Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Sio yeye atakayefunga watu 1000 wala mimi kupata kitu chochote,hiyo ni sheria kufuata mkondo mkuu,wapewe haki yao ya mafao ila tusiishie hapo kama walighushi na sheria ina maelekezo yake kwa mtu aliyeghushi,nao ufuatwe halikadhalika.
Hoja yako ni Wakipewa hupati chochote, wakikosa pia hupati chochote ila Sheria ifuate mkondo.
Sawa.

Hoja yangu ni wale ni wahalifu ni kweli ila serikali ilikubali huduma zao na sasa imewaadhibu kwa kuwafukuza kazi, Kama kuna uwezekano wa kupewa yale makato waliyokuwa wanakatwa wakati wanatoa huduma wapewe. Mbona kuna misamaha ya raisi? Kushupalia wasipewe ni roho ya ajabu. Ukumbuke wengi hapa ni walitumia majina ya watu kujiendeleza. Miaka ya nyuma imefanyika sana.
 
Bora eewe umeliona hilo. Akiwalipa vyeti feki atakuwa na tatizo.yaan jitu ligushi vyeti afu alipwe fidia?

Watanzania wanashabekia ujinga.baada ta kupambana vijana wapate kazi wanapambana vyeti feki walipwe
Fidia gani? Ni zile stahiki zao wanazokatwa za mishahara nssf🤣🤣 kwa huduma walizotoa. Sasa hizo unazichukua za nn? Embu jiulize tu, wewe wakipunguziwa adhabu wakapewa zile stahiki za 5%walizokatwa kwenye mshahara kwann unaumia?
 
Mimi nasema walipwe.

Kisha washtakiwe kwa kughushi vyeti kesi zianze mahakamani.

Kukiliwa kwa mwali na kwa kungwi kuliwe.
 
Narudia tena kukuelewesha walipwe haki yao wanayodai ila baada ya hapo wachukue mkondo wa sheria.Huduma walitoa sawa,walipofuatiliwa wakagunduliwa wamefoji vyeti wakafukuzwa hawakulipwa,walipwe sasa,then tuendelee na kufuata utaratibu wa sheria zetu.
 
Mimi nasema walipwe.

Kisha washtakiwe kwa kughushi vyeti kesi zianze mahakamani.

Kukiliwa kwa mwali na kwa kungwi kuliwe.
Hiki ndiyo kinachostahili kufuatwa,walipwe haki yao kwanza then sheria ya kughushi ifuatwe kama wakishafungwa Mama atawasamehe awasamehe hatuna shida na hilo.
 
Comment za humu zinaonesha kuna watu walipewa sumu ya ukatiri aliokuwa nao jiwe so umeharibu nchi kabisa.. mama anakazi ya kunywesha watu maziwa sumu itoke... Kazi iendelee Mama anabonyeza reset button zote.. ukatiri uishe na wasiotaka Wamfuate Jiwe Motoni akhera
 
Narudia tena kukuelewesha walipwe haki yao wanayodai ila baada ya hapo wachukue mkondo wa sheria.Huduma walitoa sawa,walipofuatiliwa wakagunduliwa wamefoji vyeti wakafukuzwa hawakulipwa,walipwe sasa,then tuendelee na kufuata utaratibu wa sheria zetu.
Huo ndo utaratibu sahihi ila wapo wengi tutapoteza muda na wakiwa na hatia hatuwezi wafunga wote.
Unajua hata nyumbu wana sheria? Wa kwanza akiingia mtoni mnafuata wote bila kujali kilichopo humo mtoni.
Sisi ni binadamu, ubinadamu una nafasi kubwa sana katika maamuzi.
5%walizokatwa kwenye mshahara wapewe kisha serikali iwe makini kwenye vetting.
 
Kama ulifanya kazi kwa jasho na ukachangia mifuko,lazima ulipwe,hatutaki dhulumati dhulumati
Sasa kama mtu alipata kazi kwa vyeti feki sii tayari alifanya dhuluma....so wacha nae adhulumiwe nguvu yake
 
Sasa kama mtu alipata kazi kwa vyeti feki sii tayari alifanya dhuluma....so wacha nae adhulumiwe nguvu yake
Wewe ni wale wa sitaki ubinadamu, wasilipwe na sitaki masihara. Hapo unapigania 5% waliyokatwa wasilipwe.
 
Hapana mkuu,wapewe haki yao ila kwa kughushi sheria ifuatwe sambamba.Muda upo,kama tulipata wa kufuatilia na kujua walighushi na kuwafukuza basi muda upo wa kuwashitaki,Walijua wazi wameghushi sio bahati mbaya.Wapewe haki yao kisha wapelekwe mahakamani.
 
Sawa boss.
 
Basi hamna shida ya ubinadamu...kinachotakiwa ni kuwafukuza na hamna kupata mafao kwa sababu hawastahili kupata.
Kuna msamaha wa raisi hata wafungwa wanaachiwa kabla ya kutumikia adhabu yote.
Kama raisi ameona ni sahihi kuwasamehe na kuwapa yale makato yao ya 5% kwann mtu imuume?
Ukitaka kujipima ww ni mtu wa aina gani maeneo kama haya ndo pa kujipima. Mtu kapewa msamaha, ila unapigania asiupate. Ili nini? Sheria zipo na misamaha ipo. Hata nyumbu wana sheria za kuhama hama kutafuta malisho ila sisi ni binadamu, kiongozi wetu anapoona ni busara kuweka sheria pembeni na ubinadamu ufanye kazi ni vizuri kuheshimu.
 
kumbuka pia raisi anatoa msamaha kwa wahalifu mkuu jielewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…