Rais Putin: Kama mnataka vita iishe acheni kuipa Ukraine silaha

Rais Putin: Kama mnataka vita iishe acheni kuipa Ukraine silaha

Bora usingeandika hii. Imeanika utupu ulionao juu ya vita.
Mkuu operation ni ngumu zaidi kuliko vita kamili, kwasababu operation unapiga maeneo maalum lakini vita unabutua tu Kila kilichopo mbele yako, ndani ya muda mfupi wa mapambano nchi nzima inaweza kuonekana Kama ufukwe wa bahari...
 
kwani hayo maneno ya putin wewe umeyaelewa vipi?
Hivi yaani: "Mnamuombea msamaha bwana mdogo, mnataka niache kumchapa bakora, kama mnataka niache kumchapa, basi acheni kwanza kumtia kiburi, mkiendelea kumtia kiburi nitaendelea kumchapa tu"
 
Hawezi tena kutekeleza Onyo lake lile kwani kwa sasa anashughulika i.e yuko bussy na Usalama wa Uhai wake binafsi kwani Jeshi lake aliloliamini mno sasa haliamini tena na limegawanyika na mojawapo ya kundi hasimu dhidi yake (Legion) limeapa kumtoa Roho yake kwa udi na uvumba [emoji24] [emoji24]. Sasa amegeuza kibao na sio onyo tena ila anasema kama wanataka vita iishe waache kumpa silaha Ukraine. Ni Kwa nini sasa? Anafahamu fika na anajua ukweli kwamba kwa Uwezeshwaji ki-Silaha unavyoendelea sasa Ukraine, na Morale ya wa-ukraine iliyopo bado kidogo Ukraine atafika/atatinga/atatua Moscow(Kremlin) na hajui yy atauficha wapi uso wake kwa aibu kuu itokanayo na maamuzi ya kijinga aliyofanya ya Uvamizi, Majigambo na Vitisho lukuki aliyokuwa anatoa e.g. Kutoa Onyo la kibeberu, Mauaji ya kutisha ya raia aliyofanya, Bomoa-bomao ya kibabe (reckless and indiscriminate demolishing of infrastructures) n.k.
Sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"...Putin Alikuwa anamjibu macroni awambie ndugu zake waache Ku supply silaha ndo vita itakoma! "
Mkuu; nauliza: kwani wasipoacha ku supply silaha itakuwaje? Mbona alipoanzisha vita ya Uvamizi hapakuwepo supply ya silaha iliyokuwa inafanyika? Ila sasa (if you read between the lines) hilo ni ombi la mtu mzima kupitia kwa Macroni. Yaani anamtuma Macron apeleke ujumbe huo kwa ndugu zake - Mbona mwanzoni alitoa Onyo na kuweka wazi kitakachotokea kwa yeyote atakaye supply silaha kwa Ukraine? .....Huyu jamaa Ubabe umekwisha na mashavu yamemshuka kwa aibu. Anatoa ushawishi kwa mzee Macroni atumie busara zake kuwakilisha kauli hiyo kwa ndugu zake 🤪.
Kwahiyo Putin alikuwa anasubiri apigiwe simu na Macron ili atoe ombi la kuonewa huruma? Huna akili.
 
Naona watu mumesoma heading tu, bila content mkaanza comments. Putin kapigiwa simu na macron akiombwa asitishe vita, siye yeye aliyeomba Bali Macron. Naye jibu lilikuwa ni kumwambia macron vita itaendelea unless waache kuipa Ukraine silaha Kama kweli wanataka vita iishe.
Yeye Putin alisema yeyote atakayejiingiza kwenye hiyo vita,atashambuliwa vikali,kama amejua Ukraine anasaidiwa,kwanini asizishambulie nchi hizo zilizojiingiza?
Putin anaonekana dhaifu sana,huwezi ukapigana na nchi Ndogo vile toka February.
Asipokua makini,atapigana hadi mwakani hapo Ukraine.
 
