jkipaji
JF-Expert Member
- Sep 22, 2019
- 6,963
- 9,401
Kwani Wazee si matibabu ni bure Tanzania nzima!? Na hata Kodi ya jengo wao hawalipi ni bure! Sasa hapa ndiyo sielewi Kama ni kweli matibabu kwa Wazee ni bure!!Kiongozi mzima wa nchi anatoa maagizo ya kibaguzi kwa kuwagawa wananchi kwamba hawa wapewe huduma hii wale wengine wasipewe eti kisa tu wamefiwa! Sasa hao amesikia msiba wao je wale wengine ambao hakusikia masaibu yaliyowakuta na wafanyeje wakati nchi yao ni hii hii na Rais wao ni yeye? Viongozi waache unafiki na waache ubaguzi kwa sababu huko mitaani kuna wazee kibao ambao hali zao mbaya na hawana watu wa kuwasaidia kiafya wala mahali pa kulala pia wapo watoto wengi sana wanaohitaji matibabu wazazi wao wamebaki kuzurura mitaani na kwenye vyombo vya habari kuomba misaada bila mafanikio.
Binafsi natoa wito kwa serikali kuboresha zaidi sekta ya afya kwa kuwekeza zaidi katika vifaa tiba,wataalamu wa afya na huku wakiweka gharama ambazo wengi watazimudu na pale inapotokea wachache miongoni mwetu wameshindwa kulipia gharama za matibabu basi kuwe na utaratibu maalum wa kuwasaidia kupata matibabu kama wengine lakini hii tabia ya kujifanya mwema kwa watu wachache tena bila ya vigezo vilivyo wazi,usikute ni kutokana na uhusiano binafsi kwa mmoja wa hao marehemu ndio kigezo kilichotumika.