Rais Samia afuta sherehe za Uhuru, aagiza fedha zitumike kusaidia huduma za kijamii

..Ni taifa la ajabu lisiloenzi uhuru wake.
Siku za uhuru kuna marudio ya matukio yale yale ya kila mwaka, wanapoamua kuahirisha wanakuwa wameshapima hasara zozote (kama zipo) zinazoweza kutokea baada ya kufanya hayo maamuzi.

Ni masuala yale yale ya makomandoo kuvunja mawe vifuani mwao na zile show za kutua na kamba kutoka kwenye helikopta.

Wajanja wanapiga pesa kupitia bajeti zinazotengwa kwa ajili ya shughuli zote za halaiki za siku ya uhuru.

Najua umeamua kupinga kwa sababu ni maamuzi ya Rais Samia ambaye upo uwezekano haumpendi, kwa hiyo unapinga sio kwa sababu unaipenda sana siku ya uhuru bali ni siasa tu za chuki.
 

..i'm on the record kupinga maonyesho ya vijana wetu kupasua matofali vichwani au miilini mwao.
 
kwanini haka kabiinti kanataka kufuta historia ya Tanganyika huku kanatapanya Mali za Tanganyika kama kamelewa mnazi?
 
Akili zetu wadanganyika tuta mshukuru. Kwasababu kadanganya eti pesa za sherehe zipelekwe wapi sijui.

Hizo pesa zimetoka wapi?
 
Sherehe za uhuru wa Tanganyika zinaamuliwa vipi jinsi ya kufanyika na mtu asiye Mtanganyika?
Just asking🤔🤔
 
Inatia hasira kwa kweli sijui kizazi kijacho kitajifunza nn
 
At least yule dikteta alikuwa chembechembe za Utanganyika wa kuchovya.
Samia anafanya mengi sana huku Tanganyika kuliko huko kwao Zanzibar, cha muhimu kwako ni kutafuta habari zake nyingi ambazo nina uhakika huzifahamu ndio maana unakimbilia kwenye hoja ya kibaguzi ya utanganyika na uzanzibari.
 
Samia anafanya mengi sana huku Tanganyika kuliko huko kwao Zanzibar, cha muhimu kwako ni kutafuta habari zake nyingi ambazo nina uhakika huzifahamu ndio maana unakimbilia kwenye hoja ya kibaguzi ya utanganyika na uzanzibari.
Waulize tu Tan road madaraja sasa hivi mvua zinanyesha yanavunjika, kama wana hata senti kuyajengea. Pili tunaposema anafanya makubwa Tanganyika, je mkusanyaji mapato mkubwa ni nani kati ya Tanganyika na Zanzibar ? Kwa hiyo ulitaka Tanganyika azalishe na pesa yake atumie mwingine, japo hata hivyo ndivyo inafavyofanyika sasa. Tatu, pesa hata sh 1 ya Zanzibar wanazokusanya inavuka kuja Tanganyika kufanya chochote au ni kinyume chake ?
 
Wakati Rais wa Kenya aliposema majuzi kwamba Tanzania kwa sasa inaizidi Kenya katika mchango wake kiuchumi alikuwa anaongelea Tanzania Bara au Visiwani?.

Samia anaiboresha hiyo TRA ili iweze kukusanya zaidi ya sasa, Samia kapigana mpaka wakulima wa korosho wamepata bei kubwa kuliko waliyowahi kuipata tangu uhuru wa nchi.

Samia anaimalizia reli ya SGR ili iwe na uwezo sawa na ile ya Lobito kule Angola, anafanya mengi sana na hii hulka ya kuuongelea uzanzibari na utanganyika ni ujinga wetu tu humu jukwaani.

Ni mbinu ya kijinga ya kuja na malalamiko mengine baada ya kushindwa kuyathamini mema anayoyapigania kwa faida ya Tanzania nzima.
 
Aliyetaja Zanzibar ni wewe mkuu. Nimejibu kukuonyesha nani anamnufaisha nani. Usingetaja hiyo Zanzibar au Tanganyika Wala nisingejibu kuvihusu. Yako mengi sana tunyamaze tu ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…