Rais Samia akiri Watanzania hawana furaha

Rais Samia akiri Watanzania hawana furaha

Nchi zenye furaha duniani utaona hata wanawake wanafuraha na wazuri pia
Utafiti huo sio mimi
Waliofika Finland, Denmark, Norway au Iceland watanielewa

Hivi mna furaha gani kutwa mnalalamika humu?
Hata yeye anawachora humu wakataa ndoa 😄
 
Attachments

  • Screenshot_2024-03-10-16-13-56-30.png
    Screenshot_2024-03-10-16-13-56-30.png
    92 KB · Views: 3

Akiwaapisha wateule Ikulu, Rais Samia Kwa kinywa chake amekataa article ya kitapeli inayosemwa Tanzania ni ya 3 Kwa wananchi wake kuwa na furaha.

Rais Samia amekataa utafiti huo uchwara na kusema Watanzania hawana furaha.

Kwahiyo Wananzengo mpaka Rais anajuwa Watanzania tunaishi kama tupo jela tu.

Habari ndio hiyo.
Kataa Chawa wa mama Hizo ndio report zao
 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar mh Othman Masoud alisema juzi kuwa Zanzibar hakuna Amani kuna Ukimya

Leo Rais kasema Watanzania hawana Furaha

Ndio nauliza Watanzania wanapendana?

Amani, Upendo, Furaha ni zao la Haki, je Haki ipo nchini?!

Ramadan Kareem 😄
 
Mleta mada wewe ni muongo maana nipo hapa Ikulu. Amesema hiyo article inasema Tanzania ni ya 4 sio 3. Na ameagizwa wateule wake wafanye kazi Watanzania wapande juu (hakutaja namba) Kwa watu wenye furaha.
 
Furaha itatoka wapi wakati bidhaa zote bei juu? Mjini foleni kibao na joto hili! Sehemu nyingi maji bado ni kitendawili. Shuleni michango ni kero tupu. Ada vyuoni kwa wasio na mikopo ndio usiseme. Trafiki nao kosa moja faini. Hospitali iwe ya serikali au binafsi foleni tu wagonjwa ni wengi. mahakamani haki zinaminywa kupendelea wenuye nacho. Madeni ya ndani serikali hailipi ipasavyo. Tumshukuru Mungu kwa uhai lakini maisha nchi hii hayana faraja hata kidogo. Hata wenye nacho watafurahi vipi wakati wengi wetu tunasononeka?
 
Akiwaapisha wateule Ikulu, Rais Samia Kwa kinywa chake amekataa article ya kitapeli inayosemwa Tanzania ni ya 3 Kwa wananchi wake kuwa na furaha.

Rais Samia amekataa utafiti huo uchwara na kusema Watanzania hawana furaha.

Kwahiyo Wananzengo mpaka Rais anajuwa Watanzania tunaishi kama tupo jela tu.

Habari ndio hiyo.
Nilitaka nishangae Watanzania wapate wapi furaha wakati huku kuna Tanesco, kushoto kuna CCM, kulia kuna uhaba wa maji, mbele kiddogo vifurushi vya Internet bei juu.

Mademu wenyewe pasua kichwa, hiyo furaha ni ndoto aisee
 
Akiwaapisha wateule Ikulu, Rais Samia Kwa kinywa chake amekataa article ya kitapeli inayosemwa Tanzania ni ya 3 Kwa wananchi wake kuwa na furaha.

Rais Samia amekataa utafiti huo uchwara na kusema Watanzania hawana furaha.

Kwahiyo Wananzengo mpaka Rais anajuwa Watanzania tunaishi kama tupo jela tu.

Habari ndio hiyo.
Kuna yule mpumbavu wa kuitwa ChoiceVariable jana nilimwambia aache kukubaliana na kila utafiti uchwara, nadhani akipita hapa hatakubali kuacha akili zake nyumbani.
 
DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amesema utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ndio sababu iliyompa nafasi ya kuaminiwa zaidi na kupandishwa cheo.
-
Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uapisho wa viongozi walioteuliwa hivi karibuni uliofanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Rais amesema Tamisemi wameanza utaratibu wa kupima viwango vya utendaji kwa watumishi ili kujua nani anafanya nini katika nafasi yake.
-
“Kwa mujibu wa tathimini iliyofanywa na Tamisemi Chacha ulionekana kufanya vizuri sana na ndio maana tumeona tukupandishe kutoka kuwa mkuu wa wilaya hadi mkuu wa mkoa”amesema Rais Samia
-
Rais Samia amemtaka mkuu huyo wa mkoa kuzimaliza changamoto zilizopo mkoani Tabora kwani hana ugeni na mkoa huo. Amesema akasimamie vyema mazao ya kilimo kwani mkuo huo ni wazalishaji wazuri wa mazao hayo.
-
Ikumbukwe kabla ya uteuzi huo Chacha alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.
-
Imeandaliwa na Antipas Kavishe

-
#HabariLeoUPDATES
 
Back
Top Bottom