Rais Samia Adai Mahakama Ina Matatizo: Je Ni Nani wa Kuyatatua

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Jana akiapisha Majaji aliowateua kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema "Kuna Tatizo Mahakama"

Jaji Prof Ibrahim Juma, kiukweli kazi ya u-CJ ni kubwa kuliko uwezo wake. Haya yalikuwa ndiyo mauteuzi ya Magufuli.

Huyu CJ ukimfuatilia siku zote ni mtu wa kulalamika kama mtuhumiwa tu. Miaka yote 7 kwenye kiti hicho hajafanya REFORM yoyote ya Mahakama. Je nini kufanyike kupunguza matatizo ya Mahakama?
Screenshot_20230524_132921_WhatsApp.jpg
 
Jana akiapisha Majaji aliowateua kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema "Kuna Tatizo Mahakama"

Jaji Prof Ibrahim Juma, kiukweli kazi ya u-CJ ni kubwa kuliko uwezo wake. Haya yalikuwa ndiyo mauteuzi ya Magufuli.

Huyu CJ ukimfuatilia siku zote ni mtu wa kulalamika kama mtuhumiwa tu. Miaka yote 7 kwenye kiti hicho hajafanya REFORM yoyote ya Mahakama. Je nini kufanyike kupunguza matatizo ya Mahakama?View attachment 2633301
Mama ana maanisha kua, penye wazuri,wabaya pia wapo! Sasa wote kwa pamoja tushirikiane kuwachomoa wale wote wabaya kwenye Mahakama zetu za chini au za juu,ila hasahasa Mama alizilenga sana Mahakama za chini. Na ni kweli Mahakama za chini zina uchafu mwingwi, Watumishi wajanja wamezigeuza kua vituo vyao vya upigaji huku wakiminya haki za watu wasiokua na uwezo wa kununua huduma zao!!!
 
Kufuatia kauli ya Mhe. Rais nimejiuliza;

Hivi kweli inawezejana Jaji/Majaji wakala rushwa?!!! Maana tunavyo jua katika mahakama Majaji ndio wanao lipwa mishahara minono, wanapewa nyumba ya kuishi, wanapewa gari na pia Wana pewa Mlinzi n.k, sasa inawezekanaje Tena watu hao wakala rushwa?!!!

Kama wapo wanao pindisha haki kwasababu ya rushwa basi hao wanapaswa watolewe mara moja hawafai.
 
Sina uhakika sana kwa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Lakini huku kwa Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi hadi Mahakama za Mwanzo, RUSHWA ndiyo mhimili wa HAKI
 
Jana akiapisha Majaji aliowateua kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema "Kuna Tatizo Mahakama"

Jaji Prof Ibrahim Juma, kiukweli kazi ya u-CJ ni kubwa kuliko uwezo wake. Haya yalikuwa ndiyo mauteuzi ya Magufuli.

Huyu CJ ukimfuatilia siku zote ni mtu wa kulalamika kama mtuhumiwa tu. Miaka yote 7 kwenye kiti hicho hajafanya REFORM yoyote ya Mahakama. Je nini kufanyike kupunguza matatizo ya Mahakama?View attachment 2633301
POWER HIERACHY YA TANZANIA

1. CCM
2. EXECUTIVES
3. BUNGE
4. MAHAKAMA
5. CHAWA
6. WANANCHI
 
Kuna matatizo mahakamani kisa Musiba alishindwa kesi!😁😁😁
 
Siku chache baada ya kifo cha Membe, shutuma zimemuendee Jaji Mkuu kwamba yeye ndiye ametumika kuivunjia Yono leseni yake.

Siku si nyingi baada ya kifo cha Membe majaji wengine wakateuliwa, na sasa Jaji Mkuu ananangwa hadharani na Raisi.

Ni dhahiri kuna kitu nyuma ya pazia.
 
Mahakama chafu chafu, Kuna case hadi nimeamua kuitupa.. wamekula rushwa live live.. hovyo sana
 
Tanzania niwapi hakuna tatizo? Wapi hakuna mambo ya hovyo? Kuwa Serikalini na bungeni hakuna mambo ya ovyo?
 
Sina uhakika sana kwa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Lakini huku kwa Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi hadi Mahakama za Mwanzo, RUSHWA ndiyo mhimili wa HAKI
Kwani yule aliye pindisha kesi ya kule Lindi ni Jaji au Hakimu?
Maana Mhe. Rais alisema Jaji alienda kutizama na akaamua kuwa wafugaji hawana makosa wakati ukweli ni kwamba kulikuwa na makosa kwa mujibu wa maelezo ya RC

Kwa kauli ya Mhe. Rais inaonyesha wazi kuwa aliye pindisha haki alikuwa Jaji.

Ndio maana nimejiuliza, inakuwaje Jaji apindishe haki?!!!
 
Jana akiapisha Majaji aliowateua kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema "Kuna Tatizo Mahakama"

Jaji Prof Ibrahim Juma, kiukweli kazi ya u-CJ ni kubwa kuliko uwezo wake. Haya yalikuwa ndiyo mauteuzi ya Magufuli.

Huyu CJ ukimfuatilia siku zote ni mtu wa kulalamika kama mtuhumiwa tu. Miaka yote 7 kwenye kiti hicho hajafanya REFORM yoyote ya Mahakama. Je nini kufanyike kupunguza matatizo ya Mahakama?View attachment 2633301

Hakuna mahakama Tanzania.
 
POWER HIERACHY YA TANZANIA

1. CCM
2. EXECUTIVES
3. BUNGE
4. MAHAKAMA
5. CHAWA
6. WANANCHI
Kwa jinsi wananchi wenye hasira kali tunavyo kuwaga seriously na mambo yetu tukiwapa vibano waharifu naona mahakama ipo chini yetu haina hadhi ya kutuzidi sisi.
Halafu Samia amesahau kuwa yeye mwenyewe alidai kuwa wanao ushahidi kuwa Mbowe ni gaidi hewa wakati Mahakama haijamtia hatiani halafu Leo ndio anagundua tatizo aisee!!
Mahakama inapelekewa kesi ya ugaidi hewa na inakaa na kesi miezi nane hadi watunga kesi ya michongo wanaona hawana uwezo kuithibitishia dunia wanaiondoa kesi hiyo mahakama au utopolo.
Nafikiri huu ndio mgawanyo mpya wa Mihimili kwa sasa nchini.
1.CCM
2.EXECUTIVES
3.WANANCHI
4.CHAWA
5.MAHAKAMA
6.BUNGE
 
Kwani huyu Profesa Ibrahim Juma anastaafu lini? Pengine ni wakati wa kupata Jaji Mkuu mwingine atakayeleta mageuzi
Mtu mmoja hawezi kuleta mageuzi. Sana sana atajitengenezea maadui.
 
Jana akiapisha Majaji aliowateua kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Rais Samia alisema "Kuna Tatizo Mahakama"

Jaji Prof Ibrahim Juma, kiukweli kazi ya u-CJ ni kubwa kuliko uwezo wake. Haya yalikuwa ndiyo mauteuzi ya Magufuli.

Huyu CJ ukimfuatilia siku zote ni mtu wa kulalamika kama mtuhumiwa tu. Miaka yote 7 kwenye kiti hicho hajafanya REFORM yoyote ya Mahakama. Je nini kufanyike kupunguza matatizo ya Mahakama?View attachment 2633301
Kuyatatua ni katiba mpya ,ili mihimili kuwa huru basi na hakuna njia nyingine
 
Back
Top Bottom