Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Watz tuache roho mbayaa,watu wapewe Chao,kwani nani aliwaajiri? wengine ni marehemu sahii.
 
Tulipwe tu kwakweli mama anaupiga mwingi ccm oyeeeeh
haaha dah hongereni sana kwa hilo .

Nakumbuka nilikuwa SHRO ofisi flani nikamsaidia jamaa kupata ajira alikuwa ni dereva mzuri sana alikuwa ananiendeshaga nikiwa na safari zangu binafsi za mikoani.

Yaani mzur sana kwani pia alikuwa fundi wa ishu ndogo ndogo za magari na leseni nzuri na cheti cha NIT lakini alikuwa hana cheti cha form four na tulikuwa tunahitaji madereva 5 pale ofisin nilimwambia jamaa ajiongeze atengeneze cheti cha form 4 feki kweli jamaa akaniletea baada ya kama siku 2 hivi nikamshortlist kwenye usaili na nkamsaidia ilikuwa miaka ya 2000 huko,
jamaa alikuwa smart sana akapanda cheo hadi kuwa principle driver na CEO wa hiyo taasisi alimpendekeza awe dreva wake.
Ishu ya vyeti feki ilivyoibuka naye akapatikana cheti chake cha form four feki nikamatafuta wenye simu akaendelea kunishukuru sana kwani alinieleza ile ajira ilimsaidia kupata nyumba 2 na kuhudumia familia yake vizuri pamoja na kufumfungulia mke biashara ya bucha la samaki. Nilimuoneaa huruma sana nikifiiria mimi ndiye niliyemuelekeza akatengeneze cheti feki
Ngoja kesho nijaribu kutafuta namba yae kwa wadau wa pale kama watakuwa nayo nimsalimie.

Kwa mujibu wa Penal Code yetu hilo kosa lipo hivi nahisi Samia atakuwa ametumia hiyo bolded part kudeal na hii ishu

Punishments for Forgery 337.
"Any person who forges any document is guilty of an offence which, unless otherwise stated, is a felony, and he is liable, unless owing to the circumstances of the forgery or the nature of the thing forged some other punishment is provided, to imprisonment for seven years."

wa Ma HR wote waliozembea kukagua vyeti penal code inaeleza hivi sio kosa kubwa
Neglect of official duty 121.
Every person employed in the public service who wilfully neglects to perform any duty which he is bound either by common law or by Statute or Ordinance to perform, provided that the discharge of such duty is not attended with greater danger than a man of ordinary courage and activity might be expected to encounter is guilty of a misdemeanour.
 
hata sijui umeandika kitu gani. Nimeonyesha kua SAA walimfukuza Ribani baada ya kugundua kuwa alikuwa akirusha ndege kwa miaka 20 huku akitumia cheti cha kufoji. Halafu wakamtaka arudishe hata malipo aliyolipwa kwa kutumia checti hicho cha kufoji ingawa hakuwa kusababisha ajali yoyote. Wakasema ile kutumi chetio cha kufoji tu ni kosa kubwa sana. majibu yako yamekuja bila kuwa na mwelekeo wowote.
 
Ni watanzania wenzetu walifanya wao kazi kwa kutumia akili zao na nguvu zao. Vyeti havikufanya kazi bali viliwawezesha kupata kazi. Ni SAHIHI WALIPWE
Kwa hiyo hawakustahili kufukuzwa kama vyeti ni irrelevant
 
Napenda sana watu mnaojua kuelezea Habari, Hongera Kwa Moyo mwepesi mkuu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Walipwe,mwendazake hesabu zake zilikuwa za dhuluma sana mfano unawapandishaje madaraja watumishi bila kupandisha mishahara pia?!
 
Neno HAKI kwa Lugha yetu inaonekana halieleweki vizuri....

Mtuhumiwa uliyemtuhumu kwa Cheti Feki,, leo unamlipa Mafao...
Kama alichofanya kilikuwa ni sahihi kwanini usimrudishe kazini aendeleee... na wale ambao hawakustaafu na wana vyeti Feki nao walipwe..?


Au mm ndio sijaelewa alichosema?
 
Kama ameshindw kuongeza mshahara . Ataweza hili.. ?😂
 
Tuache porojo!! Mchakato wenyewe nao ulikuwa FAKE na wa KIBAGUZI.. marehemu aliamua chagua wanyonge na kuwanyonga...
Mbona hakwenda vyombo vya dola!? Nijibu hili swali tuone!? Ita MATAGA wote uone kama watajibu hili!

Mama walipe pesa zao zotee...
 
Huenda Tatizo lako ni kukosa ajira, kama ndivyo nakuelewa.
 
Je ! Ni sahihi kutowalipa ilhali walikatwa pesa zao na walilitumikia taifa kwa haki!??
Walitumikia taifa kwa haki ipi? Umeshawahi kuwaza ni watu wangapi wenye sifa walikosa kazi kwa ajili yao? Udanganyifu ni kosa kama makosa mengine ya jinai
 
Sasa kama hao unaowaita covid 19 unaona walipata ubunge isivyo halali sasa wanatofauti gani na hawa vyeti feki? Maana na wao walipata hizo kazi isivyo halali.
 
Feki wapi we bwege..wakati watu waliajiriwa na mamlaka sahihi!?
Waliajiriwa kwa kuzidanganya hizo mamlaka sahihi. Ni sawa uende benki ugushi cheki ulipwe, baadae ukikamatwa useme nililipwa na mamlaka sahihi Kwahiyo sina kosa.
 
Waliajiriwa kwa kuzidanganya hizo mamlaka sahihi. Ni sawa uende benki ugushi cheki ulipwe, baadae ukikamatwa useme nililipwa na mamlaka sahihi Kwahiyo sina kosa.
Mfano ulioutoa wa cheki ya Benki hauendani na maudhui ya maelekezo ya mama. Tunaongelea haki zao siyo kurudi kazini
 
Ujue kuna waliofoji hadi digrii

Chukulia mtu form four division zero alifoji digrii ya udaktari watu wangapi watakuwa wakifa mikononi mwaka kwa kufanya kazi isiyostahili

Kiwango cha watoto kufeli kilikuwa kikubwa mno huko nyuma sababu ya hao walimu wavyeti Feki mtoto anamaliza darasa la saba akiwa hajui kusoma wala kuandika sababu huyo mwalimu chetu Feki hajawahi kanyaga chuo cha walimu

Kumlipa chochote ni uhuni alitakiwa huyo mwenye cheti feki aburuzwe mahakamani afilisiwe na kurejesha peas zote aliyowahi lipwa kama mshahara au posho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…