Rais Samia aipa Zambia ardhi hekari 20 katika bandari kavu Kwala mkoa wa Pwani

Mnatia aibu kwa hizi comment zenu hivi mnaelewa kwamba hiyo ni kwa faida ya Tanzania.
Yani kule kwenye bandari kavu ya kwala kila nchi inayopitisha mizigo kupitia bandari yetu imetengewa hekali kadhaa kwaajili ya kuhifadhi mizigo kabla ya kwenda kwenye nchi husika mfano hiyo Zambia.
Kifupi ni kwa faida yetu ni si vinginevyo.
 
Wewe ni mgeni na jf? Hili ni jukwaa la Wapinzani Sasa hivi wamepata wafuasi wao ambao ni Sukuma gang wote ni hater wa Samia
Mimi sifikirii hata kama ni wapinzani bali ni uelewa mdogo miongoni mwetu mfano angalia kwenye post ya Millardayo instagram na twitter kuhusu hii habari ndio utashangaa zaidi.
Kila mtu ni Samia kauza kipande cha ardhi kwa wazambia.
 
Je Ina tofauti na mwalimu alipotoa eneo la kunenepeshea ng'ombe kwa hayati Jumbe, mwenyekiti wa serikali ya mapinduzi?

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Wewe huwajui hawa watu wanavyopotosha mambo, Zambia wametengewa eka 20 ndani ya bandati kavu kwa mizigo yao, malipo ya huduma watazopatiwa kama kawaida.
Afadhali umenielewesha sasa nimeelewa maan Post haikuwa na maelezo ya kujitosheleza Ili mtu kuelewa kilichofanyika.
 
Tulia dada,wewe ndio unajua leo?
 
Ingekuwa heri Kwa Mbeya ingejengwa hiyo bandari kavu. Mimi na wanakijiji wenzangu tuko tayari kuwapa eneo Kwa fidia ndogo.
 
Simuelewi huyu rais. Nani kampa kibao cha kugawa ardhi ya watanzania kwa Zambia?
Miaka ya 70 Tanzania kila kona tulishuhudia kambi za wapigania uhuru hasa wa kusini mwa Afrika wakipewa ardhi na hata hivi karibuni Malawi walikuwa na bandari kavu maarufu kama Malawi cargo pale Mbeya.Hivi waliorudi makwao waliondoka na ardhi yetu?Au kuna vitu kama majengo walituachia kama nchi?Tuache siasa uchwara kwenye mambo yenye tija
 
Ndiyo mnavyojidanganya eeh? sisi tunasema Zanzibar siyo nchi na wala haitokua nchi, mlikubali wenyewe kuingia kwenye muungano au mlilazimishwa?
Sasa mbona sisi Wabara haturuhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar.
 
Bahati mbaya baadhi yenu hamjui hali au changamoto za biashara duniani. Kwani hizo hekta zilizotolewa kwa Zambia si ni kwa manufaa ya Tanzania pia ? Tafakari.
Wasikusumbue hawa. Wengi wao humu ni washamba hawajui chochote kuhusu biashara na ufanisi wa biashara duniani
 
Sasa mbona sisi Wabara haturuhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar.
Shida kubwa ni kwamba ardhi yenyewe tu hawana! lakini hawana ubavu wa kutuzuia kumiliki ardhi kwa anaetaka kwenda kuishi huko. Nakumbuka wakati wa bunge la katiba mbunge mmoja wa ZANZIBAR kwa jina SYLVESTER MASELE MABUMBA aliwahi kulalamika kwamba kule wanaonewa, Mama samia akamuuliza 'mbona wewe unamiliki shamba kubwa zaidi ya mimi?' inaonekana wapo baadi ya wadau wa huku wanaomiliki ardhi, ila siwezi kujua zaidi, nyinyi mnaojua sheria za huko inabidi mtujuze!
 
Acha gubu na nongwa! Kwani umeambiwa wamepewa waondoke na hiyo ardhi?
Sasa kama hawaondoki na hiyo Ardhi, kwanini nchi yetu iligomea ardhi kuingizwa kwenye jumuiya ya Africa mashariki? Au ndio mambo ya bendera fuata upepo?
 
Na hiki ndio anchoweza KIZIMKAZI. Watanganyika tujipange.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…