Rais Samia aagiza waliokuwa wanaishi Bonde la Mto Msimbazi kinyume na sheria kulipwa Tsh. Milioni 4 kila mmoja

Rais Samia aagiza waliokuwa wanaishi Bonde la Mto Msimbazi kinyume na sheria kulipwa Tsh. Milioni 4 kila mmoja

Mlisikia wa Jangwani, ndio walipewa viwanja mapwe Pande.


Hawakupewa viwanja watu wote huko mabwepande, naona watu wanapotosha

Waliopewa viwanja ni wale Ambao nyumba zao zilikua zinafikiwa na Maji

Huu mradi wa World Bank unaenda kuchukua eneo lote la mto Msimbazi hata kama nyumba yako ilikua haipati mafuriko kwa fidia/ posho ya aina moja
 
Kiwanja Dar ni shs ngapi? yeye akipewa 4M anaweza kujenga nyumba ya kuishi na kununu kiwanja Dar? wakati hao wananchi wana nunua na kujenga serikali ya CCM ilikuwa wapi? ni kutafuta sifa za hovyo bila sababu za msingi.
LAKINI HIVI ATHARI ANAPATA NANI? MIMI NDIYO NINGEKUWA SERIKALI NAWAACHA TU MI NAENDELEA NASHUGHURI ZANGU WAKIZAMA SHAURI YAO
 
Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa amesema kuwa Serikali itaanza kuwalipa wakazi wa Bonde la Mto Msimbazi Tsh. Mil 4 kila mmoja kama sehemu ya fidia ili wahame eneo hilo. Malipo haya yataanza kufanyika kuanzia Novemba 16, 2023.

===


Hisia mchanganyiko za wakazi wa bonde la Mto Msimbazi kufuatia tamko la Serikali kuwa watalipwa fidia ya ardhi ya Sh4 milioni kwa kila mwenye eneo, imeibuka huku wengine wakiunga mkono uamuzi huo, na wengine wakiupinga.

Awali kulikuwa na malalamiko ya wakazi hao baada ya kuonekana kuwa watafidiwa nyumba zao na si vinginevyo. Kassim Said amehoji iweje wananchi wa Loliondo wao walilipwa vizuri na kujengewa hadi nyumba lakini wao wanaokaa mjini wanapewa kiasi hicho kidogo cha fedha?

"Kwa mfano mimi nyumba yangu ya vyumba vitatu nimelipwa Sh11 milioni nikichanganya na hiyo Sh4 milioni ina maana nina Sh15 milioni, niambie naweza kujenga nyumba ya kiwango hicho hapa mjini? Ngoja tumwachie Mungu yeye ndio anajua," amesema Said.

Lakini hali ni tofauti kwa Siasa Mtambo, ambaye ameridhishwa na uamuzi huo, kwani kwa muda wa miaka 30 amekuwa akiishi kwa tabu katika eneo hilo kutokana na ukweli kuwa hakuwa na uwezo wa kwenda kujenga sehemu nyingine, pengine kwa hicho kidogo walichopewa ataweza hilo kulifanya.

Aisha Sharif mmoja wa wananchi waliokataa fidia kutokana na kutoridhishwa na tathimini, amesema kilichomfurahisha ni kitendo cha Waziri huyo kuahidi kuwasikiliza wote waliokataa pendekezo hilo.

"Hao waliokubali waachwe walipwe kwa kuwa kila mtu anajua thamani ya nyumba yake wengine kuliko tulipwe hiyo hela ni bora tuendelee kubaki hapa mjini," amesema Aisha.

Haya yote yanajiri baada Waziri wa Tamisemi, Mohammed Mchengerwa alipokutana na wananchi hao leo Jumatano Novemba 15, 2023 katika viwanja vya jangwani jijini humo, na kutangaza kuwa kesho (Alhamisi) Serikali itaanza kulipa fidia ya Sh4 milioni kwa kila mwenye ardhi itaanza kulipwa kesho.

Kimsingi, wananchi hao walikuwa na malalamiko wakitaka aina mbili za fidia kufanyika, ile ya nyumba pamoja na hiyo ya ardhi, jambo ambalo awali Serikali ilikubali kuwafidia nyumba pekee.

"Tulisikia malalamiko yenu kupitia nyie wenyewe, viongozi wenu akiwemo Mkuu wa Mkoa, Madiwani na Wabunge, nami nikalifikisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kwa kuwapenda jana ameridhia kila mwananchi anayepisha mradi huu alipwe Sh4 milioni kama kifuta jasho kwa ardhi aliyoimiliki.

"Kwani kama mlivyosikia wataalam wetu hili walisema ni eneo la ardhi owevu hivyo kisheria halikupaswa kulipwa fidia kwa kuwa sio salama kwa makazi, lakini kwa huruma ya mama amemua mlipwe hiyo Sh4 mlioni,” amesema Mchengerwa.

Sambamba na hilo la ulipaji fidia hiyo ya ardhi ambayo kimsingi ni tofauti ile fidia ya jengo, Waziri huyo aliagiza pia Mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), kuanza mara moja ujenzi wa mradi huo huku malipo ya fidia yakiendelea ili kupunguza adha ya mafuriko katika eneo hilo yanayoathiri shuguli za kila siku za wananchi.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alisema anachojua mkoa huo hauna mafuriko isipokuwa watu ndio wameziba njia zinazopitisha maji kwa kujenga na kuishi maeneo ambayo maji yanapaswa kupita.

Chanzo: Mwananchi

Hao wananchi waje huku Igangabilila kuna plot za kuhesabu miguu, milion 2 unajenga
 
Hakuna cha kupinga wala kuleta kelele wamepewa hiyo milioni 4 kwa ajili ya ardhi, kisha nyumba inathamininiwa, nimeona mtu hapo kapata milioni 15, ardhi milioni 4 na nyumba milioni 11.

Sio lazima wake dar(mjini) nje ya dar kuna maeneo makubwa tu kwa bei nzuri tu, mkuranga hapo heka milioni 2+ na lina mimea fresh tu.
Kama ni hivyo imekaa vizuri.
 
Back
Top Bottom