KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Rais anatoa msamaha kwa wahalifu ambao wameshatumikia vifungo....sasa hawa wahalifu wa vyeti feki wameshitakiwa na kuhukumiwa lini na walitumikia lini adhabu zao mpaka wastahili msamaha au huruma ya rais.....??kumbuka pia raisi anatoa msamaha kwa wahalifu mkuu jielewe
Ishu hapa sio kwamba tunaona watafaidaka na hizo hela and all that.Walikatwa 5% ya mishara yao ww mshipa unakutoka kweli. 5% walikatwa ikaenda kwenye mifuko ya jamii, hiyo ndo wakisamehewa wanalipwa daah🤣🤣🤣
Wasiposamehewa pia ni sawa tu ila inashangaza kushupalia wasisamehewe.
Shabash! Madhara yake sii tumeyaonaAliyefoji thesis ya PhD ya maganda ya korosho yeye ndio binadamu wengine sio .
Hapana, adui wa chadema ni chadema yenyewe baada ya kuiacha ile misingi iliyojengwa na waasisi wake kina Mtei, Makani, Ngwilulupi, Shinganya, Wasira, Barongo ... Hapakuwa na namna, ila kuingia shimoni. Walitarajia mafaninikio kupitia njia ya mkato.Hivi adui wa chadema hasa ni Magufuli, Polepole na Bashiru au ccm?
Walikosea na ndio Wameshafukuzwa kazi, zamani watu walitumia vyeti vya watu wengine kujiendeleza, hilo linajulikana wazi. Wala hakuna siri. Kijijini watu walinunua majina sana tu ya majirani wasiotaka kuendelea na shule na wamefaulu.Ishu hapa sio kwamba tunaona watafaidaka na hizo hela and all that.
Its about principles and setting moral standards that govern human behaviour.
Kufoji vyeti ni serious offense.
Tuchukulie mfano nafojincheti cha udaktari...maisha ya watu wa ngapi nayaweka rehani? Tuataka watumishi waaminifu hizyo basi lazima tuonyeshe pasipo shaka kuwa vitendo vyovyote vya udanganyifu havita vumiliwa.
Ugumu wa kuwa kiongozi upo katika kuweza kuweka hisia pembeni na kuongoza kulingana na miongozo iliyowekwa. Utakapoanza kuweka exceptions ndio matatizo utokea.
Hata mm namshangaa kaanza kupotosha watu,yy Amesema wa darasa la saba tu na wa vyeti feki wanatoka wapi?acheni upotoshaji.Wa vyeti feki hajawataja
Huyo aliyewaajiri na kuwathibitisha kazini hakukagua vyeti vyao? acha roho mbaya kama walifanya kazi walipwe stahiki zao acheni dhuluma za kipuuzi...Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....
Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........
Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Huyo chief anapotoshaSikiliza hotuba dakika ya kumi na tatu mpaka kumi na sita .
Amesema vyeti feki na darasa la saba ndugu bila chenga .Hv alisema na wa vyeti feki si Wale wa darasa la Saba tu!!??
Kwa hiyo tapeli akifanikiwa kumrubuni mtu na kumtapeli inakuwa halali kwa kuwa aliyetapeliwa ameshindwa kujua kuwa ametapeliwa......??Huyo aliyewaajiri na kuwathibitisha kazini hakukagua vyeti vyao? acha roho mbaya kama walifanya kazi walipwe stahiki zao acheni dhuluma za kipuuzi...
Kuna majitu yana roho mbaya kama ya mwendazake , yaani ibilisi hakosi wafuasi .Hoja yako ni Wakipewa hupati chochote, wakikosa pia hupati chochote ila Sheria ifuate mkondo.
Sawa.
Hoja yangu ni wale ni wahalifu ni kweli ila serikali ilikubali huduma zao na sasa imewaadhibu kwa kuwafukuza kazi, Kama kuna uwezekano wa kupewa yale makato waliyokuwa wanakatwa wakati wanatoa huduma wapewe. Mbona kuna misamaha ya raisi? Kushupalia wasipewe ni roho ya ajabu. Ukumbuke wengi hapa ni walitumia majina ya watu kujiendeleza. Miaka ya nyuma imefanyika sana.
