Rais Samia akikupa mualiko Ikulu wa dakika 5 utamshauri nini kama kijana wa kitanzania?

ushauri utamfikia chief
 
Nitatumia huo mda kumshauri anipe siku nzima ya kumshauri
Kwa sababu naamini dakika 5 haziwezi kufua dafu
Lakini kama hatokubali ushauri wangu huo wa kunipa mda zaidi wa kumshauri nitamuomba awe anafuatilia kijiwe changu cha kumshauri mtandaoni ambacho nitaenda kucreate baada ya kutoka hapo Magogoni
Nadhani dakika 5 zitakuwa zimeisha

Lakini akikubali ushauri wa kunisikiliza kwa siku nzima ni story ndefu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
weka summary wa hicho kijiwe cha ushauri
 
Naomba raisi mtukufu nipe kwanza huo mwaliko nitafurahia sana,jambo la kumshauri ni Siri yangu mimi siyo mtu mropokaji kihivyo
 
Nini hatma ya mitaji tuliowekeza kwenye viwanda ambavyo wakati wa COVID vilishindwa kutulipa pesa zetu? Kwa ushauri kuwe na mfuko maalum wa kufufua viwanda hivi kwa mfumo wa bail out programme, ambapo serikali itoe long term loans kwa riba nafuu ili viwanda hivi virudi katika uzalishaji. Mimi yangu ni hayo tu. Otherwise, mambo mengine Mama apewe maua yake.
 
Anipe mchongo wa kulamba asali kwanza. Mengine ni ziada tu
 
"Pamoja na kelele nyingi kwamba mateso yapo lakini kila kukicha watu wanapanda ndege wanakwenda, na msingi unaowaongoza ni uleule kheri nife nikijaribu kuliko kukaa naangamia bila kujaribu kwa sababu ambazo hazina mashiko, na ndiyo maana serikali zetu zimeingia mikataba hii ili kuweka mazingira mazuri ya watu kwenda, yeyote anayetaka kwenda kufanya kazi nje afuate utaratibu kwa kupata uthibitisho wa hiyo ajira,"- Balozi Abdallah Kilima

#MkutanoIkulu
#EastAfricaTV
 
Arejesha fedha za mauzo ya Bandari na fedha za mauzo ya Ngorongoro.
 
sio kweli. mama anajenga nchi , karibu kumshauri
Huenda anajenga ila mimi sijaona maana tunatofautiana uwezo wa kuona. Kuhusu kumshauri siwezi maana hatonielewa ila ikiwa lazima kumshauri nitamwambia arudishe bandari zetu na ajiuzulu apelekwe mahakamani ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi na kufuga majizi.
 
Ningempongeza kwa kazi nzuri. Ningemshauri asimamie zile 4R kwa vitendo zaidi. Legacy yake iko kwenye hizo na benchmark isiwe awamu ya tano. She can do better than all the previous presidents.
 
Nitachomshauri ni kwamba
(1) Asiwaamini mawaziri wake kwamba wanauwezo wa kutumia akili zao kwa manufaa ya nchi, wengi kama sio wote wanaweka maslahi yao binafsi mbele.

(2) atawale kwa mkono wa chuma kama mtangulizi wake sababu hii nchi hamna kiongoz anaeweza kujiongoza.
 
Ningempongeza kwa kazi nzuri. Ningemshauri asimamie zile 4R kwa vitendo zaidi. Legacy yake iko kwenye hizo na benchmark isiwe awamu ya tano. She can do better than all the previous presidents.
very good chief, 4R ninini nami nizijue ?
 
ushauri mzuri sana chief
 
Atuangalie na sisi wasomi tusio na ajira kama akishindwa kutuajiri basi atukabidhi ardhi tijikite kwenye kilimo watupe mitaji pia atuweke miundo mbinu wezeshi pamoja na kutuandalia soko la nje. Tulime mazao ya biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…