Rais Samia aipa Zambia ardhi hekari 20 katika bandari kavu Kwala mkoa wa Pwani

Naona kama watu wameelewa tofauti na maana iliyokusudiwa au pengine mimi ndio nimeachwa solemba na hii habari...

Ukisoma kichwa cha habari, ni rahisi kuelewa ya kwamba ndani ya ardhi ya Tanzania kumemegwa hekari 20 na kukabidhiwa nchi ya Zambia kuendesha shughuli za bandari kavu...

Lakini ukiisoma habari zaidi, binafsi nimeelewa ya kwamba ndani ya bandari kavu ya Kwala kutatengwa zone maalumu ambayo itashughulikia forodha ya mizigo ya Zambia peke yake na hii ni kutokana na sababu ya wingi wa mizigo iendayo Zambia na ile ijayo toka Zambia, pia mchango mkubwa wa kibiashara...
 
Bahati mbaya baadhi yenu hamjui hali au changamoto za biashara duniani. Kwani hizo hekta zilizotolewa kwa Zambia si ni kwa manufaa ya Tanzania pia ? Tafakari.
Changamoto za biashara duniani zinahusu kugawa maeneo ya nchi yako kwa wengine?
Hakuna njia nyingine za kukabiriana na changamoto hizo?
 
Mikanganyiko ni mingi: Sehemu moja inasema "HEKA 20", na kwingine inasema "HEKTA 20"; vipimo ambavyo ni tofauti kabisa.

Kwa vile habari inasema Zambia wamepewa "ZAWADI", ni rahisi kuelewa kuwa eneo hili ni tofauti na lile iliyopo bandari kavu. Hili litakuwa eneo wanalolimiriki Zambia wenyewe.

Mambo ya namna hili kayafanya Uhuru Kenyatta pale Naivasha, alipowagawia Uganda, Rwanda, Sudan Kusini maeneo ili waendeshee shughuli zao za mizigo toka Mombasa.

Hii ilikuwa mbinu ya kuwavuta watumie bandari ya Mombasa.
 
Bahati mbaya baadhi yenu hamjui hali au changamoto za biashara duniani. Kwani hizo hekta zilizotolewa kwa Zambia si ni kwa manufaa ya Tanzania pia ? Tafakari.
Sisi tumepewa ardhi kwenye nchi gani ili tupime hiyo biashahara ya Dunia? Au wengine hawataki hiyo faida?
 
Kiufupi tu ni kuwa mleta mada ana mawazo hasi yake kichwani dhidi ya mama na serikali yake. Katika kufikiria atoke vipi katika kusambaza chuki zake hizo, akili zake zikamtuma atumie hako kampenyo asiko na uelewa nacho ili aendeleze upotoshaji wake akifikiri watu wote humu ni wajinga au wamejaa michuki tu isiyo na sababu kama hao wajinga wengine wachache waliokuja kichwakichwa kuungana nae. Hiyo kuchanganya ni mbinu yake ya kuwafumba wajinga. Umewaumbua sana ulipowatoa gizani kwa kuwaambia kuwa hata Kenya limefanywa sana tu kama mbinu ya kibiashara, ya kukamatia fursa sawa na harakati za kipindi hiki tulichonacho cha dunia.
 
Wenye akili janja wanamuelewa mama kuwa anaipigania Tanzania kimataifa.
Wenye akili dororo wao kila kitu ni hasi tu
Kazi iendelee
Wajinga kweli yaani.
Basi wana kiswali chao wenyewe, 'sisi tanzania tumewahi kupewa wapi'?🤣🤣🤣
 

Ni kweli mkuu lakini tujue Zambia wameanza kufikiria kutumia Bandari ya Angola, huu ni mkakati maalumu wa kuwashawishi kubaki nasi!
 
Sijui ametumia akilii gani. Atagawaje ardhi yetu kwa nchi yenye ardhi utadhani mali yake binafsi. Rais hana ardhi bali ni msimamizi tu. Kumbe ndiyo maana anagawa bandari zetu! Kama Zambia wanafanya biashara walipaswa kununua siyo kuzawadiwa. Inakuwaje wageni wamilki ardhi wakati wana diaspora hawaruhusiwi?
 
Taarifa ziko mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa rais Samia Suluhu Hassan ameipa Zambia ardhi eneo la Kwala kujenga bandari kavu. Ajabu, wakati sheria ya Tanzania iko wazi kuwa asiye mtanzania haruhusiwi kumilki ardhi, rais anagawa ardhi kwa wageni. Je huku si kuvunja sheria?

Je huu si ubaguzi tukizingatia kuwa watanzania wazaliwa wenye uraia wa nchi nyingine hawaruhusiwi kumilki ardhi nchini mwao? Naomba ushauri na michango yenu wanangu.
 
HURUMA mbaya sana, hata Bible yasema tuwe na kiasi!
 

Mbona eka 20 ni kidogo sana hizo kwa mizigo ya Zambia?

Mimi naona wangepewa hekta 20 kwa uchahe. Mzigo wa Zambia ni biashara kubwa sana.
 
Saa100 hajui hesabu .
Amegawa acres 49.4 za ardhi ila hajui hesabu.
1 hactre = 2.47 acre
That means 20* 2.47 = 49.4
Huyu mama anakoelekea ni kugawa kila kilichoko mbele yake sisi tunapiga makofi kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…