Hizi kazi zipo kwa ajili ya kila mtanzania mwenye sifa zinazoendana nazo; possibly wewe ukiwa ni mmoja wao. Unakuwa mpumbavu wewe kwa kuziita kuwa ni za kipumbavu kwa sababu in essence, wewe pia ni mmojawapo wa watu wanaowajibika kufanya kazi hizi, na pasipo hiari yako. Ni kwa sababu tu tuna tatizo la ajira, ndiyo maana inaonekana kama kazi hizi ni ulaji na za hiari wakati siyo. Mamlaka za uteuzi zikishaamua kuwa wewe ufanye kazi hizo, inakuwa siyo hiari. Sema tu kwa sababu tunaozihitaji tupo wengi, ikitokea ukaamua kuomba uachwe apewe mtu mwingine, mamlaka za uteuzi huwa hazioni sababu yoyote ya kuendelea kumng'ang'ania mtu mmoja wakati walio na sifa bado wapo wengi tu mtaani. Tuseme kwa mfano, wewe ndiyo mtu pekee mwenye sifa ya kufanya kazi ambayo mamlaka ya uteuzi imeamua kukuteua, katika mazingira hayo unakuwa huna hiari ya kutokufanya kazi hiyo; whether unapenda au hupendi, kazi hiyo lazima utaifanya; iwe ni ukuu wa Mkoa au uwaziri, ni lazima utafanya bila kujali unapenda au hupendi