Rais Putin: Kama mnataka vita iishe acheni kuipa Ukraine silaha

Rais Putin: Kama mnataka vita iishe acheni kuipa Ukraine silaha

Lakini Putin aliyajua haya yote,alijua anakwenda kulipiga Taifa dhaifu kijeshi kuliko yeye,na Ukraine kusaidiwa alilijua mapema tu ndiyo maana akatoa lile onyo,sasa tunachoshangaa kwa nini asitekeleze kwa vitendo lile onyo lake kwa watakaomsaidia Ukraine?
mkwaraa
 
mbona West media zimetangaza kuwa May 9 ndo Putin anatangaza rasmi vita na Ukraine sasa hivi ilikuwa operation tu ya kuimarisha usalama
kwani Putin alikuwa hajui hilo? Jamaa sasa hivi wanatapatapa wakati wenzake wanataka vita iendelee kidogo akate punzi kabisa
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema mataifa ya Ulaya yanatakiwa kusaidia kumaliza vita dhidi ya Ukraine kwa kuweka shinikizo kwa Rais Volodymyr Zelensky na kusitisha kumpelekea silaha.

Rais Putin amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ambaye alikuwa akishawishi kumaliza vita hiyo baada ya Urusi kuivamia kijeshi Ukraine.

Nchi za Magharibi zimekuwa zikiisaidia Ukraine kwa vifaa vya kujilinda na kupigana na Urusi, jana Mei 2, 2022 Uingereza kutoa msaada wa vifaa vya dola 376m ikiwemo vifaa vya kielektroniki vya vita, mfumo wa rada, vifaa vya GPS na vifaa vya kuona usiku.

Maelfu ya watu wakiwemo raia wa kawaida wameuawa au kujeruhiwa katika vita hiyo tangu ilipoanza Februari 24, 2022.

Rais Macron ndiye aliyempigia simu Rais Putin na kusema yupo tayari kusaidia kumaliza mgogoro huo.

Source: BBC
Hii vita haitaweza kuisha kirahisi.
Ukiichunguza kwa undani, kuna mataifa mawili makubwa hasim yanatafutana, labda muda tu.
US anamtafuta Russia, na Russia anaitafuta US, na mbabe kati ya hawa ndiye atakaye unda dola la NWO.
 
ugomvi wa kuchangiwa hata wakiwa watoto wadogo wanaweza kukupiga.
kwani mzee Gaddafi kaangushwa na Nani?kama sio hao wamarekani na wazungu waliowapa silaha raia
Mkuu Mimi hata wakija watoto wa miaka 13 million moja.....Napiga wote
 
Naona kama vile putin mwisho wake utakuwa kama mike Tyson baada ya kupigwa Evander Holly Field,
Baada ya lile pambano hata mabondia waliondoa woga wakaanza kuomba mchezo.
Urusi ilikuwa inaogopeka duniani ila kwa sasa kajishushia heshima.
 
mwandishi uliyeleta hii mada naona wachangiaji wengi hawajakuelewa.. wengi wanafikiri Putin ndo ameziomba nchi za magharibi zisitishe kutoka siraha kwa Ukraine.. kumbe Putin Alikuwa anamjibu macroni awambie ndugu zake waache Ku supply silaha ndo vita itakoma!
Kama anajua kuna watu wana supply silaha mbona hajawaonyesha cha moto?
au kusupply silaha siyo kuingilia vita?
 
mbona West media zimetangaza kuwa May 9 ndo Putin anatangaza rasmi vita na Ukraine sasa hivi ilikuwa operation tu ya kuimarisha usalama
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]oparesheni miezi miwili sasa vita si atapigana miaka 20 asee hata akishinda atakuwa amechoka balaa. jamaa ye mwenyewe anamalizia malizia pumzi za mwisho kifo ni kwa kila mtu ila wazee ni kipaumbele .....
 
Alijua Vita itakuwa ndogo tu.
Sasa kila siku anaona jamaa wanapewa misaada yeye yupo peke yake.
Made in china yupo kimiya Sana, hahahaha hahahaha asithubutu kumpa silaha Russia lasivyo uchumi unadondoka fasta kabisa
 
ugomvi wa kuchangiwa hata wakiwa watoto wadogo wanaweza kukupiga.
kwani mzee Gaddafi kaangushwa na Nani?kama sio hao wamarekani na wazungu waliowapa silaha raia
Vita haina macho,kabla hujaanza kupigana na jirani yako lazima ujiulize kama kuna majirani wanakuunga mkono au vinginevyo ujipange kwamba hata wakimuunga mkono adui yako utawamudu.
 
mwandishi uliyeleta hii mada naona wachangiaji wengi hawajakuelewa.. wengi wanafikiri Putin ndo ameziomba nchi za magharibi zisitishe kutoka siraha kwa Ukraine.. kumbe Putin Alikuwa anamjibu macroni awambie ndugu zake waache Ku supply silaha ndo vita itakoma!
Put-in alisema atakaethubutu kumpa silaha atajibiwa mara Moja uingereza na USA wamempa silaha waziwazi na hakuna chochote alichokifanya waingereza ni watu majasiri sana kuzidi hata USA
 
Back
Top Bottom