Pre GE2025 Rais Samia aamsha shangwe baada ya kuwalipia tiketi abiria wote waliosafiri kwa treni ya kisasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha Watanzania Daktari Samia Suluhu Hasssan ameibua shangwe na kuteka hisia za watanzania wengi sana, baada ya Rais wetu mpendwa kwa moyo wake wa upendo, huruma, ukarimu na unyenyekevu.

kuamua kwa dhati ya Moyo wake na kwa pesa zake binafsi zinazotokana na jasho lake. Kuamua kuwalipia tiketi abiria wote waliokuwa wamefanya safari kwa mara ya kwanza na treni ya kisasa kabisa kutoka Dar kwenda Morogoro na Morogoro kwenda Dar.

Rais wetu anafanya hivyo kuwapa hamasa Watanzania kutumia usafiri huo wa kisasa, mzuri,salama,nafuu,wa haraka na wenye utulivu wa hali ya juu sana .ambao watu watakaa vizuri pasipo kuchoka wala uchovu wala bughudha wala hofu huku wakifurahia mazingira mazurii ya njiani na hali ya hewa nzuri na safi sana kwa afya ya Mwanadamu..

Rais wetu Anaendelea kugusa na kuteka mioyo ya Watanzania ,kwa matendo yake ya huruma na upendo kwa watu wote . Niambie ni kiasi gani furaha waliyo nayo abiria hao ambao wamepewa ofa hiyo buree kabisa na mama yao mpendwa mwenye moyo wa huruma kwa watu wake. Wameokoa kiasi gani cha pesa ndugu zangu Watanzania?

Hii ndio raha ya kuongozwa na Mama, raha ya kuwa na kiongozi mwenye upendo na ukarimu kwa watu,raha ya kuwa na kiongozi anayewajali na kuwathamini watu wake. Najisikia fahari sana na mwenye bahati sana kuongozwa na Rais Samia .ni historia kwagu nitakayoisimulia miaka ya baadaye panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

Imefika wakati watanzania raha zimewazidi mpaka wakifika mahali na wakiona mabango ya Rais wetu njiani yenye picha yake ,wanasimama kwa bashasha na tabasamu na kujipiga picha mbele ya mabango hayo huku wakifurahia na kumuombea Maisha marefu yeye heri na baraka tele kwake..

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kulipia nauli raia ama kuwapa free entry Kuna impact gani kwa mtanzania anae ishi mwabagalu..
 
Katiba hii ibadilishwe.tumerithisha mtu ambaye maono yake ni cm1 badala ya kuwa km10000.kama anania ya kuwasaidia punguza gharama ili Kila mtanzania aweze kumudu huo usafiri.anawalipia Kwa pesa za umma anasema za kwake?Hii ni hongo ya uchaguzi 2025 na anatakiwa kufunguliwa mashaka ya rushwa.Au kama ameamua kuwalipia wtz awalipie Kila siku.huu uhuni haukubaliki
Upotevu wa fedha huo
 
Dawa za hospitalini zitanunulia kwa kodi zetu kama ambavyo zimeendelea kununuliwa wakati wote .hata hivyo Rais wetu kutumia pesa zake ambazo ana uhuru nazo na pia hazuiliwi kutoa na kusaidia watu.pia kuna watu hapo walikuwa wanakwenda hospitali na kupitia kulipiwa nauli maana yake wataweza kupata hela ya kununua dawa kwa pesa walioweza kuokoa
Kwann asiongezee bidii kwa kujitolea na hizo pesa za mfukoni kwake ili kuokoa maisha ya wananchi wake?? Kuliko kulipia nauli watu ambao wana uwezo wa kuandaa safari ili wakashangae treni
 
Niambie ni wapi ambako Rais Samia hajafikisha mkono wake na kugusa maisha ya watu, kwa kuyapatia matumaini na nuru.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha Watanzania Daktari Samia Suluhu Hasssan ameibua shangwe na kuteka hisia za watanzania wengi sana, baada ya Rais wetu mpendwa kwa moyo wake wa upendo, huruma, ukarimu na unyenyekevu.

kuamua kwa dhati ya Moyo wake na kwa pesa zake binafsi zinazotokana na jasho lake. Kuamua kuwalipia tiketi abiria wote waliokuwa wamefanya safari kwa mara ya kwanza na treni ya kisasa kabisa kutoka Dar kwenda Morogoro na Morogoro kwenda Dar.

Rais wetu anafanya hivyo kuwapa hamasa Watanzania kutumia usafiri huo wa kisasa, mzuri,salama,nafuu,wa haraka na wenye utulivu wa hali ya juu sana .ambao watu watakaa vizuri pasipo kuchoka wala uchovu wala bughudha wala hofu huku wakifurahia mazingira mazurii ya njiani na hali ya hewa nzuri na safi sana kwa afya ya Mwanadamu..

Rais wetu Anaendelea kugusa na kuteka mioyo ya Watanzania ,kwa matendo yake ya huruma na upendo kwa watu wote . Niambie ni kiasi gani furaha waliyo nayo abiria hao ambao wamepewa ofa hiyo buree kabisa na mama yao mpendwa mwenye moyo wa huruma kwa watu wake. Wameokoa kiasi gani cha pesa ndugu zangu Watanzania?

Hii ndio raha ya kuongozwa na Mama, raha ya kuwa na kiongozi mwenye upendo na ukarimu kwa watu,raha ya kuwa na kiongozi anayewajali na kuwathamini watu wake. Najisikia fahari sana na mwenye bahati sana kuongozwa na Rais Samia .ni historia kwagu nitakayoisimulia miaka ya baadaye panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

Imefika wakati watanzania raha zimewazidi mpaka wakifika mahali na wakiona mabango ya Rais wetu njiani yenye picha yake ,wanasimama kwa bashasha na tabasamu na kujipiga picha mbele ya mabango hayo huku wakifurahia na kumuombea Maisha marefu yeye heri na baraka tele kwake..

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Nimependa sana huo ukarimu wa mama.
Napenda kujua namna alivyowalipia.Jee walikuwa wameshakata tiketi wakarudishiwa pesa au lilitoka tangazo kabla ya kukata tiketi kuwa watalipiwa.
Nahofia lingetoka tangazo la kulipiwa mwanzo watu wengi wasio na jamaa huko waendako wangejaza treni nzima na wenye shida ya kusafiri wangeshindwa kwa kiminyano cha kupata viti.
 
Back
Top Bottom