Rais Samia akiri Watanzania hawana furaha

Rais Samia akiri Watanzania hawana furaha

Akiwaapisha wateule Ikulu, Rais Samia Kwa kinywa chake amekataa article ya kitapeli inayosemwa Tanzania ni ya 3 Kwa wananchi wake kuwa na furaha.

Rais Samia amekataa utafiti huo uchwara na kusema Watanzania hawana furaha.

Kwahiyo Wananzengo mpaka Rais anajuwa Watanzania tunaishi kama tupo jela tu.

Habari ndio hiyo.
Lucas mwashambwa anasemaje
 
Chawa ambao walikuwa wanatoa sifa kede kede,kwamba chini ya mama watu wanacheka kwa furaha watabadili msemo chap kuendana na kauli ya boss.
 
Ongeza bidii huenda ukaambulia visenti kwenye kampeni za serikali za mtaa.
serikali za mitaa nipo,
na nitakuepo kikamilifu kuhakikisha viongozi makini, wenye sifa, wabunifu, waadilifu, mahiri na wanaokubalika na wananchi katika kuwaletea tabasamu waTanzania wote wa eneo husika, ndio wanachaguliwa kuongoza wenzao kwa weledi bila mbambamba 🐒

Na kwa Neema na Baraka za Mungu na 2025 katika kumpatia mtanzania kicheko ntakuepo vilevile,
Kwan nini mbaya na kuna shida gan🐒
 
Akiwaapisha wateule Ikulu, Rais Samia Kwa kinywa chake amekataa article ya kitapeli inayosemwa Tanzania ni ya 3 Kwa wananchi wake kuwa na furaha.

Rais Samia amekataa utafiti huo uchwara na kusema Watanzania hawana furaha.

Kwahiyo Wananzengo mpaka Rais anajuwa Watanzania tunaishi kama tupo jela tu.

Habari ndio hiyo.
Amekataa kwa kusema nini. We ni dk wa nini
 
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar mh Othman Masoud alisema juzi kuwa Zanzibar hakuna Amani kuna Ukimya

Leo Rais kasema Watanzania hawana Furaha

Ndio nauliza Watanzania wanapendana?

Amani, Upendo, Furaha ni zao la Haki, je Haki ipo nchini?!

Ramadan Kareem [emoji1]
Hii ilitakiwa iwe thread kabisa.

Tupeana mwaliko wa kufuturu.
 
Anajua watakuaje na furaha wakati wanaamka saa 9 usiku kufuata maji umbali wa km 10+, wakienda hospital tena za serikali bila pesa hutibiwi wakikuonea huruma watakupa panadol hata kama una malaria kali, sukari ndio usiseme kila mfanyabiashara ana bei yake na hakuna wa kuwagusa, bado kuna chawa wanamsifia uongo kwa ajili ya kujaza utumbo mpana wao, umeme sio wa uhakika, mfumuko wa bei, nauli za usafiri wa umma zimepanda wakati mishahara ipo palepale, kuwa mbunge angalao ujue kusoma na kuandika halafu mbunge huyo huyo anategemewa kutunga sheria inayoenda kusimamiwa wanasheria wasomi, ripoti za CAG za miaka yote wahusika wapo mtaani wanadunda na hakuna wa kuwagusa.

Barabara mbovu baada ya mvua za El nino hazijakarabatiwa ni porojo kila kukicha.
 
ndiyo, ni kweli
hiyo ni kumaanisha furaha yake Rais, comrade DR SSH, na ya waTanzania wote ni kuona maji safi na salama yanapatikana kwa uhakika na yanawafikia waTanzania wote popote walipo 🐒

Furaha yake na ya waTanzania wote nikuona hudumu za afya, nishati na elimu zinapatikana kwa uhakika na kuwatosheleza waTanzania wote popote walipo 🐒

na katika hudumu nyingine zote unazozifahamu kiuchumi, kijamii na kisiasa , Rais angependelea hao alowaapisha na watendaji wengine kufanya bidii zaidi na kupeleka tabasamu ya huduma za uhakika kwa wanainchi na hatimae CHEKO KAMILI la haja Oct.2025🐒
Chawa wa mama kazini. Akigeuka na nyie mnageuka.
 
Akiwaapisha wateule Ikulu, Rais Samia Kwa kinywa chake amekataa article ya kitapeli inayosemwa Tanzania ni ya 3 Kwa wananchi wake kuwa na furaha.

Rais Samia amekataa utafiti huo uchwara na kusema Watanzania hawana furaha.

Kwahiyo Wananzengo mpaka Rais anajuwa Watanzania tunaishi kama tupo jela tu.

Habari ndio hiyo.
Yeye ndo alipaswa kutufanya tuwe na furaha alkini wwpi
 
Back
Top Bottom