Rais Samia akikupa mualiko Ikulu wa dakika 5 utamshauri nini kama kijana wa kitanzania?

Awamu ya sita ya mama Samia tumeona mengi yakifanyika ikiwemo utekelezaji wa miradi ya umwangiliaji ya kilimo, BBT, Ruzuku ya mbolea, Afya, Ajira, Veta, kupandishwa madaraja kwa watumishi nk

Lakini pia zipo changamoto kadha wa kadha ambazo watanzania wanatamani wamfikishie Rais wao, nao wajione ni sehemu ya watanzania wanaofaidi matunda ya nchi hii!

Rais amekupa dakika tano tu umpongeze na umshauri kipi kiboreshwe ama kiongezeke kwenye utawala wake ili kila mtu ajivunie kuwa mtanzania, utazungumza nini?
Asiwape madaraka wahuni. Najua mzenji mama yetu sio muhuni.
 
Siyo changamoto ni woga na kuwalinda maswahiba, namshauri
  1. Awachukulie hatua waliotajwa kwenye report ya CAG ikibidi afumue namkusuka upya baraza la mawaziri
  2. Aboreshe maslahi na mafao ya watumishi wa umma ili kuboresha utendaji kazini
  3. Aachane na timu ya wale jamaa wa Chalinze
  4. Tupate katiba mpya ili kuondokana na hii adha ya kuchezewa na wajanja wachache
ushauri mzuri chief
 
Ningempongeza kwa yote aliyoyafanya
Ushauri wangu ungekua kwenye maeneo haya;
 AFYA
Afanye mpango kuwepo na upatikanaji wa bima ya afya kwa wote na ikiwezekana kusiwepo na uchaguzi wa huduma kulingana na uchangiaji, kila mtu akatwe kulingana na mapato yakena wasio na kipato kabisa serikali isimamie michango yao, uwekezaji zaidi katika sekta ya afya kwa upande wa public na udhibiti kwa upande wa private. Madaktari, watumishi wa afya na vifaa tiba kwa wingi kadri inavyowezekana.
ELIMU.
Nashauri suala la elimu ya juu liangaliwe vizuri zaidi, tuition fees zinaumiza sana, na mkopo wenyewe umekua mdogo sana, magumashi ni mengi pia, utoaji hauzingatii vigezo na sifa za muombaji kulinganisha na hali aliyonayo ndo vile unaskia mtu Yatima ana div 1 tena science studies na hapati mkopo, uwezeshaji zaidi kwenye masomo ya ufundi, kilimo na sanaa (kwa sasa ameonesha dira ila matokeo bado hayajaanza kuonekana), lakini pia elimu jamii na maadili kwa wanafunzi wa ngazi zote ipewe kipaumbele, hakuna uwajibikaji kwa wanafunzi kwa asilimia kubwa katika ngazi zote, wengi tunasoma ili kupata ajira na maisha mazuri na kundi kubwa zaid hata halielewi kwanini linasoma, ndo hilo baadhi yao kutwa na kulalama na kutukana tu 😁, na hata wanaotoboa ndo huja kuwa wezi katika mali za umma.
UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI NA UZALENDO
Mzee baba katika sehemu aliwahi kuziweka vizuri mapema ni suala la ufuatiliaji wa masuala na shughuli za serikali, kuna stori kuwa aliajiri usalama wa taifa kila mahali hivyo kupata taarifa haraka vile jinsi mambo yanavyokwenda, nahisi Mama hapa anakwama sana, intelijensia yake bado ina watu wengi wa michongo wanampoteza,
Pia suala la kuwajibika na kuwawajibisha wote wanaofanya vizuri na vibaya pia, hili kwa Tanzania yetu bado tuko nyuma sana, hata chuma aliishia kutumbua tu ila action baada ya hapo hatukuziona watu walipotelea hewani tu. Tumbua na funga jela ili wengine waogope na wanaofanya vizuri ziwepo zawadi na motisha za wazi kabisa kwa utumishi wao. Uzalendo sasa dah...............................................
 
ujumbe wako umepokelewa chief , pia jali afya kwenye hizo mbuno .
Nijali afya ya nini wacha nile mbuno tu mkuu, nikianza kujali afya ndio hapo restrictions zinaoozaliwa mara asiukalie atauvunja ukuni, mara tusinyonye papuchi na jirani yake, mara tuvae mifuko ya nylon, tule pipi na miganda yake. Mara usimuinamishe utamsogeza kizazi.. Tafrani tu.
Acha tule burudani mkuu.
(utani tu) 🤣😂😂
 
1. Ishu ya umeme, yani haingii akilini tatizo la umeme lilikuwa limeisha kwa miaka kadhaa nyuma alafu kwa sasa limerudi kwa kasi sana inamaana mwendazake aliweza vipi kudhibiti hili tatizo so ukituzama kiundani utaona kuna shida mahali alafu yeye hajalitilia manani.
 
