Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao

Shida mkuu ni pale ambapo najiuliza ni raia gani wa kawaida mwenye ujasiri wa kuingia ndani ya basi mchana kweupe na kumfunga mtu pingu huku wakiwa na silaha za moto?

Ingekuwa ni suala la visasi vya kifamilia basi ingekuwa wanaviziana tu lakini sio kumfunga mtu pingu mchana kweupe mbele ya umati wa watu.
Najiuliza sana, tusubiri tuone.
 
Umeambiwa walikuwa na cruiser mbili za kazin kwao, wakaiblock bus wakashuka na mabunduki mchana kweupe, ndan ya bus siti ya mbele kabisa alikuwepo police wa usalama barabarani aliwaona wanachokifanya na nadhani aliwatambua maana wanatambuana, akawaruhusu wala kuwahoji wakatekeleza majukum yao yaliyowaleta... Wakamchukua mzee wakatokomea nae. Hapa unataka kutuaminisha nin kwamba serikali haijui inachokifanya ama kinachofanyika mpaka sasa?
Wanaotekwa na kupotezwa ni wengi sana labda nikwambie hao wanaotekwa na ukawasikia kwenye vyombo vya habari ni wale maarufu wenye majina na wenye wanaowasemea ila wanaopotea ni wengi sana kwa sitaili kama hii. Usikute hata hii coment yangu ikawachefua wakanitafuta kimya kmya wakanipoteza kmya kimya na msinione tena online
 
Naanza sasa Kuhisi kuwa huenda kuna Watu wana Bifu zao ama za Kibiashara au Kisiasa na hata Kifamilia na Watekelezaji wa kumsaidia Israeli kufanya Kazi yake tukuka ya Kuzima Pumzi zetu za Duniani wakatumia Lifti ya Taasisi fulani inayolaumiwa kila Siku kuwa Wao ndiyo Wamesaidiana na huyo Israeli.
Usilete utani kwenye mambo serious.
 
Maswal kichwani mwangu ni mengi sana ila na mm niseme tuuu pasipo kujalisha stori zilizopo nitakuwa wa mwisho kuamini POLISI TANZANIA ndio walofanya tukio hili la kuondoa uhai wa binadamu mwenzangu.

Narudia tena.
Nitakuwa wa mwisho kuamini.
 
Binafsi hili tukio limenipa mshtuko na simanzi sana. Nakosa chakusema zaidi ya uchungu.

Lakini kutokana na mengi yanayosemwa juu ya utekwaji wa Mzee wetu, hakuna aliyebahatika kupata picha ya yale mazingira ukiachilia mbali CCTV za kwenye bus?
Raia hawakufanikiwa kabisa kupata picha Kwa simu zao? Naelewa mazingira hatarishi kama ingedgundulika unapiga picha, lakini haijapatilana picha yoyote hata wakiwa wanatoka nae kwenye gari au kuingia nae kwenye magari Yao?

Ni baadhi ya maswali yanayoweza kutusaidia kutafakari zaidi.

Na endapo wao hawajahusika na hawawafahamu waliohusika, basi nchi ipo kwenye hali mbaya zaidi ya hatari tunayoifikiria.
 
URAIS NI TAASISI KUBWA SANA, HAIMAANISHI KILA LITAKALOFANYWA RAIS ATALIFAHAMU, KATIKA TAASISI HIYO HUWA NA VITENGO MBALI MBALI, NAKATAA YA KWAMBA RAIS HUYU
ETI ANAYAFAHAMU HAYA MAUAJI NAKATAA KWA NGUVU ZOTE, ISPOKUWA NADHANI VIPO VITENGO VINAVYOFANYA KAZI KWA MIHEMKO, BILA KUTUMIA WISDOM ENTELEGENCY, NA HILI NI HATARI SANA.
 
Zingatia location ya matukio pendwa-Ununio/Mbweni.
Kwa namna walivyosafirishwa Sugu na Mnyika kutoka Mbeya kwenda Makambako,hapana hawa ndugu zetu Polisi bila shaka ni wao!

Lakini nadharia nyingine ni Wazee wa Eagle house,Mama kawavuruga sana inawezekana Kuna zengwe wanamchezeshea!!
 
Kaka kila mtu na mtazamo wake ni sawa. Ila mimi bado nakazia kwa mashuhuda, wamemtaja traffic, namba yake kuwa alikaa siti ya mbele wakamtambua vizuri. Na wabongo kwa mambo hayo wako vizuri kufatilia, wameona yote.

Kikawaida inaweza kuwa ngumu kuamini. Ila inaonyesha hali ni mbaya sana, kuliko tunavyodhani. Ni kwamba wanakuchomoa popote na unamalizwa, mtawafanya nini? Nenda kasome walivyojichanganya kwenye masaa, huitaji hata kuwaza mara mbili.
 
Binafsi hili tukio limenipa mshtuko na simanzi sana. Nakosa chakusema zaidi ya uchungu.

Lakini kutokana na mengi yanayosemwa juu ya utekwaji wa Mzee wetu, hakuna aliyebahatika kupata picha ya Yale mazingira ukiachilia mbali CCTV za kwenye bus...
Haya mambo wanafanya vyombo vya ulinzi na Usalama, nchi hii huwezi fanya jambo baya kama lile la kuchafua taswira ya nchi wakakuacha salama tena mazingira ya wazi vile
 
Rejea taarifa ya Tanga,Polisi walikaa na mtu 29 days watu wanamtafuta ndugu yao wanaambiwa hayupo.
 
Haya mambo wanafanya vyombo vya ulinzi na Usalama, nchi hii huwezi fanya jambo baya kama lile la kuchafua taswira ya nchi wakakuacha salama tena mazingira ya wazi vile

Nakuelewa sana Mkuu, Kwa vyovyote vile itakavyokua, iwe ni vyombo vya usalama vimehusika au havijahusika, Bado hawawezi kujikwamua na lawama za hili janga na yote yanayoendelea.

Lakini maswali yangu pia yazingatiwe kutupatia pa kuanzia, lilikua ni bus la kampuni Gani, namba zake za usajili pia ni muhimu sana. Hapo ni kama hakuna raia aliyefanikiwa kupata picha ya wakati wa tukio la kumkamata Mzee wetu.
 
Nakuelewa sana Mkuu, Kwa vyovyote vile itakavyokua, iwe ni vyombo vya usalama vimehusika au havijahusika, Bado hawawezi kujikwamua na lawama za hili janga na yote yanayoendelea...
Taarifa zote hizo zinafahamika na mabus mengi siku ya CCTV camera
 
Nipo sambamba na wewe kiongozi, kwenye mtandao ya kijamii au popote pale Kuna taarifa za Hilo bus alilopanda Mzee wetu?
Screenshot_20240909-083321.png
 
Huenda Waganga wa kienyeji wakawa wahanga wa Majibu ya Maagizo.
Changamoto tu ni kuwa majibu ya maagizo yatapatikana lini?!
 
Back
Top Bottom