Kama yeye mwanaume kweli anaogopa nini Ukraine akisaidiwa
SI anajiamini.
kauli za msiwaidie ni za kinyonge Sana
Kaamua kupiga apige tu.
asianze kulia lia.
Hivi yaani: "Mnamuombea msamaha bwana mdogo, mnataka niache kumchapa bakora, kama mnataka niache kumchapa, basi acheni kwanza kumtia kiburi, mkiendelea kumtia kiburi nitaendelea kumchapa tu"
 
Yeye Putin alisema yeyote atakayejiingiza kwenye hiyo vita,atashambuliwa vikali,kama amejua Ukraine anasaidiwa,kwanini asizishambulie nchi hizo zilizojiingiza?
Putin anaonekana dhaifu sana,huwezi ukapigana na nchi Ndogo vile toka February.
Asipokua makini,atapigana hadi mwakani hapo Ukraine.
Ndugu, inaonekana una shauku kubwa sana ya kuona Russia anarusha bomu Washington, nadhani siku likitokea hili jambo utapiga sana vigeregere. Omba maisha marefu tu, mabomu yanatengenezwa ili yatumike, kuna siku kiu yako itakatwa, unachokitamani kitakuja kutokea tu, hata kama kitachelewa.
 
Kama yeye mwanaume kweli anaogopa nini Ukraine akisaidiwa
SI anajiamini.
kauli za msiwaidie ni za kinyonge Sana
Kaamua kupiga apige tu.
asianze kulia lia.
Ndugu hapo muoga ni Macron, kwanini ampigie simu Putin wakati huu ambao Russia ameshajichokea (kwa mtazamo wako)? Huu ndio ulikuwa muda wa kuendelea kutuma silaha zaidi Ukraine, tena wakati huu ulikuwa ni wakati wa kutuma majeshi sio silaha tu, huu ulikuwa ni wakati wa kumpiga Russia mpaka Moscow. Kumpigia simu Putin kumuomba aache kuipiga Ukraine ni uoga uliopitiliza.
 
ndio wajue hana mpango wakumaliza vita, na huenda akatangaza vita kamili.
Vita kamili ni ipi,maana pale anapigana vita toka February hadi leo.Kama ile vita siyo kamili,basi vita kamili itapigwa miaka mingi sana.
 
Ndugu, inaonekana una shauku kubwa sana ya kuona Russia anarusha bomu Washington, nadhani siku likitokea hili jambo utapiga sana vigeregere. Omba maisha marefu tu, mabomu yanatengenezwa ili yatumike, kuna siku kiu yako itakatwa, unachokitamani kitakuja kutokea tu, hata kama kitachelewa.
Yeye arushe tu,US naye atajua atachomfanya.
 
Hii vita haitaweza kuisha kirahisi.
Ukiichunguza kwa undani, kuna mataifa mawili makubwa hasim yanatafutana, labda muda tu.
US anamtafuta Russia, na Russia anaitafuta US, na mbabe kati ya hawa ndiye atakaye unda dola la NWO.
Sidhani kama Russia anamtafuta US, amtafute kwa kipi? US anaweza akawa anamuwinda Russia sababu kila akipanga mipango yake huwa Russia anaingia kuweka ugumu. Na anawea ugumu ili tu aaminishe dunia kuwa hakuna mwenye nguvu kijeshi kama yeye. Sasa awamu hii Russia kaingia pabaya.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]oparesheni miezi miwili sasa vita si atapigana miaka 20 asee hata akishinda atakuwa amechoka balaa. jamaa ye mwenyewe anamalizia malizia pumzi za mwisho kifo ni kwa kila mtu ila wazee ni kipaumbele .....
Operation imeanza mwezi wa tatu tayari.
 
Maneno ya putin ni ya mtu aliyekata Tamaa.

Back
Top Bottom