Rais Samia aagiza waliokuwa wanaishi Bonde la Mto Msimbazi kinyume na sheria kulipwa Tsh. Milioni 4 kila mmoja

Hiyo milioni nne na kazi za uyaya hakuna tofauti.

Awamu hii raia wanadharaulika mno.
 
Hapa kuna upigaji unaenda kutokea.
 
Lineup tayari kupata pesa

View: https://www.instagram.com/p/CztYIWjvScj/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
Amewahurumia kama binadamu ila wangekutana na mtu kama Jiwe wangeisoma namba 😂😂
Jiwe angewakurupusha tu, mbiombio, aliselema alija, "tulisha waambia kitambo maeneo haya ni ya hatari na serekali yenu ilishakutengeeni maeneo pale mabwepande matokeo yake mkayauza, sasa ondokeni hakuna cha lelemama, hatuwezi kuongea na watu ambao pengine ni wakorofi, nakupeni siku 3,muwe mmeondoka!
 
Mbona mnapenda kutufanya sisi ng'ombe nyie sio kwamba raisi ameamua watu walipwe mil 4!!?? World Bank ambao ni miongoni mwa watoa fedha za mradi wameagiza watu walipwe fidia no matter what. Hv hii dunia ya information zote bado mnathubutu kutudanganya!!?
 
Waulizwe hao world Bank tujue mbivu na mbichi !!
 
Upigaji na uchaguzi hamna suluhisho la kudumu hapo ni kucheza danadana tu
 
Ila bora Samia, marehemu bichwa angewafukuza kwa kutumia jeshi na hata mia wasingepata
Kwani mbona miaka yote ya utawala wake mbona haliwaacha?hata hivyo hiyo milioni 4 nisawa na bure maana hauwezi pata kiwanja Cha milioni 4 hapa Dar.
 
Anuani zao hao World Bank zipo kwenye Google ni bora wajulishwe kinachoendelea labda itasaidia !
Tutawafikishia taarifa haiwezekani baadhi ya watu wana hati halali alafu umlipe mtu milioni 4 eneo lipo karibu na lami limezungukwa na maduka fidia ya ardhi umlipe mtu milioni 4!!???huo ni uonevu wa mchana kweupe. Serekali hii madeni ya wazungu mabilioni wanalipa haraka haraka fidia ya wanachi wake inawalipa kiduchu tena baada ya mlolongo mrefu!?
 
Kiwanja Dar ni shs ngapi? yeye akipewa 4M anaweza kujenga nyumba ya kuishi na kununu kiwanja Dar? wakati hao wananchi wana nunua na kujenga serikali ya CCM ilikuwa wapi? ni kutafuta sifa za hovyo bila sababu za msingi.
Wengi walivamia... Hivyo hata kulipwa fidia ya ardhi ya 4M + mengineyo ni fadhila kubwa!
 
Mh, hii nchi ngumu sana, ili uweze kuishi ni lazima ujizime data a.k.a usitumie akili! Mpaka leo kimya! Hayo majibu yao sasa!

Wakazi wa Bonde la Mto Msimbazi Kulipwa Fidia Kupisha Uendelezaji wa Bonde hilo​


Hayo yamejiri leo Novemba 15, 2023 wakati Waziri wa Nchi Ofisi Rais TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila alipokutana na wakazi hao katika viunga vya Ofisi za Young African Ilala Jijini Dar es Salaam

Akiongea na Wananchi hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa Kauli ya Serikali ya kuwalipa wakazi hao kuanzia kesho Novemba 16, 2023 ambapo hadi sasa asilimia zaidi ya 92 wameshahakikiwa wanasubiri kulipwa.


Source: Mwanzo › new › wakazi-wa


2400 kulipwa fidia bonde la Msimbazi kesho​


15 Nov 2023 — Amesema “leo hii nimekuja hapa kutoa Tamko ya hatua ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi uanze mara moja kuanzia sasa na hii iende sambamba ...


Source: Timesmajira › 2400-kuli..
 
Huko Kipunguni wametapeliwa na Waziri kabisa yaani ! Hawaamini Macho yao ! usicheze na ccm wewe !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…