Rais Samia ahutubia taifa leo Agosti 22, 2022. Ametoa wito na kuwasihi Watanzania wote kujitokeza kuhesabiwa

Huyu mama ni mkatili sana,Itakuwa anmsokiliza yule makamu wake anayeongea Kama ameweka mkaa wa moto mdomoni.
Mama yetu mh Rais Ni kiongozi mwenye huruma na upendo mkubwa Sana kwetu watanzania, ndio maana unaona akihangaika huku na kule kutatua kero za wananchi, ndio maana unaona akifanya juhudi za kusogezwa huduma muhimu karibu na wananchi, ndio maana unaona akifikia hatua ya kutoa Ruzuku ili kumsaidia mwananchi asielemewe na mzigo kichwani

Ndio maana kila sent inayopatikana anaipeleka kupunguza au kumaliza kero kwa wananchi, ndio maana unaona akifuta ada na kuweka Elimu bure Hadi kidato Cha sita ili hata watoto wa wananchi wanyonge wapate Elimu sawa na wale watokao katika familia zenye kipato kikubwa

Ndio maana unaona akiendelea kuboresha huduma mbalimbali zinazogusa maisha ya mwananchi, ndio maana unaona akiwasihi wasaidizi wake kuwa wanyenyekevu na wenye upendo kwa wananchi hasa wanyonge

Ndio maana unaona Hataki mtu yoyote Yule aonewe au kudhulumiwa haki yake, ndio maana unaona akifuta kesi za kisiasa ili watu walejee kwenye familia zao Hataki kuongoza nchi ambayo Kuna familia zinakesha usiku kucha zikilia machozi kwa kuwa Kuna mpendwa wao kafungwa kwa kuonewa
 
Hakuna sheria inayomlinda huyo raia ,yaani hakuna privacy kama kuna mtu anayo naomba aweke hapa
 
We dogo acha ujinga. Usidhani humu kila mtu mtoto mwenzako.

Mode fungieni hawa watoto. Huyu tangu asubuhi anatuma vitu vya ajabu tu
Wote ni Maboya kasoro wasio na vyama. Kwani CCM wamefanya nini? Wapinzani wamefanya nini?
 
Rais Samia wa JMT atalihutubia Taifa saa 3 00 usiku huu

Usikose

Chanzo: ITV

Updates;

Rais Samia amewaomba watanzania wote watoe ushirikiano kwa makarani wa Sensa katika zoezi litakaloanza das 6:00 usiku huu
Hiyo sio hotuba ni tangazo tu.

Hatuna rais wa kuhutubia taifa ilikuwaga Mkapa tu
 
Nani amekwambia Watanzania tunataka huruma?

Tunataka rais wa kutimiza majukumu yake kama mkuu wa nchi.

Atuhurumie kwasababu gani?

Tunalipa kodi tunataka return basi.
 
Aliyesikiliza atupe mrejesho
 
Hili la sensa mkawape ushirikiano kina ngoswe wote ~ alisikika malkia wa nyuki mmiliki wa asali
 
Nani amekwambia Watanzania tunataka huruma?

Tunataka rais wa kutimiza majukumu yake kama mkuu wa nchi.

Atuhurumie kwasababu gani?

Tunalipa kodi tunataka return basi.
Ndio hayo majukumu mh Rais wetu Anaya tekeleza kwa weledi mkubwa Sanaa, mh Rais wetu anatanguliza mbele maslahi ya Taifa, ndio maana unaona namna anavyokubalika na kuungwa mkono na watanzania wengi
 
Asante kwa taarifa, tunamfuatilia
P
 
Akimaliza muda wake 2030, watanzania tutamtaka atusubiri Tuamue juu ya katiba yetu kuhusu ukomo, maana tunampenda Sana Rais wetu na tunamhitaji ili aendelee kututumikia watanzania, tumeridhishwa na kulizika na utendaji kazi wake mh Rais wetu
Hahaha watu washachoka dadadeki, huyu raisi siku anamaliza muda wake nadhani watu watacheza barabarani kwa maana duh!
 
Hiyo sio hotuba ni tangazo tu.

Hatuna rais wa kuhutubia taifa ilikuwaga Mkapa tu
Kwako ndio labda Tangazo lakini mh Rais wetu ukisikika tu atazungumza au kuhutubia muda fulani au kuwa mahali fulani unakuta hata kazi zinasimama ili kuweza kupata na kutoa muda wa kumsikiliza mh Rais wetu, anakubalika Sana Rais wetu na anapendwaa Sana mh Rais, hii yote inatokana na namna anavyofanya kazi kwa juhudi na maarifa katik kuwatumikia watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…