Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Walikatwa 5% ya mishara yao ww mshipa unakutoka kweli. 5% walikatwa ikaenda kwenye mifuko ya jamii, hiyo ndo wakisamehewa wanalipwa daah🤣🤣🤣
Wasiposamehewa pia ni sawa tu ila inashangaza kushupalia wasisamehewe.
Ishu hapa sio kwamba tunaona watafaidaka na hizo hela and all that.
Its about principles and setting moral standards that govern human behaviour.
Kufoji vyeti ni serious offense.

Tuchukulie mfano nafojincheti cha udaktari...maisha ya watu wa ngapi nayaweka rehani? Tuataka watumishi waaminifu hizyo basi lazima tuonyeshe pasipo shaka kuwa vitendo vyovyote vya udanganyifu havita vumiliwa.

Ugumu wa kuwa kiongozi upo katika kuweza kuweka hisia pembeni na kuongoza kulingana na miongozo iliyowekwa. Utakapoanza kuweka exceptions ndio matatizo utokea.
 
Hivi adui wa chadema hasa ni Magufuli, Polepole na Bashiru au ccm?
Hapana, adui wa chadema ni chadema yenyewe baada ya kuiacha ile misingi iliyojengwa na waasisi wake kina Mtei, Makani, Ngwilulupi, Shinganya, Wasira, Barongo ... Hapakuwa na namna, ila kuingia shimoni. Walitarajia mafaninikio kupitia njia ya mkato.

Wangekuwa wakurupukaji kipindi kile wazee wetu hao, Mrema 1995, at his political peak, angejiunga chadema. Lakini wale wazee walipima masharti waliyopewa na mrema, na long term benefits, wakaona huyu ni boya. Na NCCR kipindi kile kwa hofu ya nguvu ya CDM wakambeba Mrema bila kujiuliza kesho ingekuwaje.

Itoshe tu kusema kama CDM ingesimamia misingi yake bila kubabatikia haya kina Lowasa, pamoja na figisu za JPM, leo CDM ingekuwa level nyingine.
 
Ishu hapa sio kwamba tunaona watafaidaka na hizo hela and all that.
Its about principles and setting moral standards that govern human behaviour.
Kufoji vyeti ni serious offense.

Tuchukulie mfano nafojincheti cha udaktari...maisha ya watu wa ngapi nayaweka rehani? Tuataka watumishi waaminifu hizyo basi lazima tuonyeshe pasipo shaka kuwa vitendo vyovyote vya udanganyifu havita vumiliwa.

Ugumu wa kuwa kiongozi upo katika kuweza kuweka hisia pembeni na kuongoza kulingana na miongozo iliyowekwa. Utakapoanza kuweka exceptions ndio matatizo utokea.
Walikosea na ndio Wameshafukuzwa kazi, zamani watu walitumia vyeti vya watu wengine kujiendeleza, hilo linajulikana wazi. Wala hakuna siri. Kijijini watu walinunua majina sana tu ya majirani wasiotaka kuendelea na shule na wamefaulu.
Na kuwaondoa si sababu walikuwa hawawafahamu kuna watumishi wamejiendeleza kwa vyeti vya wengine na sasa wamekamatwa, sababu ni nyingine kabisa, ukifikiri kwa makini utaifahamu.

Ikitokea wakasamehewa na kupewa hizo 5% wewe una tatizo na hilo?
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Huyo aliyewaajiri na kuwathibitisha kazini hakukagua vyeti vyao? acha roho mbaya kama walifanya kazi walipwe stahiki zao acheni dhuluma za kipuuzi...
 
Huyo aliyewaajiri na kuwathibitisha kazini hakukagua vyeti vyao? acha roho mbaya kama walifanya kazi walipwe stahiki zao acheni dhuluma za kipuuzi...
Kwa hiyo tapeli akifanikiwa kumrubuni mtu na kumtapeli inakuwa halali kwa kuwa aliyetapeliwa ameshindwa kujua kuwa ametapeliwa......??
 
Hoja yako ni Wakipewa hupati chochote, wakikosa pia hupati chochote ila Sheria ifuate mkondo.
Sawa.

Hoja yangu ni wale ni wahalifu ni kweli ila serikali ilikubali huduma zao na sasa imewaadhibu kwa kuwafukuza kazi, Kama kuna uwezekano wa kupewa yale makato waliyokuwa wanakatwa wakati wanatoa huduma wapewe. Mbona kuna misamaha ya raisi? Kushupalia wasipewe ni roho ya ajabu. Ukumbuke wengi hapa ni walitumia majina ya watu kujiendeleza. Miaka ya nyuma imefanyika sana.
Kuna majitu yana roho mbaya kama ya mwendazake , yaani ibilisi hakosi wafuasi .
 
