Rais Samia akiingia katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar

Rais Samia akiingia katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar

Atakuwa raisi wa ngapi na awamu ya ngapi please
rais wa awamu ya sita, awamu ya kwanza, awamu ya pili ni 2030 mpaka 2035. labda aamue kuishia awamu mmoja tu. hii awamu inayoisha mwaka kesho haihesabiki kama ni awamu yake
 
Yani ukisoma hizo comment unapata picha jinsi watu walivyo kuwa wamekata tamaa.
 
Atakuwa raisi wa ngapi na awamu ya ngapi please
mwaka kesho ndiyo mama anatakiwa kuanza awamu yake ya kwanza hadi 2030, kisha amalize mihula miwili 2035. Hapa anamalizia awamu ya rais wa tano, awamu zake bado hazijaanza
 
Kikao cha baraza la mawaziri la Tanganyika kinafanyika Zanzibar chini ya Mzanzibari! Watanganyika safari hii tumepatikana.
 
mwaka kesho ndiyo mama anatakiwa kuanza awamu yake ya kwanza hadi 2030, kisha amalize mihula miwili 2035. Hapa anamalizia awamu ya rais wa tano, awamu zake bado hazijaanza
Hayo ni mawazo yako lakini kwa mujibu wa Katiba muda aliotumikia unahesabika kuwa ni awamu kamili labda wabadilishe Katiba au waamue kuvunja Katiba. Pascal Mayalla hebu mpe darasa kijana.
 
Attachments

  • IMG-20240903-WA0004.jpg
    IMG-20240903-WA0004.jpg
    53.6 KB · Views: 2
Hayo ni mawazo yako lakini kwa mujibu wa Katiba muda aliotumikia unahesabika kuwa ni awamu kamili labda wabadilishe Katiba au waamue kuvunja Katiba.
nec ya chama chake ilimpitisha lini, alishindanishwa na kina nani ndani ya chama chake, alipigiwa kura na nani? Katiba haisemi kuwa huu ni muhula wake wa kwanza au wa pili. Muhula wake wa kwanza unatakiwa uanze mwaka kesho. Labda muhula wa pili aseme hatagombea kwa kuwa hii miaka minne aijazie huko mbeleni ionekane ni mihula miwili! Sasa mbona itakuwa haijakamilika miaka? Itakuwa ni miaka tisa badala ya kumi iliyokamilika mihula miwili.
 
Katiba imefafanua vizuri juu ya jambo hili sasa kulibishia unajidhalilisha tu mkuu, bahati mbaya hapa nilipo sina Katiba ningeinukuu kama ilivyo kwani inajibu hizo hoja zako.Ni vizuri kubishana kwa jambo unalolielewa ili usijivue nguo hadharani.
 
Hivi na wewe una akili kichwani ya kuweza kuielewa hata katiba?
Lucas ukitaka kujilinganisha na mimi kwa siasa za nchi hii na za CCM ni kama kulinganisha mlima Kilimanjaro na kichuguu wewe ukiwa kichuguu. Usione nakujibu kihuni ni kwa vile nakuona una akiherere tu cha kutaka uteuzi ilhali wewe bado ni mchanga sana na zaidi ya yote wewe ni mshamba tu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ukimuangalia Rais Samia Unagundua ya kuwa Muda wote amejaa ari,nguvu na hamasa kubwa sana ya kufanya kazi. Unaona muda wote akiwa na morali na utayari wa kuwatumikia watanzania.unaona muda wote mawazo,akili,fikira na kiu yake ni kuwatumikia na kuwawazia watanzania.

Unaona Mungu akiendelea kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.yupo imara kila muda na mwenye nguvu Utafikiri kijana wa miaka 30.Huyu Mama na Rais ni Bahati sana kuwa naye na kuongozwa naye.yupo imara kiakili na kimwili.

Embu angalia Alivyoingia na kuelekea katika kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri ikulu ndogo ya Tunguu visiwani Zanzibar hii leo.Hatua zake na mwendo wake na hata muonekano wake ni wakuleta matumaini kwa watanzania.Ni wakuleta tabasamu katika maisha ya watanzania.unaona wazi kwa jicho la tatu kuwa Huyu ni kiongozi tuliyemhitaji watanzania kutuongozaView attachment 3135089

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Siku hizi machawa ndio waandishi wa Rais....kweli urahisi umekuwa rahisi sana...
 
Katiba imefafanua vizuri juu ya jambo hili sasa kulibishia unajidhalilisha tu mkuu, bahati mbaya hapa nilipo sina Katiba ningeinukuu kama ilivyo kwani inajibu hizo hoja zako.Ni vizuri kubishana kwa jambo unalolielewa ili usijivue nguo hadharani.
hebu eleza kwa kifupi tu, katiba inasemaje kama makamu wa rais atakuwa rais, lets say kama mama angechukua madaraka ikiwa imebaki muda wa miaka miwili kumalizika kwa muhula wa mtangulizi wake. Hiyo miaka miwili itajumuishwa kuwa ni awamu yake? Katiba ninayo ila sijafungua nisome ibara hiyo kuhusu makamu wa rais anapokuwa rais pindi rais aondokapo madarakani kama ilivyotokea. Tuelimishane, hii miaka minne ni awamu ya rais samia kwa mujibu wa katiba?
 
Back
Top Bottom