Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa. Ally Hapi, Kigaigai, Kafulila na Eng. Robert Gabriel watemwa

Wengine wanatumia fursa ku set mambo yao kwa muda mfupi kwakuwa wanajua aina ya kazi ilivyo.
Ukipata ukuu wa Mkoa hata kwa miezi 6 tu fanya kitu.
Aina hizi za ajira ndio zinapelekea Hawa wakuu kuwa wadokozi wa pesa za Uma na kupiga madili.
 
Atakuwa alikwisha jiandaa kisaikolojia...
Its a game of thrones! Leo yuko huyu, kesho yuko yule...

Leo uko kwenye kiyoyozi, kesho uko kwenye mionzi, unapigwa na jua.
Leo unafunguliwa mlango wa V8, kesho unashika bomba kwenye DCM la Gongo la Mboto.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]pumbav
 
Hao Brigedia warudi jeshini. Ukuu wa mkoa wapewe makanali. Sio brigedia. Brigedia warudi jeshini, wapande vyeo kuwq Major, wapewe uongozi wa kamandi na Idara jeshini. Kuna vyuo vya kijeshi, kuna hospitali za jeshi, kuna balozi, kuna kamandi, kuna vitengo vya makao makuu.
Pengine CDF Mkunda ndio kawahitaji kwa ajili ya re-organisation yake jeshini.
Lakini pia majors wanastaafu. Wao waende kuziba mapengo.
 
Wale ambao hawakuwa na kazi kabla ya kupata ukuu wa mkoa, warudi kwanza home, watangiwa majukumu mengine.
 
1.Alli hapi
2.Kafulila
3.Eng Gabriel
Nk
Wameliwa kichwa

NB
Mtaka kutoka Dodoma hadi Njombe ni kama wamemla kichwa kistaarabu.
Ajirekebishe tabia yake ya u much know, kiburi na dharau.
Alisifiwa mwanzo naona sasa hivi anaharibu,sifa zinamlevya wahenga walipata kusema"...... Mgema akisifiwa tembo hulitia maji."
 
Kazi za kipumbavu sana unakua at President's disposal all the time. Mara uhamishwe, mara ufutwe as though maisha yako hayana dira. Huwa sielewi kwanini wanazikubali.
Hizi kazi zipo kwa ajili ya kila mtanzania mwenye sifa zinazoendana nazo; possibly wewe ukiwa ni mmoja wao. Unakuwa mpumbavu wewe kwa kuziita kuwa ni za kipumbavu kwa sababu in essence, wewe pia ni mmojawapo wa watu wanaowajibika kufanya kazi hizi, na pasipo hiari yako. Ni kwa sababu tu tuna tatizo la ajira, ndiyo maana inaonekana kama kazi hizi ni ulaji na za hiari wakati siyo. Mamlaka za uteuzi zikishaamua kuwa wewe ufanye kazi hizo, inakuwa siyo hiari. Sema tu kwa sababu tunaozihitaji tupo wengi, ikitokea ukaamua kuomba uachwe apewe mtu mwingine, mamlaka za uteuzi huwa hazioni sababu yoyote ya kuendelea kumng'ang'ania mtu mmoja wakati walio na sifa bado wapo wengi tu mtaani. Tuseme kwa mfano, wewe ndiyo mtu pekee mwenye sifa ya kufanya kazi ambayo mamlaka ya uteuzi imeamua kukuteua, katika mazingira hayo unakuwa huna hiari ya kutokufanya kazi hiyo; whether unapenda au hupendi, kazi hiyo lazima utaifanya; iwe ni ukuu wa Mkoa au uwaziri, ni lazima utafanya bila kujali unapenda au hupendi
 
Raisi amefanya teuzi, mikoa yote ya Tanzania Bara ipo kwenye mkeka, kasoro Mkoa wa Simiyu tu.

Tayari watu wana assume Kafulila kaliwa kichwa, pamoja na Mkoa wake kitoonekana kwenye huo mkeka.

Zuhura Yunus weka sawa mambo yako, makosa madogo madogo yanajirudia sana, kila siku na jambo jipya.
Kwamba hujaona Nawanda anakwenda Simiyu? Kafulila Bwana!! Wewe fungasha tu, kwenye barua ya Yunus hakuna kipengele cha waliotumbuliwa.
 
Atakuwa amehamishiwa uraiani kujiunga na wana nzengo , aangalie vizuri jina lake huko uaiani
 
Back
Top Bottom