Maoni yako hayana ubinadamu wa kujua hawa watumishi walitumikia hii nchi kuliko hata Jiwe , Wana familia zao na mchango wait wa taifa upo na wamechangia mifuko ya hifadhi ya jamii .
Hata matapeli pia wanafamilia na wanaitumikia nchi kwa njia zisizo halali.......kuwalipa walioghushi vyeti ni kuhalalisha uhalifu wao na kuwavunja moyo vijana wanaosoma vyuoni.......
 
Kuna majitu yana roho mbaya kama ya mwendazake , yaani ibilisi hakosi wafuasi .
Kati ya aliyeghushi vyeti na kujipatia ajira isivyo halali huku wenye sifa stahiki na vyeti halali wakiachwa wakiteseka......na anayegoma kuwalipa wasichostahili kwa udanganyifu wao nani mwenye roho mbaya......???
 
Tatizo ni kwamba kuna watu hawataki msamaha kwa sababu labda anamfahamu atakayelipwa sasa anataka ateseke asilipwe. Maana najaribu kuwaza kwann uumie mwingine akisamehewa sipati jibu.
Hata ibilisi hakosi wafuasi ndugu , mwendazake ameacha wafuasi ndio hao .
 
Walikosea na ndio Wameshafukuzwa kazi, zamani watu walitumia vyeti vya watu wengine kujiendeleza, hilo linajulikana wazi. Wala hakuna siri. Kijijini watu walinunua majina sana tu ya majirani wasiotaka kuendelea na shule na wamefaulu.
Na kuwaondoa si sababu walikuwa hawawafahamu kuna watumishi wamejiendeleza kwa vyeti vya wengine na sasa wamekamatwa, sababu ni nyingine kabisa, ukifikiri kwa makini utaifahamu.

Ikitokea wakasamehewa na kupewa hizo 5% wewe una tatizo na hilo?
Tatizo langu ni moja tuu. Tunaweka mfano mbaya kwa kizazi kijacho.
 
Kwa hiyo tapeli akifanikiwa kumrubuni mtu na kumtapeli inakuwa halali kwa kuwa aliyetapeliwa ameshindwa kujua kuwa ametapeliwa......??
Amekutapeli nini wakati umekaa naye miaka yote na umeridhika na kazi yake.....kama ni tapeli si ungemgundua kutoka mwanzo kwamba hawezi ku-perform kama ulivyotarajia na ungemwondoa kabla ya kumthibitisha, usilete undezi hapa hao watu walipwe stahiki zao.
 
Hata matapeli pia wanafamilia na wanaitumikia nchi kwa njia zisizo halali.......kuwalipa walioghushi vyeti ni kuhalalisha uhalifu wao na kuwavunja moyo vijana wanaosoma vyuoni.......
Mbona jeshini , polisi , magereza , uhamiaji na usalama wataifa hawakufukuzwa kazi huko jeshini cheti kimoja mpaka watu kumi wanakitumia na Wana vyeo vikubwa sana , hii double standard ya nini ?
 
Kati ya aliyeghushi vyeti na kujipatia ajira isivyo halali huku wenye sifa stahiki na vyeti halali wakiachwa wakiteseka......na anayegoma kuwalipa wasichostahili kwa udanganyifu wao nani mwenye roho mbaya......???
Hawa unaowapigania wasilipwe wengi ni 50yrs, 55yrs hata 60yrs. Kuna ambao walikuwa wanastahafu wiki inayofuata. Na wengi ni wale waliotumia majina ya watu kujiendeleza zamani hizo. Yaani mtoto A anafulu haendi shule mtoto B anatumia jina lake kuendelea na masomo. Imefanyika sana zamani hii. Kwann unaumia sana na hawa watu?
 
Mbona wamepokea michango yao kama ni feki.Acha chuki za mwendazake
Mifuko ya hifadhi za kijamii haiwajibiki na ukaguzi wa uhalali wa muajiriwa hill ni jukumu la muajiri.....kama muajiriwa amemuongopea muajiri kwa kughushi vyeti hiyo ni habari nyingine.....na kile kipato atakacholipwa ni haramu pamoja na mafao yap yalioukuwa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii.....
 
Kati ya aliyeghushi vyeti na kujipatia ajira isivyo halali huku wenye sifa stahiki na vyeti halali wakiachwa wakiteseka......na anayegoma kuwalipa wasichostahili kwa udanganyifu wao nani mwenye roho mbaya......???
Na aliyeiba tilioni moja pointi tano , hajaacha watu wakiteseka kwa kukosa maji , madawa na huduma mbalimbali za serikali .
 
Back
Top Bottom