona sio sahihi nchi nyingine imwingilie katika uendeshaji wa nchi yake na aka kataa ushauri wake. Baada ya kukataa ushauri/maelekezo akamwabia nitakupiga kipigo cha mbwa koko, kweli akaingiza jeshi akitegemea ndani ya siku mbili tatu ataiteka nchi; haikuwa hivyo, baadaye anasema sasa nitatumia silaha za nuclear: ebo imekuwa hivyo tena.
.
Sasa wewe kwa akili yako huwezi kuona huyu jamaa ameshindwa. au yale malengo yake ya awali yamekwamaa. Mkuu sio lazima uwe uwanja wa vita: ukiunganisha doti, hoja na dondoo mbalimbali kama una akili mzuri katika kuchambua mambo na hasa masuala ya operation za kivita utajua tu nani kazidiwa.
Wakuu wenzio wakuomba na kukushauri kuachana na mambo ya ugomvi wewe HUTAKI na hata kuwasikiliza HUTAKI unang'ang'ania mambo ya kibabe unaposhindwa unawaomba mkae vikakao, wakikataa unatafuta mishale ya sumu na magobole, silaha ambazo mwenzio hana: Wewe si MBABE sasa NUCLEAR wapi na wapi?