PreGE2025 Rais Samia: 4R zisitumike kama kisingizo cha kuvunja sheria

PreGE2025 Rais Samia: 4R zisitumike kama kisingizo cha kuvunja sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwani serikali ni ya nani?? wanafarakanisha vipi wakati serikali ndo inahusika? Police ni sehemu ya serikali. uliofanyika jana ni ubaya na si kitu cha kushabikia. Sioni sababu watu kuuwawa na kuvunjwa viungo vyao sababu ya kulinda serikali ya ccm.
Waibe kura wao,wawasingizie wanao pinga wizi wa muda!? Nchi hii ni ya Watanzania wote, sio Nchi ya ccm peke yao, mtu yeyote mwenye vigezo vya kugombea agombee na achaguliwe sio kuenguliwa ,halafu watu wanapinga udhalimu wenu wakati wa chaguzi mnawaweka ndani kwa kesi za uhaini!

Wahaini wako maofisini, kwakua kuiba uchaguzi ni UHAINI pia
 
Rais Samia Suluhu Hassan anategemea kulihutubia Taifa saa mbili kamili usiku wa leo, Aprili 25, 2025.

Nasisitiza tena, yaliyotokea jana nchini mwetu hayapo hata kwenye nchi za madikteta! Ni mambo ya kufarakanisha kati ya watawala na wenye mawazo tofauti. Ni chuki ni uhasama!

Updates....

Rais Samia ameeleza kuwakwa mwaka huu sherehe za Muungano zitafanyika kwenye mikoa yote Tanzania ambapo viongozi mbalimbali wataungana na wananchi katika uzinduzzi w miradi ya Maendeleo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni "miaka 61 ya muungano wa Tanzania, Muungano wetu ni dhamana, eshima na tunu ya Taifa, shiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025"

Rais Samia: Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na amani ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki

Rais Samia ameeleza pia kuwa falsafa ya 4R isiwe sababu ya kuvunja sheria. Aidha amewataka wananchikujittokeza kushiriki kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi

Hakuna aliye juu ya sheria na wote tunatakiwa kuendesha shughuli zetu za kisiasa, tukizingatia amani na usalama wa nchni



===
Siwezi kupoteza mda wangu kumsikiliza mpuuzi na upuuzi
 
Inauma Sana kufanyia unyama binadamu wenzako.
Nimesikitika sana. Mfano waliovunjwa miguu ni ndugu zako unaowategemea, utajisikiaje? Tuna lockups, magereza nk, kote huko umeshindwa kuwapeleka hadi uwavunjevunje miguu,kweli ni haki? Wazee kama hawa hawana silaha yeyote.
 
Nilichogundua...hizi ni kafara...kama mkuu wa nchi anaona ni sawa wananchi wake kubunjwa miguu..mikono.,migongo kwa sababu wanavunja amani kwa kwenda mahakamani basi behind the scene ana jambo lake la kigiza....najua wengine hawaamini haya mambo but huu ndo ukweli....vitu vya kiroho mara nyingi havimake sense
 
Asante sana mheshimiwa Rais Samia suluhu hassan, umeongea kwa sauti ya mamlaka haswa, Mungu aendelee kukupa nguvu utufikishe penye neema pia
Ameen
 
Lissu hakutegemea kuwa mwenyekiti, alitaka kumtisha mbowe ili wayamalize kwa kupewa umakamu, it seems mbowe alikuwa ameshamchoka akaamua kukausha, alivyoona ataaibika kaamua kurukia kwenye bwawa la mamba. kwasasa wanatengeneza content ionekane wameshwa kutokana na mabavu ya serikali, by the way baada ya oktoba hawatakuwa na mbunge hata mmoja maana yake hawatakuwa na ruzuku, sasa hii tonetone sidhani hata mishahara watalipana
 
Hatoongea kuhusu ya watu kupigwa mahakamani. Ataongelea sherehe za muungano za kesho.

Akiwa na ujasiri sana anaweza kufafanua kauli za mvutano wa kibiashara na south africa na malawi kwa kunyoosha alipoharibu bashe

Pia atapiga mikwara viongozi wa dini na.wanasiasa. Atamalizia na simba kufuzu.
Kama ulijua, au una karama ya unabii nini?
 
4 R ndio katiba? Anavunja katiba anajificha kwenye 4R tujihurumie tu haki.
 
Back
Top Bottom