Mkuu tuseme serikali imeajiri dereva ambaye kafanya kazi ya kuendesha mabosi zaidi ya miaka 20 kwa uaminifu na kwa ufanisi mkubwa hadi kuaminiwa kumwendesha mkuu wa nchi, leo hii unamwondoa kwa kufoji cheti na unamnyima kila kitu wakati miaka yote hiyo ulitumia huduma yake. Unataka kutuaminisha cheti chake ndo kilikuwa kinaendesha mabosi au yeye kama yeye......yaani wewe umwajiri mtu halafu baada ya miaka 30 ndo ugundue hakufaa kuajiriwa na unamyima stahiki zake zote, huu unakuwa zaidi ya uzwazwa..Mimi sija-ungunga elimu yangu lakini siungi mkono swala hilo.Mtu aliye-gushi cheti na kufanya kazi amefanya makosa mawili:
1.Kugushi cheti,kosa ambalo ni prosecutable by law,
2.Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kosa ambalo pia ni prosecutable by law.
Sasa tuwe wakweli tu, mtu kama huyo analipwa mafao,si alitakiwa kupelekwa mahakamani in the first place.
Kiukweli maamuzi ya kuwalipa hawa watu hayaja-zingatia sheria,weledi na yana-set an extremely bad precedent.
Tunaomba Rais afikirie upya maamuzi yake,yanachangia moja kwa moja katika kuiharibu jamii yetu morally.