Hata matapeli pia wanafamilia na wanaitumikia nchi kwa njia zisizo halali.......kuwalipa walioghushi vyeti ni kuhalalisha uhalifu wao na kuwavunja moyo vijana wanaosoma vyuoni.......Maoni yako hayana ubinadamu wa kujua hawa watumishi walitumikia hii nchi kuliko hata Jiwe , Wana familia zao na mchango wait wa taifa upo na wamechangia mifuko ya hifadhi ya jamii .
Kati ya aliyeghushi vyeti na kujipatia ajira isivyo halali huku wenye sifa stahiki na vyeti halali wakiachwa wakiteseka......na anayegoma kuwalipa wasichostahili kwa udanganyifu wao nani mwenye roho mbaya......???Kuna majitu yana roho mbaya kama ya mwendazake , yaani ibilisi hakosi wafuasi .
Hata ibilisi hakosi wafuasi ndugu , mwendazake ameacha wafuasi ndio hao .Tatizo ni kwamba kuna watu hawataki msamaha kwa sababu labda anamfahamu atakayelipwa sasa anataka ateseke asilipwe. Maana najaribu kuwaza kwann uumie mwingine akisamehewa sipati jibu.
Tatizo langu ni moja tuu. Tunaweka mfano mbaya kwa kizazi kijacho.Walikosea na ndio Wameshafukuzwa kazi, zamani watu walitumia vyeti vya watu wengine kujiendeleza, hilo linajulikana wazi. Wala hakuna siri. Kijijini watu walinunua majina sana tu ya majirani wasiotaka kuendelea na shule na wamefaulu.
Na kuwaondoa si sababu walikuwa hawawafahamu kuna watumishi wamejiendeleza kwa vyeti vya wengine na sasa wamekamatwa, sababu ni nyingine kabisa, ukifikiri kwa makini utaifahamu.
Ikitokea wakasamehewa na kupewa hizo 5% wewe una tatizo na hilo?
Amekutapeli nini wakati umekaa naye miaka yote na umeridhika na kazi yake.....kama ni tapeli si ungemgundua kutoka mwanzo kwamba hawezi ku-perform kama ulivyotarajia na ungemwondoa kabla ya kumthibitisha, usilete undezi hapa hao watu walipwe stahiki zao.Kwa hiyo tapeli akifanikiwa kumrubuni mtu na kumtapeli inakuwa halali kwa kuwa aliyetapeliwa ameshindwa kujua kuwa ametapeliwa......??
Mbona jeshini , polisi , magereza , uhamiaji na usalama wataifa hawakufukuzwa kazi huko jeshini cheti kimoja mpaka watu kumi wanakitumia na Wana vyeo vikubwa sana , hii double standard ya nini ?Hata matapeli pia wanafamilia na wanaitumikia nchi kwa njia zisizo halali.......kuwalipa walioghushi vyeti ni kuhalalisha uhalifu wao na kuwavunja moyo vijana wanaosoma vyuoni.......
Hawa unaowapigania wasilipwe wengi ni 50yrs, 55yrs hata 60yrs. Kuna ambao walikuwa wanastahafu wiki inayofuata. Na wengi ni wale waliotumia majina ya watu kujiendeleza zamani hizo. Yaani mtoto A anafulu haendi shule mtoto B anatumia jina lake kuendelea na masomo. Imefanyika sana zamani hii. Kwann unaumia sana na hawa watu?Kati ya aliyeghushi vyeti na kujipatia ajira isivyo halali huku wenye sifa stahiki na vyeti halali wakiachwa wakiteseka......na anayegoma kuwalipa wasichostahili kwa udanganyifu wao nani mwenye roho mbaya......???
Mifuko ya hifadhi za kijamii haiwajibiki na ukaguzi wa uhalali wa muajiriwa hill ni jukumu la muajiri.....kama muajiriwa amemuongopea muajiri kwa kughushi vyeti hiyo ni habari nyingine.....na kile kipato atakacholipwa ni haramu pamoja na mafao yap yalioukuwa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii.....Mbona wamepokea michango yao kama ni feki.Acha chuki za mwendazake
Na aliyeiba tilioni moja pointi tano , hajaacha watu wakiteseka kwa kukosa maji , madawa na huduma mbalimbali za serikali .Kati ya aliyeghushi vyeti na kujipatia ajira isivyo halali huku wenye sifa stahiki na vyeti halali wakiachwa wakiteseka......na anayegoma kuwalipa wasichostahili kwa udanganyifu wao nani mwenye roho mbaya......???