Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Lakini si waliajiriwa na Serikali yenyewe?
Walikuwa wanazalisha na kuchangia pato la Taifa,walikuwa wanakatwa kodi ambayo ilikuwa inaendesha shughuli za serikali harafu Serikali inawafukuza bila huruma?
Kwa uharifu wao hawawezi kurudishwa kazini kwa sababu hawana sifa lakini serikali iwalipe mafao yao.
 
Unajua sheria ingefata mkondo nani angeshitakiwa na kuhukumiwa ?kama ni stahiki zao mahakama si zipo kwanini hawajaenda?
 
Common sense ukijumlisha na sheria unadhani nani wakulaumiwa na nani mwenye makosa
Taratibu za kuajiri zinamtaka mwajiri kujithibitishia uhalali wa nyaraka za muajiriwa.
 
Una uhakika hawaijui??? ..unaelewa experiential learning???..wangekuwa hawaijui wasingezalisha,kampuni zingekufa kibudu...natural death....Mama Samia hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Unafikiri kabla hiyo experience hawajaipata wangapi waliumia au kufa kabisa?
 
Unajua sheria ingefata mkondo nani angeshitakiwa na kuhukumiwa ?kama ni stahiki zao mahakama si zipo kwanini hawajaenda?
Kwanini serikali haijaenda mahakamani?
 
Mkuu kama umesaha walipewa nafasi ya kukata rufaa kama kuna waliofukuzwa kimakosa
Na wapo wenye kasoro kama ulizotaja walikata rufaa na kurudi kazini
 
Unajua sheria ingefata mkondo nani angeshitakiwa na kuhukumiwa ?kama ni stahiki zao mahakama si zipo kwanini hawajaenda?
Hizo ni assumption zako wewe. Sheria ingefuata mkondo kungekuwa na kesi kisha hukumu ingetoka ambapo ingetegemeana na hati ya mashtaka aliyoifungua mwajiriwa husika.

Suala la hukumu ingekuaje hilo haliwezi kuthibitishwa kwa wewe kufanya assumptions kuwa hukumu ingetokaje maana JF sio mahakamani hata kama wewe ni jaji wa mahakama kuu na unaijua sheria vilivyo.

Ukumbuke mazingira ya hivyo vyeti feki hayafanani kwa wote. Serikali iliwagroup pamoja sio kwa sababu wote walifanana ila sababu nia ilikuwa ni kupunguza gharama ya mshahara bila kuibuka kwa gharama nyingine za fidia ya kuondoa watu kazini na wakaruhusiwa kwenda mahakamani kama unahisi umeonewa... LAKINIIII
Ulitegemea mwajiriwa aende mahakamani kumshati
Mwajiri wake ambaye ni amiri jeshi mkuu ambaye ni JPM? Hahahaha.

HILI JAMBO SAMIA ATALIMALIZA VIZURI SANA AKIWAPA HIZO 5%. ITAKUWA NI WALIFANYA MAKOSA, SERIKALI IKAFANYA MAKOSA KUWAPA AJIRA, SERIKALI IKAWAADHIBU BILA KUJALI HAKI ZAO NA SERIKALI IKAJISAHIHISHA KWA KUREKEBISHA KIWANGO CHA ADHABU. HUTOSIKIA TENA MALALAMIKO NA LAWAMA SABABU MAKOSA NI KWELI YALIFANYIKA.
 
Hata wenye maarifa stahiki mbona hata faida zao hatuoni!?
 
Unafikiri kabla hiyo experience hawajaipata wangapi waliumia au kufa kabisa?
Sasa hawa walio kuja kuokoa jahazi ndo wazuri sasa mkuu tunawaenzi na kuwapa moyo wa shukrani kwa kuokoa jahazi? au mie ndo sijaelewa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…