Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Mimi sija-ungunga elimu yangu lakini siungi mkono swala hilo.Mtu aliye-gushi cheti na kufanya kazi amefanya makosa mawili:
1.Kugushi cheti,kosa ambalo ni prosecutable by law,
2.Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kosa ambalo pia ni prosecutable by law.

Sasa tuwe wakweli tu, mtu kama huyo analipwa mafao,si alitakiwa kupelekwa mahakamani in the first place.

Kiukweli maamuzi ya kuwalipa hawa watu hayaja-zingatia sheria,weledi na yana-set an extremely bad precedent.

Tunaomba Rais afikirie upya maamuzi yake,yanachangia moja kwa moja katika kuiharibu jamii yetu morally.
Mkuu tuseme serikali imeajiri dereva ambaye kafanya kazi ya kuendesha mabosi zaidi ya miaka 20 kwa uaminifu na kwa ufanisi mkubwa hadi kuaminiwa kumwendesha mkuu wa nchi, leo hii unamwondoa kwa kufoji cheti na unamnyima kila kitu wakati miaka yote hiyo ulitumia huduma yake. Unataka kutuaminisha cheti chake ndo kilikuwa kinaendesha mabosi au yeye kama yeye......yaani wewe umwajiri mtu halafu baada ya miaka 30 ndo ugundue hakufaa kuajiriwa na unamyima stahiki zake zote, huu unakuwa zaidi ya uzwazwa..
 
Kosa la kudanganya na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu lipo pale pale mkuu.Umepata fedha kwa njia ya udanganyifu!
Mwizi kumwambia alirudishiwe chake alichoiba aiseeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!

Magufuli huko uliko fufuka tunakukumbuka.Njoo huku wezi waambiwa warudishiwe chao walichoiba ni jasho lao!!
 
Kosa namba 2 linakuaje kama alifanya kazi? Cheti ni kikatatasi tu, hata cha kwako kwa hapa hakikusaidii kufikiri vizuri!
Suala la msingi, mama ameamua walipwe na maumivu yenu yapo kwenye maamuzi ya mama kwenda kinyume na #yesuwalugola wenu! Legacy legacy, legacy! na mengi yatapanguliwa na madudu kuibuliwa!
Linakuwepo kwa sababu aligushi cheti,kwa hivo fedha alizopata amezipata kwa kuwa kadanganya.
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Hoja yako ya ushindani sawa wa ajira ni tofauti na hoja ya watuhumiwa wa kuajiriwa Kwa vyeti deli kisha kufanya kazi katika Serikali au taasisi zake, kulipwa haki zake. Suala la illegality haliondoi ukweli kuwa mhanga alifanya kazi na anastahili kulipwa mara anapoachiwa au kuacha kazi. Serikali ilitakiwa kujitafakari katika ulegevu wa muundo na mifumo yake kiasi cha kuruhusu/kupitisha watu wasiokuwa na vigezo stahiki kuajiriwa. Na kama wahanga waliweza kufanya kazi zao kwa ufanisi, basi hakukuwa na sababu wa kuwekwa kwa vigezo vya ajira Kwa kuwa havihusiani na utendaji kazini. Hapa pia patahitaji review! Hayo yote ni makosa ya Serikali, siyo walioajiriwa na kisha kutimuliwa Kwa hoja ya vyeti fake. Inawezekana kabisa Serikali ilikuwa na uhitaji wa nguvukazi wakati huo inaajiri watumishi wasiokuwa na vyeti stahiki kiasi kwamba hakukuwa na ushindani Kwa walioajiriwa. Katika hili, hoja kwamba kuna watu waliachwa wakiwa most qualified haina mashiko yoyote. Let's be realistic please!
 
Mkuu tuseme serikali imeajiri dereva ambaye kafanya kazi ya kuendesha mabosi zaidi ya miaka 20 kwa uaminifu na kwa ufanisi mkubwa hadi kuaminiwa kumwendesha mkuu wa nchi, leo hii unamwondoa kwa kufoji cheti na unamnyima kila kitu wakati miaka yote hiyo ulitumia huduma yake. Unataka kutuaminisha cheti chake ndo kilikuwa kinaendesha mabosi au yeye kama yeye......yaani wewe umwajiri mtu halafu baada ya miaka 30 ndo ugundue hakufaa kuajiriwa na unamyima stahiki zake zote, huu unakuwa zaidi ya uzwazwa..
Uaminifu wake na umahiri wake haubadili kosa,bado kosa lipo pale pale mkuu:kagushi cheti na kajipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Yaani Watanzania dah!Our thinking capacity has much to be desired.
 
