Rais Samia aagiza Waziri wa Biashara kudhibiti Wageni kufanya biashara za Machinga, ahoji vijana wetu watafanya kazi gani?

Sio biashara tu ata ajira leo hii kumejaa watu hadi level ya degree na masters kutoka nje wakati wabongo wanasugua benchi tu
 
Huu ni uoga wa viongozi. Dunia ni kijiji, unaweza kwenda popote ukafanya kazi. Tunahitaji wageni sana watakaofanya kazi hadi za machinga.
Yeye alienda Uarabuni kwa mabwana zake kuwaombea watanzania kazi za ndani (beki 3).
 
Amechelewa. Yaweza kuwa gea ya kusaka kura na kupumbaza wadanganyika tu.
 
Una mawazo finyu sana
Acheni uoga na uvivu. Unahisi mchina atakudhibia ridhiki?
Huo uoga kwasababu viongozi wako wameendekeza rushwa, ubadhirifu, ufisadi, kupindisha sheria na kuwa na katiba mbovu ndiyo maana unaona kama wachina wamekudhibia ridhiki.
Mwaka 2025 viongozi wanaenda kuzindua maji kwenye kijiji fulani ambacho kisima ni milion 10 halafu gari la kiongozi ni milioni 25
 
Awaache tu hao wageni wafanye hizo biashara. Maana hao vijana wake anao wazungumzia, tayari wameshagundua biashara ya UCHAWA, na ambayo kwao ndiyo inalipa zaidi kuliko hiyo biashara ya umachinga.

Imagine kijana kama Lucas Mwashambwa na wenzake eti unawaambia wakafanye kazi ya umachinga! Unafikiri watakubali? Na wakati wameshazoea kuendesha maisha yao kwa kulamba watu miguu!!
 
Waziri wa mambo ya ndani ambapo uhamiaji ni kazi yao! Fanyeni operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu. Jeshi lipo tuuu kazi kushiriki mambo ya siasa badala ya kulinda mipaka ya nchi na wananchi wake.
Mkulu asiongee tu kwa sababu october ni jirani.
 
Hayo mbona kila siku anayasema na kuyarudia lkn hakuna kinachofanyika, wachina wapo hadi mtwara wamegeuka kangomba na wengine wanatembeza korosho kwenye mabasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…