Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Huyo ana muda mwingi sana wa kutangatanga na kufanya mikutano ya kijiji kwa kijiji, baadaye anaenda Ubelgiji au Marekani kupumzika miezi miwili au mitatu na familia yake ambao ni raia wa huko... Huwezi kumlinganisha na Rais mwenye ratiba ngumu
[emoji2956][emoji2956]
 
Hizi itifaki zinamfanya rais asijue kinachoendelea on the ground... viongozi hawawezi kumfikishia vitu negative mara moja moja sio mbaya kusikiliza raia ....
Huwezi kuongoza nchi kubwa kama Tanzania kwa mfumo wa Rais kusikiliza matatizo binafsi ya watu nchi ikasonga mbele.

Wenzetu wanaojua maana ya Rais, waziri mbunge inapofanyika town Hall meeting watu wanauliza, wanatoa malalamiko yao mapendekezo kwa masuala ya mtaa, mji, jimbo au taifa. Sio malalimiko ya umenyang'anywa kiwanja na tajiri au umefukuzwa kazini ambayo ni masuala ya polisi na mahakama.
 
Sasa pale kasimama kufanya nini!?....kama anajua Mbunge yupo, why bother kusimama barabarani kusikiliza kero za wananchi?...mimi naamini kuna wananchi wameshazunguka ngazi za chini na hawapati msaada, Kiongozi wa nchi akisikiliza hizo special cases,anaweza kutoa msukumo mwananch asaidiwe.
Angetumia ndege tuu au aache kujisumbua akae ofisini asubiri wabunge wamletee haja za wananchi ka atakavyoomba kura 2025 kupitia wabunge
 
Sahihi kabisa, utaratibu wa Rais kusikiliza shida za mtu mmoja mmoja barabarani haufai
Kusikiliza si vibaya... Ila kutatua shida za mmoja mmoja ndo tatizo!
Kuna kipindi ilifikia ukiweza kupata microphone 🎤 kwenye ziara ya Rais ukatunga uongo wa kuaminika ghafla bin vuu unapigwa mahela!

Rais anatakiwa aelekeze jinsi ya kutatua shida za watu!
 
Huwezi kuongoza nchi kubwa kama Tanzania kwa mfumo wa Rais kusikiliza matatizo binafsi ya watu nchi ikasonga mbele.
Wenzetu wanaojua maana ya Rais, waziri mbunge inapofanyika town Hall meeting watu wanauliza, wanatoa malalamiko yao mapendekezo kwa masuala ya mtaa, mji, jimbo au taifa. Sio malalimiko ya umenyang'anywa kiwanja na tajiri au umefukuzwa kazini ambayo ni masuala ya polisi na mahakama.
Polisi hawa hawa? Umeshawahi kudeal na polisi hata maiti tu ya ndugu yako kupatiwa ukazike mpaka uwape kitu kidogo...
 
Uongozi Huwa ni karama.


Huyu SAMIA , ni kama tu Mwijaku, alale aamke aamue ajiunge na CCM ili mambo yake yawe sawa, kuongea ongea Mara paa anapewa UDC .


Hamna kiongozi humo
Kwani posho zenu 40,000 za kukesha usiku kushona vijeraha halmashauri huwa hawawalipi ?!!

Yaani vetting ifanyike aonekane anatosha halafu sakala mmoja asiyeweza kufanya kazi bila ya leseni ya MCT atupigie makelele koko humu JF?!!![emoji15][emoji1787][emoji1787]
 
Rais Samia leo September akiwa Nangurukuru mkoani Mtwara alisimamisha msafara wake kuongea na wananchi wa eneo hilo. Moja wananchi hao aliomba kuongea jambo ambapo Rais alimwambia mambo ni mengi na Tanzania ni kubwa.

Rais Samia alimtaka mwananchi huyo ampatie jambo lake mbunge kisha amfikishie Rais au wasaidizi wake.

Mwaka 2017 Rais Magufuli akiwa anaelekea Mtwara alisimamishwa Somanga na mwananchi aliyeelezea changamoto ya zahanati katika eneo hilo kutokamilika kwa miaka mingi. Rais Magufuli alichangia na kuamrisha ikamilike.

Alipopita tena barabara hiyo miaka 3 baadae mwananchi huyo alimzawadia jogoo na Magufuli alimsubiri mpaka alipomkamatia na kumpa. Alipofariki, mwananchi huyo alifunga safari kumzika Rais Magufuli mwaka 2021.

Rais ws matajiri anawsjobu wananchi kuwa Tanzania ni kubwa na ina mambo mengi.

Lakini Tajiri akikohoa anaitwa ikulu hata mikutano atawaandalia kuongea shida zao.

Tuna rais wa ajabu sana nawaambia. Lakini hili tukio siyo ajali, ni Mungu anatuonesha moyo wa rais wetu ulivyo
 
Kusikiliza si vibaya... Ila kutatua shida za mmoja mMoja ndo tatizo!
Kuna kipindi ilifikia ukiweza kupata microphone [emoji441] kwenye ziara ya Rais ukatunga uongo wa kuaminika ghafla bin vuu unapigwa mahela!

Rais anatakiwa aelekeze jinsi ya kutatua shida za watu!
Rais inatakiwa aweke mifumo na sera bora za kutatua matatizo ya watu, sio hata kuelekeza kutokea majukwaani.
 
Polisi hawa hawa ? Umeshawahi kudeal na polisi hata maiti tu ya ndugu yako kupatiwa ukazike mpaka uwape kitu kidogo...
Sasa Rais hawezi na hatakiwi kufanya kazi ya polisi au mahakama.
 
Haya mambo tumeyaona awamu ya tano, hakukuwa na lolote la maana
Dawa ni kuimarisha mifumo iliyopo tu la sivyo itakuwa kutwanga maji kwenye kinu na kutafuta sifa za bei rahisi
Unairudishaje sokoni nyanya iliyooza?
 
Back
Top Bottom