Michango yao waliyokatwa wakati wanatumikia umma ni Hali yao. Sasa kunashida gani, kwani hiyo mifuko wakibaki na hiyo michango wao ndio hazina? Wapewe stahiki zao waanzie maisha Basi. Hao ni watanzania, na ustawi wao ni muhimu pia hata Kama mfumo rasmi wa ajira umewatema.
Wanatakiwa kuilipa serikali mishahara na posho zote walizopata kwa njia ya udanganyifu pension walikatwa kwenye mishahara waliyopata kwa udanganyifu hiyo ni mali ya serikali.Pension zao ni mali ya serikali na wao wanatakiwa warudishe kila senti waliyolipwa toka walipoajiriwa na cheti feki na riba juu
 
Uongo vinginevyo hata mama Samia asingekuwa Raisi Wahuni wangemgomea.Sheria ndizo zimemuweka pale
Hata nyumbu wanazo sheria, wakianza kudumbukia mtoni ni wote bila kujali ndani kuna nn.. Ila kuna tofauti kati ya sheria za nyumbu na ss binadamu ndio maana kuna misamaha ya raisi baada ya sheria kuhukumu.
 
Sheria zenyewe hizi zilizopelekwa bungeni kwa hati ya dharula?
Kama kushitakiwa kuzuri kwanini viongozi wako wamejitengenezea Kinga zakisheria wasishitakiwe kwa kosa lolote?
Ifike muda na sisi kama raia wa kawaida tuwe tunateteana.
Afadhali wewe umeongea kitu, siyo kupinga kila kitu ni ujuha maana hata polisi ni mlinda sheria ila ukikaa vibaya anakuumiza.
 
Kosa la kudanganya na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu lipo pale pale mkuu.Umepata fedha kwa njia ya udanganyifu!And than mambo mengine ni ya ajabu sana,wewe una-matatizo gani mpaka utumie cheti cha mtu mwingine?Mwenzio kasoma mpaka kafika point X ,halafu wewe unadandia juu kwa juu,huoni kwamba hilo ni kosa!

Nirudie,Watanzania inabidi tubadilike,our moral values are way too low.
Kwa hiyo malipo hayo, ulitaka alipwe nani, ambayo huyu ameyafanyia kazi? Huyo aliye soma mpaka point x? Kila Mtu anakuwa paid for their service, nataka ufafanue upande huu wa kazi ya huyu mwenye cheti feki! Kama alifanya kazi nzuri, amefundisha na wanafunzi wamefaulu, unafanyaje hiyo huduma yake? Utawatafuta watoto aliowafundisha ufute hiyo elimu kwenye vichwa vyao? Au kamtibu mgonjwa akapona, utaurudisha ugonjwa?!
Pia, moral values za Watanzania unao wazungumzia ni pamoja na wewe mwabudu #yesuwalugola, au Wewe ni Mrundi?
 
Hebu pata mawaidha ya huyu mdau hapo chini alafu endelea na ujuha wako!
Kuua watu , kuteka kufunga ,kwenye viroba , kuzuia uhuru wa vyombo vya habari , demokrasia , ukiukaji mkubwa sana wa haki za binadamu , ubambikiaji kesi za uonezi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha sio kuvunja sheria , jamani watu wametumikia kazi Wana jasho lao walipwe .
👇🏾
Huyu ndio wale wale binti yake wa miaka 14 anatiwa mimba na Fataki, halafu fataki linakuja kumuomba msamaha na kumpa hela anasamehe sababu ni swala la ubinadamu bila kujua mwenzake ndio kazi yake hiyo kuharibu watoto wa wenzake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria zipo kwa ajili ya binadamu sio binadamu kwa ajili ya sheria, ndo maana huwa tunahalalisha misamaha ya raisi baada ya hukumu.
Usiongozwe na roho ya aina hiyo, haitakupeleka popote katika siku zako za kuishi.
Basi katiba iliyopo iendelee Rais abaki na madaraka kama yote, na akiamua kuendelea abaki.
Huwezi kufunika sheria kisa ubinadam.
Sheria lazima zifuatwe.
 
Wanatakiwa kuilipa serikali mishahara na posho zote wlizopata kwa njia ya udanganyifu pension walikatwa kwenye mishahara waliyopata kwa udanganyifu hiyo ni mali ya serikali.Pension zao ni mali ya serikali na wao wanatakiwa warudishe kila senti waliyolipwa toka walipoajiriwa na cheti feki na riba juu
Tupo pamoja Yehoyadaya katika hili.Kila hela waliyolipa kutoka kwenye mishahara yao kwenye Social Security Funds ni mali ya serikali kwa hiyo wasilipwe mafao.

Furthermore hela yote waliyolipwa kwa miaka yote interest iwe calculated walipe,pamoja na kulipa mishahara yote waliyolipwa.

