Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Rais Samia aagiza walioondolewa na Hayati Magufuli kwa vyeti feki walipwe

Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Lakini si waliajiriwa na Serikali yenyewe?
Walikuwa wanazalisha na kuchangia pato la Taifa,walikuwa wanakatwa kodi ambayo ilikuwa inaendesha shughuli za serikali harafu Serikali inawafukuza bila huruma?
Kwa uharifu wao hawawezi kurudishwa kazini kwa sababu hawana sifa lakini serikali iwalipe mafao yao.
 
Raisi wa awamu ya 5(RIP) aliposema anataka baadhi ya watu waishi kama mashetani alikuwa ameyaona wapi hayo mashetani yanavyoishi maana naona unataka kutumia neno shetani kuanzisha mdahalo.

Ukiadhibu kwa kumyang'anya mtu fedha bila kufuata utaratibu tuliojiwekea ili kiwango cha adhabu kilinganishwe na kosa kuhakikisha haki inapatikana unakuwa hujatumia ubinadamu, kinyume cha ubinadamu ni ushetani au Unyama. Ndo maana nikasema tusitoe adhabu kama mashetani.
Unajua sheria ingefata mkondo nani angeshitakiwa na kuhukumiwa ?kama ni stahiki zao mahakama si zipo kwanini hawajaenda?
 
Common sense ukijumlisha na sheria unadhani nani wakulaumiwa na nani mwenye makosa
Taratibu za kuajiri zinamtaka mwajiri kujithibitishia uhalali wa nyaraka za muajiriwa.
 
Ndiyo ni halali yangu kwakuwa nitauza nipate hela najenga majumbana kuwasaidia maskini!! km yangekuwa si halali wangenikamata nayo!! lkn nimepita nayo salalma ni halali yangu ndiyo! nitauza yangu yatatimia!!

kwani napiata nayo ili iweje??? nikauze nipate hela niishi vizuri baaasiL
Una uhakika hawaijui??? ..unaelewa experiential learning???..wangekuwa hawaijui wasingezalisha,kampuni zingekufa kibudu...natural death....Mama Samia hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Unafikiri kabla hiyo experience hawajaipata wangapi waliumia au kufa kabisa?
 
Unajua sheria ingefata mkondo nani angeshitakiwa na kuhukumiwa ?kama ni stahiki zao mahakama si zipo kwanini hawajaenda?
Kwanini serikali haijaenda mahakamani?
 
Kwanza kabisa, hatujui hata kama tuhuma ni za kweli, hatujui makubaliano ya ajira yalikuwaje.

Mchakato mzima umeendeshwa kibabe sana, watu hawakusikilizwa katika due process.

Kuna watu wamebadilisha majina tu wakaambiwa wana vyeti feki, ni wengi sana hawa.
Mkuu kama umesaha walipewa nafasi ya kukata rufaa kama kuna waliofukuzwa kimakosa
Na wapo wenye kasoro kama ulizotaja walikata rufaa na kurudi kazini
 
Unajua sheria ingefata mkondo nani angeshitakiwa na kuhukumiwa ?kama ni stahiki zao mahakama si zipo kwanini hawajaenda?
Hizo ni assumption zako wewe. Sheria ingefuata mkondo kungekuwa na kesi kisha hukumu ingetoka ambapo ingetegemeana na hati ya mashtaka aliyoifungua mwajiriwa husika.

Suala la hukumu ingekuaje hilo haliwezi kuthibitishwa kwa wewe kufanya assumptions kuwa hukumu ingetokaje maana JF sio mahakamani hata kama wewe ni jaji wa mahakama kuu na unaijua sheria vilivyo.

Ukumbuke mazingira ya hivyo vyeti feki hayafanani kwa wote. Serikali iliwagroup pamoja sio kwa sababu wote walifanana ila sababu nia ilikuwa ni kupunguza gharama ya mshahara bila kuibuka kwa gharama nyingine za fidia ya kuondoa watu kazini na wakaruhusiwa kwenda mahakamani kama unahisi umeonewa... LAKINIIII
Ulitegemea mwajiriwa aende mahakamani kumshati
Mwajiri wake ambaye ni amiri jeshi mkuu ambaye ni JPM? Hahahaha.

HILI JAMBO SAMIA ATALIMALIZA VIZURI SANA AKIWAPA HIZO 5%. ITAKUWA NI WALIFANYA MAKOSA, SERIKALI IKAFANYA MAKOSA KUWAPA AJIRA, SERIKALI IKAWAADHIBU BILA KUJALI HAKI ZAO NA SERIKALI IKAJISAHIHISHA KWA KUREKEBISHA KIWANGO CHA ADHABU. HUTOSIKIA TENA MALALAMIKO NA LAWAMA SABABU MAKOSA NI KWELI YALIFANYIKA.
 
Ni Mei Mosi ambpo Samia ametoa maagizo haya kuwa walioondolewa kwa vyeti feki enzi za Magufuli walipwe stahiki zao kama mafao ya kustaafu
Je ni sahihi kuwalipa hasa ikizingatiwa walitenda uhalifu kuingia kazini?
Bila kusahau hasara waliyoisababisha kwa kutoa huduma hafifu kutokana na kutokuwa na maarifa yanayotakiwa
Hata wenye maarifa stahiki mbona hata faida zao hatuoni!?
 
Unafikiri kabla hiyo experience hawajaipata wangapi waliumia au kufa kabisa?
Sasa hawa walio kuja kuokoa jahazi ndo wazuri sasa mkuu tunawaenzi na kuwapa moyo wa shukrani kwa kuokoa jahazi? au mie ndo sijaelewa??
 
Back
Top Bottom