Ningempongeza kwa yote aliyoyafanya
Ushauri wangu ungekua kwenye maeneo haya;
AFYA
Afanye mpango kuwepo na upatikanaji wa bima ya afya kwa wote na ikiwezekana kusiwepo na uchaguzi wa huduma kulingana na uchangiaji, kila mtu akatwe kulingana na mapato yakena wasio na kipato kabisa serikali isimamie michango yao, uwekezaji zaidi katika sekta ya afya kwa upande wa public na udhibiti kwa upande wa private. Madaktari, watumishi wa afya na vifaa tiba kwa wingi kadri inavyowezekana.
ELIMU.
Nashauri suala la elimu ya juu liangaliwe vizuri zaidi, tuition fees zinaumiza sana, na mkopo wenyewe umekua mdogo sana, magumashi ni mengi pia, utoaji hauzingatii vigezo na sifa za muombaji kulinganisha na hali aliyonayo ndo vile unaskia mtu Yatima ana div 1 tena science studies na hapati mkopo, uwezeshaji zaidi kwenye masomo ya ufundi, kilimo na sanaa (kwa sasa ameonesha dira ila matokeo bado hayajaanza kuonekana), lakini pia elimu jamii na maadili kwa wanafunzi wa ngazi zote ipewe kipaumbele, hakuna uwajibikaji kwa wanafunzi kwa asilimia kubwa katika ngazi zote, wengi tunasoma ili kupata ajira na maisha mazuri na kundi kubwa zaid hata halielewi kwanini linasoma, ndo hilo baadhi yao kutwa na kulalama na kutukana tu 😁, na hata wanaotoboa ndo huja kuwa wezi katika mali za umma.
UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI NA UZALENDO
Mzee baba katika sehemu aliwahi kuziweka vizuri mapema ni suala la ufuatiliaji wa masuala na shughuli za serikali, kuna stori kuwa aliajiri usalama wa taifa kila mahali hivyo kupata taarifa haraka vile jinsi mambo yanavyokwenda, nahisi Mama hapa anakwama sana, intelijensia yake bado ina watu wengi wa michongo wanampoteza,
Pia suala la kuwajibika na kuwawajibisha wote wanaofanya vizuri na vibaya pia, hili kwa Tanzania yetu bado tuko nyuma sana, hata chuma aliishia kutumbua tu ila action baada ya hapo hatukuziona watu walipotelea hewani tu. Tumbua na funga jela ili wengine waogope na wanaofanya vizuri ziwepo zawadi na motisha za wazi kabisa kwa utumishi wao. Uzalendo sasa dah...............................................