Watu wanaiba fedha zetu halafu eti walipwe mafao.Mwishoni tuta-ambiwa warudishwe kazini na muda wote ambao hawakulipwa walipwe with disturbance allowance!Inaudhi frankly.
 
Uaminifu wake na umahiri wake haubadili kosa,bado kosa lipo pale pale mkuu:kagushi cheti na kajipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Yaani Watanzania dah!Our thinking capacity has much to be desired.
Miaka yote hiyo mwajiri anakuwa wapi kufanya verification ya credentials za huyo mwajiriwa...ina maana kama umemwacha aendelee kukufanyia kazi ina maana amekidhi vigezo na matarajio yako, hivyo huna sababu ya kumnyima chochote anachostahili.
 
Mimi sija-ungunga elimu yangu lakini siungi mkono swala hilo.Mtu aliye-gushi cheti na kufanya kazi amefanya makosa mawili:
1.Kugushi cheti,kosa ambalo ni prosecutable by law,
2.Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kosa ambalo pia ni prosecutable by law.

Sasa tuwe wakweli tu, mtu kama huyo analipwa mafao,si alitakiwa kupelekwa mahakamani in the first place.

Kiukweli maamuzi ya kuwalipa hawa watu hayaja-zingatia sheria,weledi na yana-set an extremely bad precedent.

Tunaomba Rais afikirie upya maamuzi yake,yanachangia moja kwa moja katika kuiharibu jamii yetu morally.
amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wakati amefanya kazi ya halali?!...kwani serikali ilishindwa kuwagundua tangu mwanzo?!...unasubiri mtu afanye kazi miaka 40 ndo unamfukuza eti ana vyeti feki wewe unaona ni maamuzi ya busara hayo!?....mtu katumikia taifa alipwe stahiki zake kisha serikali iwe makini isiajiri tena watu wa aina hiyo wakati mwingine.....acheni roho mbaya kisa tu tangazo la rais limeenda kinyume na msimamo wa rais aliyekufa....kauli yake haikuwa neno la mungu..
 
Basi katiba iliyopo iendelee Rais abaki na madaraka kama yote, na akiamua kuendelea abaki.
Huwezi kufunika sheria kisa ubinadam.
Sheria lazima zifuatwe.
Hapa sasa unafikiri kama mnyama. Kwamba sababu nimesema sheria zipo ila ubinadamu pia upo basi tuachane na sheria tufate ubinafamu. Tofauti yetu ss na wanyama ni uwezo wa reasoning na busara....
 
Kwa hiyo malipo hayo, ulitaka alipwe nani, ambayo huyu ameyafanyia kazi? Huyo aliye soma mpaka point x? Kila Mtu anakuwa paid for their service, nataka ufafanue upande huu wa kazi ya huyu mwenye cheti feki! Kama alifanya kazi nzuri, amefundisha na wanafunzi wamefaulu, unafanyaje hiyo huduma yake? Utawatafuta watoto aliowafundisha ufute hiyo elimu kwenye vichwa vyao? Au kamtibu mgonjwa akapona, utaurudisha ugonjwa?!
Pia, moral values za Watanzania unao wazungumzia ni pamoja na wewe mwabudu #yesuwalugola, au Wewe ni Mrundi?
Malipo gani,hiyo ni mali ya serikali mkuu.Halafu ni maswali gani hayaa!
 
Mwalimu asiye na cheti cha ualimu alifanya kazi gani ya maana? WAtoto walikuwa wakimaliza shule za msingi wengi hawajui kusoma wala kuandika kwa sababu yao

Utendaji maofisini ulijaa ubabaishaji sababu ya hiyo mijitu ya vyeti feki

Sasa hivi wenye vyeti halali wameshika nafasi ufaulu uko juu na nenda maofisini baada ya mijitu yenye vyeti feki kuondoka huduma ziko vizuri
Kwa hiyo malipo hayo, ulitaka alipwe nani, ambayo huyu ameyafanyia kazi? Kila Mtu anakuwa paid for their service, nataka ufafanue upande huu wa kazi ya huyu mwenye cheti feki! Kama alifanya kazi nzuri, amefundisha na wanafunzi wamefaulu, unafanyaje hiyo huduma yake? Utawatafuta watoto aliowafundisha ufute hiyo elimu kwenye vichwa vyao? Au kamtibu mgonjwa akapona, utaurudisha ugonjwa?!
 
Hapa sasa unafikiri kama mnyama. Kwamba sababu nimesema sheria zipo ila ubinadamu pia upo basi tuachane na sheria tufate ubinafamu. Tofauti yetu ss na wanyama ni uwezo wa reasoning....
Ndo unyama unaomaanisha, limekuchoma.
Sheria zifuatwe over.
 
Back
Top Bottom