Rais Samia aingilie kati tatizo la wazee kuwaoa mabinti wadogo; aagize sheria ya ndoa kurekebishwa

Rais Samia aingilie kati tatizo la wazee kuwaoa mabinti wadogo; aagize sheria ya ndoa kurekebishwa

Jambo wakuu!

Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au​
Mtu akishafikisha miaka 18 anahesabiwa mtu mwenye haki ya kufanya maamuzi yake mwenyewe, ikiwamo kuoa na kuolewa.

Hilo liko kisheria.

Sasa hao wanaoolewa wanalazimishwa?

Au wako chini ya miaka 18?
 
Jambo wakuu!

Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa. Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa walipaswa kuonyesha mfano bora kwa watanzania, badala yake wamegeuka kuwa kero kwa kugeuza uharibifu wa mabinti kuwa jambo la umaarufu. Halafu wamekuwa siku zote wakitamba kabla na baada ya kufanya vitendo hivyo wakidhani kuwa wanafanya jambo zuri. Inasikitisha sana.

Baadhi ya viongozi wakubwa wa kitaifa ambao wamejitumbukiza kwenye mchezo huu mchafu wa kuwaoa mabinti wadogo ni Profesa Kapuya, Pius Ngwandu, Abrahamu Mengi na sasa mzee Augustine Lyatonga Mrema ametangaza kufunga ndoa hivi karibuni na binti mbichi kabisa anayelingana na wajukuu zake. Namuomba Mh mama Samia uingilie kati jambo hili kwa kuagiza Wizara ya Sheria kuifanyia mabadiliko sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuwasnusuru mabinti wasiolewe na wazee vikongwe. Sheria iweke tofauti ya umri wa watu wanaofaa kuoana; ikiwa tofauti ya umri itakuwa kubwa (kwa mfano miaka kuanzia 20 na kuandelea) basi ndoa hiyo ichukuliwe kuwa ni batili na mhusika (mume) atakayekuwa ametenda kosa hilo achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Watanzania wanapaswa kuiga mfano bora wa Pius Msekwa na John Malecela waliowaoa watu wazima wanaolingana nao kiumri.

Mama Samia umefanya jambo jema kuwaruhusu mabinti waliozaa kurejea shule kutimiza ndoto zao za kielimu. Hapa umeupiga mwingi mama yangu mpendwa. Adhma yako ya kutoa elimu kwa mabinti haiwezi kutimia ikiwa mabinti hao unaowapigania kurudi shule kupata elimu watakwapuliwa na wazee wenye uchu wa ngono. Nakuomba pia ushughulikie tatizo hili la mabinti wadogo kuolewa na baba au babu zao ili kuwakoa mabinti wanaoingia kwenye mtego huu wa fisi wapenda ngono.

Watu wanaweza kuchukulia jambo hili kuwa dogo lakini ukiliangalia kwa jicho la latu, hili ni tatizo kubwa sana linaweza kuathiri maadili ya kitaifa na ukosefu wa uzalendo na utii wa sheria. Ikiwa wazee wataendelea na tabia yao hii ya kuwaoa mabinti wadogo kuna uwezekano vijana wadogo wakiume nao wakaanza kuwaoa wanawake watu wazima ili kulipiza kisasi. Ndio. Ipo siku vijana watakosa mabinti wa kuwaoa na kuwageukia vikongwe. Endapo nchi itafikia hatua hii, maadili ya kitaifa yatamomonyoka kwa kiasi kikubwa. Kuliko kusubiri ukuta uanguke tujenge mpya, nakuomba mama Samia uingilie kati suala hili kabla hali haijwa mbaya sana.

Nawasilisha.​
Mzee wa msoga naye ninasikia fununu anataka kuvuta kibebi kidogo
 
Yan unashindwa kumshauri afocus kwenye mambo ya mhimu unamwambia anze kudeal na hisia za watu
Suala ndoa ni kisheria sio hisia za watu mkuu.

Ndio maana sheria inakataza watu ambao ni ndugu kuoana hata kama hisia zao zinawabana kuoana.

umenipata eeh?
 
Mtu akishafikisha miaka 18 anahesabiwa mtu mwenye haki ya kufanya maamuzi yake mwenyewe, ikiwamo kuoa na kuolewa.

Hilo liko kisheria.

Sasa hao wanaoolewa wanalazimishwa? Au wako chini ya miaka 18?
Baadhi yao ni under 18 na wengine wanarubuniwa kwa kuwa wanatoka kwenye familia fukara
 
Unamuonea wivu Augustino Lyatonga Mrema. Jamaa keshaopoa kabinti kadogo keupe, hata usemeje haitasaidia wala kubadilisha kitu.
 
Sasa mambo ya familia za watu wewe yanakuhusu nini?
Sio suala la familia hili bali ni suala la uvunjivu wa sheria.

Ndio maana wazazi wakiwazuia watoto kwenda shule huchukuliwa hatiua za kisheria.

Hawaachiwi kwa sababu eti hilo ni jambo la familia.

Umenipata?
 
Sio suala la familia hili bali ni suala la uvunjivu wa sheria. Ndio maana wazazi wakiwazuia watoto kwenda shule huchukuliwa hatiua za kisheria. Hawaachiwi kwa sababu eti hilo ni jambo la familia. Umenipata?
Kwa walio chini ya miaka 18 nimekwambia kafungue kesi polisi.

Hao wengine walio zaidi ya miaka 18 ni suala la familia.

Mpaka sasa ushafungua kesi ngapi?
 
Kwa walio chini ya miaka 18 nimekwambia kafungue kesi polisi.

Hao wengine walio zaidi ya miaka 18 ni suala la familia.

Mpaka sasa ushafungua kesi ngapi?
Mkuu mimi nimetuma maombi kwa mama Samia aingilie kati, kwa mtu kama wewe usiyejuasheria hata nikuelimisheje huwezi kunielewa mkuu.
 
Mkuu mimi nimetuma maombi kwa mama Samia aingilie kati, kwa mtu kama wewe usiyejuasheria hata nikuelimisheje huwezi kunielewa mkuu.
Kwa nini unamtumia mashtaka Rais Samia wakati kuna mfumo wa sheria unaoanzia polisi?

Sheria gani hiyo inayosema mashtaka ya jinai yaanze kwa rais?
 
Back
Top Bottom