Ningempongeza kwa yote aliyoyafanya
Ushauri wangu ungekua kwenye maeneo haya;
 AFYA
Afanye mpango kuwepo na upatikanaji wa bima ya afya kwa wote na ikiwezekana kusiwepo na uchaguzi wa huduma kulingana na uchangiaji, kila mtu akatwe kulingana na mapato yakena wasio na kipato kabisa serikali isimamie michango yao, uwekezaji zaidi katika sekta ya afya kwa upande wa public na udhibiti kwa upande wa private. Madaktari, watumishi wa afya na vifaa tiba kwa wingi kadri inavyowezekana.
ELIMU.
Nashauri suala la elimu ya juu liangaliwe vizuri zaidi, tuition fees zinaumiza sana, na mkopo wenyewe umekua mdogo sana, magumashi ni mengi pia, utoaji hauzingatii vigezo na sifa za muombaji kulinganisha na hali aliyonayo ndo vile unaskia mtu Yatima ana div 1 tena science studies na hapati mkopo, uwezeshaji zaidi kwenye masomo ya ufundi, kilimo na sanaa (kwa sasa ameonesha dira ila matokeo bado hayajaanza kuonekana), lakini pia elimu jamii na maadili kwa wanafunzi wa ngazi zote ipewe kipaumbele, hakuna uwajibikaji kwa wanafunzi kwa asilimia kubwa katika ngazi zote, wengi tunasoma ili kupata ajira na maisha mazuri na kundi kubwa zaid hata halielewi kwanini linasoma, ndo hilo baadhi yao kutwa na kulalama na kutukana tu 😁, na hata wanaotoboa ndo huja kuwa wezi katika mali za umma.
UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI NA UZALENDO
Mzee baba katika sehemu aliwahi kuziweka vizuri mapema ni suala la ufuatiliaji wa masuala na shughuli za serikali, kuna stori kuwa aliajiri usalama wa taifa kila mahali hivyo kupata taarifa haraka vile jinsi mambo yanavyokwenda, nahisi Mama hapa anakwama sana, intelijensia yake bado ina watu wengi wa michongo wanampoteza,
Pia suala la kuwajibika na kuwawajibisha wote wanaofanya vizuri na vibaya pia, hili kwa Tanzania yetu bado tuko nyuma sana, hata chuma aliishia kutumbua tu ila action baada ya hapo hatukuziona watu walipotelea hewani tu. Tumbua na funga jela ili wengine waogope na wanaofanya vizuri ziwepo zawadi na motisha za wazi kabisa kwa utumishi wao. Uzalendo sasa dah...............................................
ushauri mzuri chief, hope ameona
ada elimu ya juu ni jipu sana aiseeh
 
1. Ishu ya umeme, yani haingii akilini tatizo la umeme lilikuwa limeisha kwa miaka kadhaa nyuma alafu kwa sasa limerudi kwa kasi sana inamaana mwendazake aliweza vipi kudhibiti hili tatizo so ukituzama kiundani utaona kuna shida mahali alafu yeye hajalitilia manani.
tatizo la umeme kiukweli linakwamisha wajasiriamali wadogo, vijana walio jiajiri nk

ushauri kaupokea
 
Awamu ya sita ya mama Samia tumeona mengi yakifanyika ikiwemo utekelezaji wa miradi ya umwangiliaji ya kilimo, BBT, Ruzuku ya mbolea, Afya, Ajira, Veta, kupandishwa madaraja kwa watumishi nk

Lakini pia zipo changamoto kadha wa kadha ambazo watanzania wanatamani wamfikishie Rais wao, nao wajione ni sehemu ya watanzania wanaofaidi matunda ya nchi hii!

Rais amekupa dakika tano tu umpongeze na umshauri kipi kiboreshwe ama kiongezeke kwenye utawala wake ili kila mtu ajivunie kuwa mtanzania, utazungumza nini?
Wimbo wa taifa uimbwe kwa staili ya singeli au amapiano
 
Back
Top Bottom