Rais Samia achana na Mchengerwa kwenye baraza jipya, anakuharibia sana

Rais Samia achana na Mchengerwa kwenye baraza jipya, anakuharibia sana

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,875
Reaction score
29,427
Najuwa kuwa ni mkwe wako na una msifu kuwa ana kifua kikubwa lakini uwezo wake kiakili (IQ) ni mdogo.

Mwaka jana alitumia mbinu zile zile za Magufuli za mwaka 2019 kuharibu uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Na huo uchaguzi ndiyo uliozaa No Reforms No Elections. Kama CHADEMA wangetendewa haki basi hata 4R ingeendelea kuchakatwa, lakini ikaonekana haina maana kabisa kama bado matendo ya 2019/20 yanajirudia.

Kwa uzoefu wangu kama Mchengerwa asingeingilia uchaguzi huo Upinzani wangeweza kufika hadi 30-35% ya uongozi wa kata na vitongoji. Hivyo bado CCM ingeendelea kupeta.

NRNE ndiyo imeleta sintofahamu zote tulizonazo kwa sasa. Tunailaumu Mahakama na TANPOL lakini hawa wanafanya damage control tu.

soma pia uzi huu:-

 
Soma na uzi huu pia;-
 
Soma na hii hapa;-
 
Uwezo wa Hangaya kuchakata mambo mdogo sana. Hangaya kuwa hata VP lilikua tusi baya sana kwa watz matokeo yake ndo haya.
Umepimaje?..hasa ukizingatia ana post graduate ya credible university na masters ya out
 
Umeandika hoja yenye mashiko. Shida iliyoko kwa huyo mama yeni ni kuzungukwa na washauri vilaza na wasio na maono! Nakuhakikishia kama kiburi na dharau zitaendelea dhidi ya CHADEMA, wafuasi wake na viongozi wake! basi maafa siku zijazo yatakuwa ni makubwa zaidi.

Ni ujinga mkubwa sana mpaka leo kuna watu wanaamini kwamba ccm pekee ndiyo ina haki ya kuitawala hii nchi hata kama wananchi walio wengi wameichoka!

Haya maandamano na mauaji yaliyo tokea, yamesababishwa kwa asilimia kubwa na viongozi wa wa ccm!
Hoja zote walizotoa CHADEMA zina mashiko!
1. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi, ambayo wasimamizi wake wote wanateuliwa na mgombea wa ccm!

2. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi ambayo mara zote imekuwa ikiwaengua wagombea wa vyama vya upinzani tu kutokana na kasoro mbalimbali.

3. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi inayowazuia mawakala wa vyama kuwepo kwenye vituo vya kupigia kura.

4. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi ambayo inapiga marufuku wagombea na mawakala wao kukusanya takwimu za matokeo kutoka vituoni.

5. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi inayowategemea walimu na watumishi wengine wa serikali iliyoko madarakani kusimamia uchaguzi.

6. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi inayopika matokeo hadharani.

7. Hatuwezi kuwa na uchaguzi unaombeba mgombea mmoja tu wa chama tawala kupitia; vyombo vya habari, vitisho, rushwa za wazi, mahakama, msajili wa vyama vya siasa, nk.

All in all, mapungufu ni mengi. Na yasipofanyiwa kazi kwa haraka, basi mbele ya safari balaa litakuwa ni kubwa zaidi. Ombi langu kwa watawala ni kwamba; waache kuishi na pia kuiendesha nchi kwa mazoea. Dunia imebadilika! Na uelewa pia wa watu umeongezeka sana.
 
Umeandika hoja yenye mashiko. Shida iliyoko kwa huyo mama yeni ni kuzungukwa na washauri vilaza na wasio na maono! Nakuhakikishia kama kiburi na dharau zitaendelea dhidi ya CHADEMA, wafuasi wake na viongozi wake! basi maafa siku zijazo yatakuwa ni makubwa zaidi.

Ni ujinga mkubwa sana mpaka leo kuna watu wanaamini kwamba ccm pekee ndiyo ina haki ya kuitawala hii nchi hata kama wananchi walio wengi wameichoka!

Haya maandamano na mauaji yaliyo tokea, yamesababishwa kwa asilimia kubwa na viongozi wa wa ccm!
Hoja zote walizotoa CHADEMA zina mashiko!
1. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi, ambayo wasimamizi wake wote wanateuliwa na mgombea wa ccm!

2. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi ambayo mara zote imekuwa ikiwaengua wagombea wa vyama vya upinzani tu kutokana na kasoro mbalimbali.

3. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi inayowazuia mawakala wa vyama kuwepo kwenye vituo vya kupigia kura.

4. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi ambayo inapiga marufuku wagombea na mawakala wao kukusanya takwimu za matokeo kutoka vituoni.

5. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi inayowategemea walimu na watumishi wengine wa serikali iliyoko madarakani kusimamia uchaguzi.

6. Hatuwezi kuwa na tume huru ya uchaguzi inayopika matokeo hadharani.

7. Hatuwezi kuwa na uchaguzi unaombeba mgombea mmoja tu wa chama tawala kupitia vyombo vya habari, mahakama, msajili wa vyama vya siasa, nk.

All in all, mapungufu ni mengi. Na yasipofanyiwa kazi kwa haraka, basi mbele ya safari balaa itakuwa ni kubwa zaidi. Ombi langu kwa watawala ni kwamba; waache kuishi na pia kuiendesha nchi kwa mazoea. Dunia imebadilika! Na uelewa pia wa watu umeongezeka sana.
Unaharibu credibility yako,ulionekana critical huko nyuma
 
Nahisi hapo kwenye kutosikiliza watu ndio tatizo lake kubwa. Halafu anaona ni sifa nzuri kujiita chura kiziwi!
Alisikiliza vizuri,akawa mtu wa maridhiano,toa mbowe gerezani,ruhusu mikutano..ghafla mkapata kichaa
 
Back
Top Bottom