Rais Samia akiingia katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar

Rais Samia akiingia katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar

Mwaka kesho atakuwa na kampeni kuzunguka nchi nzima kuomba kura kwa watanzania wamchague kuwaongoza, tunamtakia afya njema na nguvu tele kuweza kufanya kampeni vema
Atakuwa raisi wa ngapi na awamu ya ngapi please
 
Kazi iliyopo na inayofanyika na kufanywa na Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge ni kuwaletea maendeleo watanzania,ni kuwainua na kuwakwamua kiuchumi Watanzania,ni kuhakikisha rasilimali zetu zinatumika katika kuboresha maisha ya watanzania .Mama anafanya kazi ya kuhakikisha watanzania wanapata milo mitatu iliyo bora mezani pao.Mama yupo kazini kuleta matumaini na tabasamu katika nyuso na mioyo ya mamilioni ya watanzania.hiyo ndio kazi kubwa aliyonayo Mama yetu Mpendwa Tumaini la watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Funga mdomo watu wana njaa hawana ajira wewe unabwabwaja tu. Toka hapa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ukimuangalia Rais Samia Unagundua ya kuwa Muda wote amejaa ari,nguvu na hamasa kubwa sana ya kufanya kazi. Unaona muda wote akiwa na morali na utayari wa kuwatumikia watanzania.unaona muda wote mawazo,akili,fikira na kiu yake ni kuwatumikia na kuwawazia watanzania.

Unaona Mungu akiendelea kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.yupo imara kila muda na mwenye nguvu Utafikiri kijana wa miaka 30.Huyu Mama na Rais ni Bahati sana kuwa naye na kuongozwa naye.yupo imara kiakili na kimwili.

Embu angalia Alivyoingia na kuelekea katika kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri ikulu ndogo ya Tunguu visiwani Zanzibar hii leo.Hatua zake na mwendo wake na hata muonekano wake ni wakuleta matumaini kwa watanzania.Ni wakuleta tabasamu katika maisha ya watanzania.unaona wazi kwa jicho la tatu kuwa Huyu ni kiongozi tuliyemhitaji watanzania kutuongozaView attachment 3135089

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ninachowaza litokee kuhusu hili kusanyiko, ngoja nikatubu tu
 
Tupate Rais Mchaga au Mhaya sasa ili vikao vya baraza la mawaziri viwe vinafanyika Machame ndani ndani huko, au Muleba pale..
 
Hivi lakini wewe Lucas, mkeo, watoto wako au mama yako anajua kwamba kuna mtu una-muabudu kama Mungu huku - kutwa kuchwa kusifia hata visivyosifika ? Wanajua kuwa ndugu yao akili zake zote kawekeza kwenye uchawa na kutukuza watu??
 
Mimi siyo chawa
 
Dua zangu mama akuone upate teuzi Lucas maana unatumia calories nyingi sanaa.

Nimesoma maoni ya wadau na comment one after one.

🙏🙏
 
Nchi ya zbar ina ikulu za nchi 2 tofauti, zenye wimbo na bendera tofauti za taifa.

Yaani Zambia wameandaa kikao cha mawaziri Tunduma
 
Kazi iliyopo na inayofanyika na kufanywa na Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge ni kuwaletea maendeleo watanzania,ni kuwainua na kuwakwamua kiuchumi Watanzania,ni kuhakikisha rasilimali zetu zinatumika katika kuboresha maisha ya watanzania .Mama anafanya kazi ya kuhakikisha watanzania wanapata milo mitatu iliyo bora mezani pao.Mama yupo kazini kuleta matumaini na tabasamu katika nyuso na mioyo ya mamilioni ya watanzania.hiyo ndio kazi kubwa aliyonayo Mama yetu Mpendwa Tumaini la watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
😀😀😀😀😀😀😭
 
Back
Top Bottom