Huyu mama hana upeo wa kuweza kuongoza nchi.
Hivi ili mtu aweze kuongoza nchi inabidi aweje??
Maana wengi wetu humu hata kuniongoza wenyewe hatuwezi, kuongoza mahusiano ya wawili tuu hatuwezi, kuongoza familia ni shida.
Kujikomboa kiuchumi kwaajili yetu wenyewe shidaa.
Kujiajiri tuu shida, kushirikiana na jamii katika masuala mbalimbali ngumu mno.
Tukikosolewa na mtu weee unaweza hata ukatamani umuue.. Na hatukubali hata kushauriwa.
Ila ndio sisi sisi tunaouchambua uchumi wa nchi, chambua viongozi sijui kashindwa au kafeli au hawezi kitu.
Wengine tunakosoa kwa lugha chafu zisizo na staha zenye kuudhi na kutia hasira..
Halafu tunataka tunaemkosea au kumkosoa ajibu Amina maana yeye ni Malaika ana moyo wa upepo.
Ila akithubutu kutujibu nongwa na matusi, kejeli, dharau na kusema hakutakiwa kusema hivi wala vile.
Tunamtaka Rais au kiongozi yeyote avumilie chochote anachoambiwa ila sisi humu humu kwenye jukwaa hatuvumiani.
Ole wako uwe na mtazamo au maoni tofauti au ushauri utakula matusi mpaka utamani kuua mtu...
Tunitathimini sana sana, tujikague sana mioyoni mwetu kama sisi ni wakamilifu kuliko hao tunao washambulia kila siku.
Mimi huwa napenda kukosoa kwenye mambo ambayo mimi nimefanikiwa vizuri..
Utasikia Serikali ibuni vyanzo vipya vya mapato wakati anayesema hivyo yeye mwenyewe hana hata chanzo chochote cha mapato, hajui hata abuni nini mamskini. Kachapwa na maisha na kachapika haswaa.
Huwa siwapendi kabisa watawala wetu lakini huwa nachukia zaidi kuwashambulia kwa kufuata mikumbo tuu na vishawishi vya kisiasa.
Nchi yetu hii ukiwatazama hata hao wakosoaji yaani hadi unacheka.
KUKOSOA NDIO KAZI RAHISI KULIKO ZOTE DUNIANI NDIO MAANA WAJINGA WOTE HUJAZANA KWENYE SEKTA HIYO.