Rais Samia aingilie kati tatizo la wazee kuwaoa mabinti wadogo; aagize sheria ya ndoa kurekebishwa

Rais Samia aingilie kati tatizo la wazee kuwaoa mabinti wadogo; aagize sheria ya ndoa kurekebishwa

Huyu Agostino Mrema kilichomtokea Pius Ng'wandu kinamnyemelea very soon. Mzigo wote ule atauweza kweli yule mzee aliyechoka kama ng'onda?
Kwanza kabisa hiyo habari nzima ya Mrema kuoa ni fake news.

Mpaka hapo ushaingia cha kike.
 
Kwanza kabisa hiyo habari nzima ya Mrema kuoa ni fake news.

Mpaka hapo ushaingia cha kike.
Kwa hiyo yule aliyemuoa leo ni jini sio binadamu? 😳 😳 😳
 
Na mabinti mnaowapa mimba na kuaacha then baadae mnakuja jinadi hamuoi single mother mnalichukuliaje
Wanawake wanajiachisha wenyewe, hakuna mwanaume anayemuacha mwanamke mkuu.
 
Jambo wakuu!

Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa.

Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa walipaswa kuonyesha mfano bora kwa watanzania, badala yake wamegeuka kuwa kero kwa kugeuza uharibifu wa mabinti kuwa jambo la umaarufu. Halafu wamekuwa siku zote wakitamba kabla na baada ya kufanya vitendo hivyo wakidhani kuwa wanafanya jambo zuri. Inasikitisha sana.

Baadhi ya viongozi wakubwa wa kitaifa ambao wamejitumbukiza kwenye mchezo huu mchafu wa kuwaoa mabinti wadogo ni Profesa Kapuya, Pius Ngwandu, Abrahamu Mengi na kesho tarehe 24/03/2022 mzee Augustine Lyatonga Mrema ametangaza kufunga ndoa na binti mbichi kabisa anayelingana na wajukuu zake. Namuomba Mh mama Samia uingilie kati jambo hili kwa kuagiza Wizara ya Sheria kuifanyia mabadiliko sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuwasnusuru mabinti wasiolewe na wazee vikongwe.

Sheria iweke tofauti ya umri wa watu wanaofaa kuoana; ikiwa tofauti ya umri itakuwa kubwa (kwa mfano miaka kuanzia 20 na kuandelea) basi ndoa hiyo ichukuliwe kuwa ni batili na mhusika (mume) atakayekuwa ametenda kosa hilo achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Watanzania wanapaswa kuiga mfano bora wa Pius Msekwa na John Malecela waliowaoa watu wazima wanaolingana nao kiumri.

Mama Samia umefanya jambo jema kuwaruhusu mabinti waliozaa kurejea shule kutimiza ndoto zao za kielimu. Hapa umeupiga mwingi mama yangu mpendwa. Adhma yako ya kutoa elimu kwa mabinti haiwezi kutimia ikiwa mabinti hao unaowapigania kurudi shule kupata elimu watakwapuliwa na wazee wenye uchu wa ngono.

Nakuomba pia ushughulikie tatizo hili la mabinti wadogo kuolewa na baba au babu zao ili kuwakoa mabinti wanaoingia kwenye mtego huu wa fisi wapenda ngono.

Watu wanaweza kuchukulia jambo hili kuwa dogo lakini ukiliangalia kwa jicho la latu, hili ni tatizo kubwa sana linaweza kuathiri maadili ya kitaifa na ukosefu wa uzalendo na utii wa sheria. Ikiwa wazee wataendelea na tabia yao hii ya kuwaoa mabinti wadogo kuna uwezekano vijana wadogo wakiume nao wakaanza kuwaoa wanawake watu wazima ili kulipiza kisasi. Ndio.

Ipo siku vijana watakosa mabinti wa kuwaoa na kuwageukia vikongwe. Endapo nchi itafikia hatua hii, maadili ya kitaifa yatamomonyoka kwa kiasi kikubwa. Kuliko kusubiri ukuta uanguke tujenge mpya, nakuomba mama Samia uingilie kati suala hili kabla hali haijwa mbaya sana.

Nawasilisha.​

Tuanze na wewe umeoa???
Maana mada za ndoa zinapendeza wakizidiskas wanandoa
 
Kwa hiyo yule aliyemuoa leo ni jini sio binadamu? 😳 😳 😳
Aah, my bad. Kuna binti alikanusha. Nafikiri watu wa mitandao walitumia picha yake kwa uongo.

Mrema anasema ana haki ya kuoa, mke wake alifariki, na huyu anayemuoa kafuata taratibu zote za kanisa na wazazi wa mke wameridhika.

Wewe tatizo lako nini?

Ulitaka wewe uolewe na Mrema?

 
Kama kafika miaka 18 mambo yao waachieni wenyewe...

Hata hivyo binti kakanusha...
 
Naunga mkono Ili kuepuka ya mengi na jack, na kuleta migogoro kwenye familia. Mabinti wanafata mirathi. Huwezi sema binti wa miaka ishirini kuolewa na mzee wa miaka 70.
 
Umri wa miaka 70 ni umri wa kujitengeneza na Mola wako ujiandae mwisho mwema, ashiki ni mind inatawalika.
 
Watu mnachekesha sana .. [emoji1][emoji1]
 
Wamechukua demu wako? Hakuna kitabu cha dini kimeweka vigezo vya tofauti ya umri kwa wanaotaka kuoana. Acha waoane.
 
Wazee hawana utelezi
Mpaka utafute artificial
Ivo vibint ni kushika tu skioo unapata utelezi
 
Mleta Mada yupo sahihi kabisa, hizi kesi za Mirathi mtaani zimekuwa nyingi sana hasa kwa mabinti wadogo waliofiwa na waume zao ambao ni wazee
 
Back
Top Bottom