Rais Samia aipa Zambia ardhi hekari 20 katika bandari kavu Kwala mkoa wa Pwani

Rais Samia aipa Zambia ardhi hekari 20 katika bandari kavu Kwala mkoa wa Pwani

Bahati mbaya baadhi yenu hamjui hali au changamoto za biashara duniani. Kwani hizo hekta zilizotolewa kwa Zambia si ni kwa manufaa ya Tanzania pia ? Tafakari.
Shida sio hekari. Shida ni kitu kingine hujakijua.
Zambia akipewa eneo kwanza itachagiza biashara sababu zambia anatumia 34% kama tulivvoelezwa. Hivi mdau mkubwa kama huyu hekta 20 awe anahifdhia mizogo yake nayo ni shida? Subir uwe laisi wewe bas uje utengue.
 
Ujinga sana kujadili ardhi ya ekari 20 Kwala ambayo thamani yake hata milioni mia haifiki Kwa biashara inayoingiza mabilioni ya shilingi na ajira Kwa Watanzania. Kumbuka Msumbiji na AFRIKA kusini nao wanahitaji Hilo soko .Tena mjadala unaingiza Uzanzibar
 
Simuelewi huyu rais. Nani kampa kibao cha kugawa ardhi ya watanzania kwa Zambia?
Halafu watu wengi hawajui, wale wazambia ni waarabu kwa asili, watakuja kutuletea al-shababu hapa!
 
Halafu watu wengi hawajui, wale wazambia ni waarabu kwa asili, watakuja kutuletea al-shababu hapa!
Shida niliyosema ndio hii. Imedhiirika kweupe. Nilisema shida sio hekar. Shida ni kitu kingine. Sasa kimewekwa
 
Ujinga sana kujadili ardhi ya ekari 20 Kwala ambayo thamani yake hata milioni mia haifiki Kwa biashara inayoingiza mabilioni ya shilingi na ajira Kwa Watanzania. Kumbuka Msumbiji na AFRIKA kusini nao wanahitaji Hilo soko .Tena mjadala unaingiza Uzanzibar
Tatizo lako wewe hujasoma seminari, ndio maana huelewi!
 
Mkuu wengi wanatazama mambo kihisia hasa Uzi kama huu,comment ya kwanza huwa INA athari sana kwenye mtiririko mzima wa mjadala. Watanzania tunapenda lawama sana.
"Mteja Zambia hapa amekamatwa mazima hawezi geuka"
That's the means of lobbying!
-force iwekwe jinsi ya kulobby DRC ili naye asiwe kigeugeu maana anakatabia ka kugeuka geuka!
 
Mwambukusi na chadema hawajaliona hili ?

Ila nauliza raia wa TZ anaweza kuomba ekari 20 akapewa bila ya masharti ya kukatiza tamaa ?
 
Ni sehemu ya lengo la kujenga bandari kavu ya Kwala.

Kule bandarini hakuna ardhi ya kutosha kuwapa watumiaji bandari wakubwa mfano walivyopewa akina Malawi Cargo.

Ni kuifanya bandari ya Dar iwe efficient zaidi ili watumiaji wakubwa kama Zambia tuendelee kubaki nao.
 
Mwambieni mama hata mimi nina uhitaji wa kipande cha ardhi kwaajili ya uwekezaji. Nahitaji hekari 10 pekee, mimi kama mzawa wa nchi hii.
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imetenga eneo la hekari 20 za ardhi katika Bandari kavu eneo la Kwala Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhudumia mizigo kutoka Zambia ambapo amesema hiyo ndio zawadi ya Tanzania kwa Zambia katika wakati huu wa sherehe za Uhuru wa Zambia.

Rais Samia amesema hayo kwenye hotuba yake akiwa ni Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia iliyofanyika Ikulu ya Lusaka, Zambia.

“Kwa nia ya kuwaweka Watu wa Zambia kama kipaumbele katika mipango yetu na kutokana na azma yetu ya kurahisisha biashara kati ya Nchi hizi mbili, Serikali yangu imefanya maamuzi ya kutenga eneo la hekta 20 katika Bandari kavu ya Kwala katika ukanda wa pwani ya Tanzania kwaajili ya shehena maalum kwaajili ya Zambia”

“Zambia itakuwa na uwezo wa kuhifadhi bidhaa kwa muda mrefu na pia hatua hii itaondoa msongamano, ucheleweshaji na kupunguza gharama za kufanya biashara nchini Zambia ikipelekea kukuza biashara kati ya Nchi zetu mbili na kutengeneza fursa za kibiashara kwa Wananchi kutokea Zambia na Tanzania na hii ni zawadi yetu kutoka Tanzania katika wakati huu wa sherehe za uhuru wa Taifa lenu”

Zambia ni Mteja mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam, ikichukua asilimia 34 ya mizigo yote inayopitia Bandari hiyo kwenda nje ya Tanzania.

Millard Ayo

----
Maoni yangu

Hadi tukifika mwaka 2030 Tanganyika itabidi kuomba uhuru upya ili tujikomboe kwa sababu nchi nzima itakuwa mikononi mwa wachache.

Je, kwanini hakutoa bure eneo la zanzibar!
Ni hekta 20(ekari 50) sio ekari 20 wewe kima wa chadomo,shule ukienda kukuza nywele?

Mwisho sio Zambia tuu hata DRC wamepewa na sio Tanzania tuu hata Kenya wametoa Kwa Wateja wao wa Bandari
 
Bahati mbaya baadhi yenu hamjui hali au changamoto za biashara duniani. Kwani hizo hekta zilizotolewa kwa Zambia si ni kwa manufaa ya Tanzania pia ? Tafakari.
Hayo majinga usiwe unahangaika kuyajibu,kimsingi hayana akili.

Mwisho sio tuu Tanzania Imetoa hata Kenya wametoa Kwa DRC,Uganda nk
 
Ni sehemu ya lengo la kujenga bandari kavu ya Kwala.

Kule bandarini hakuna ardhi ya kutosha kuwapa watumiaji bandari wakubwa mfano walivyopewa akina Malawi Cargo.

Ni kuifanya bandari ya Dar iwe efficient zaidi ili watumiaji wakubwa kama Zambia tuendelee kubaki nao.
Unajaza maji kwenye net
 
Back
Top Bottom