Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tafuta kazi ya kufanya. Hii imekushinda, me nashauri wale wanaopigaga makelele na mayowe wakitafuta/kuwataka watu waandamane wawatafute majobless. Mapema tu kinaeleweka mbona, watu wamechoka mtaani hapakalikiRais Samia Suluhu Hassan ameendeleza juhudi zake za kuwawezesha vijana na kuboresha ufanisi wa kazi katika taasisi za serikali. Ndani ya miezi sita ya kwanza ya mwaka 2023,serikali imeajili vijana 18,449.
Idadi hiyo inajumuisha walimu wapatao 13,130 ambao wamepata nafasi za ajira katika sekta ya elimu. Aidha, kada ya Afya imepokea watumishi wapya 5,319, wanaosaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Licha ya mipango mbalimbali ya kuwawezesha vijana kujiajiri, Rais Samia ameendelea kutoa vibali vya ajira kwa taasisi za serikali zenye uhitaji. Hatua hii inalenga kutoa fursa kwa vijana wenye ujuzi na talanta, wakati huo huo kukuza ufanisi wa kazi katika taasisi hizo.
Rais Samia ameonyesha dhamira yake ya kusaidia vijana kujenga kazi na kuchangia katika maendeleo ya nchi. Utekelezaji wa sera hii ya ajira kwa vijana unaonyesha nia ya serikali ya kujenga taifa lenye nguvu kazi ya vijana wenye ujuzi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.
Mafanikio haya yanathibitisha jitihada za serikali katika kutoa fursa za ajira kwa vijana na kuboresha sekta muhimu kama elimu na afya. Wananchi wana matumaini kuwa hatua hii italeta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma na kukuza ustawi wa taifa.
TINDO umekuja kivingine.Basi ukute hapo wale wafuasi wa lile shetani wamefura mpk basi kwa sababu for 6yrs lile dubwana lilishindwa kabisa kuajiri.
Siyo kidogo, ni sana. Jiwe afe tena huko aliko.sasa angekuwa kma mama hivi miaka yake mitano bwam yule Vijaja wengi wengekuwa vizur msongamano ungepungua kuliko uliopo saivi, Jiwe alisababisha umasikini endelefu kidogo kwa vijana wa taifa hili,
Inashangaza we ulichoelewa umeandika pumbaTukusaidiaje au mfuate kaburini maana huelewi hata ulichoandika,kisome uone.
walio kula teuziKuna wapumbavu wanamsifu 😁😁
babaakomchawi