Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Una elimu gani mkuu?? Kwahiyo aliyekuwa analipwa 330000 mwanzoni ataendelea kulipwa hivyo kwa akili yako?
Nyongeza ya mishahara inasetiwa kwa kima cha chini ili kubalance kule juu, hivyo nyongeza ya kima cha chini maana yake unawasogeza wengine juu zaidi.
Mbona yy ametolea ufafanuzi mzuri tu we ndo hujamjelewa ambapo hujasema kuwa nawe umetumia Elimu gani kumuelewa!
 
Bila kubisha andiko lina utata mkubwa.

Hapo hakukuwa na ulazima wa kutaja kauli ya
"ikiwemo kima cha chini"

Kama wengine walivyotangaza kuwa ongezeko ni kwa asilimia kadhaa. Hapo kila mtu ngeelewa kiasi atakacho ongezewa.

Kutaja kima cha chini pekee kunaweza kukuta watu wanaongezeana mishahara kwa kupendeleana tu na wengine wakaongezwa kidogo sana na huna pa kuanzia kudai.

Kwa mfano wewe sio wa kima cha chini ukikuta unaongezeko la asilimia tano utaanzia wapi kudai kuwa umepunjwa ?

Hii nchi ni bora tuanze kuona namna ya kujiongezea vipato kwa kuangalia kazi nje ya kazi rasmi.
 
23.3% Kwa kima cha chini maana yake ni NYONGEZA KWA LEVEL ZOTE, KUANZIA CHINI.
Ndiyo ni nyongeza kwa level zote lakini kwa viwango mbali mbali!! Anayepata milioni 10 hawezi kuongezewa asilimia 23.3. Asilimia itapungua!! Ila nadhani haiwezi kushuka chini ya asilimia 10.
 
Hebu ngoja hapa:-
23.3/100=0.233
0.233×270000/= =62,910
KWA hiyo:-
270000+62910=332,910/=
KWA kima cha CHINI hicho!!
Nakaribisha masahihisho kama yapo!!
Mimi Raisi ajaye nimeona hivi KWA lima cha CHINI ya wewe je!!?
 
Ndiyo ni nyongeza kwa level zote lakini kwa viwango mbali mbali!! Anayepata milioni 10 hawezi kuongezewa asilimia 23.3. Asilimia itapungua!! Ila nadhani haiwezi kushuka chini ya asilimia 10.
Kwanini isishuke ?

We unayepata kwa mfano Tsh 500 000/= unaijua haki yako ya nyongeza ? Na kwanini usiambiwe ? Ukipata asilimia 2 utaona sawa ? Utadai wapi ?
 
Tunakamuana ili kulipana mishahara tu.

Miradi ya maendeleo imelala huko.

Watu tunawaza kula tu.
ni haki yao, wewe na mimi tusio watumishi wa umma pia tutafaidika kupitia shughuli tunazofanya! Hata hivyo katika hiyo mishahara watumishi wanalipa kodi inayotumika kwenye hiyo miradi ya maendeleo! Acha roho mbaya mkuu
 
Watanzania walivyo WAPUMBAVU wapo ambao watapinga na kutoka kejeli hata kwa hili la kuongeza mishahara kwa 23.3% tena TZ ikiongoza kwa nyongeza kubwa zaidi ya Mishahara EAC.
Tena siyo EAC tu, nadhani ni zaidi ya EAC. Ghana walikua juu, nadhani walikua 17%. Lakini mkuu, hii ni kwa sababu watu wamekaa 6+ bila ongezeko. Hizo nchi zingine walikua wakiongezewa. Hii ndiyo madhara ya kukaa miaka mingi bila kuongeza mishahara. Kwa hiyo hii 23% inaweza isiwe na impact kubwa ukilinganisha na nchi zingine za EAC ambazo wameongezewa mara kwa mara. Kenya wameongezewa 12% safari hii.
 
Naomba ifahamike thamani ya pesa ni purchasing power Yan uwezo wake wa kununua bidhaa na huduma Kwa hili ya mfumuko wa bei ulivyo Kwa sasa hili ongezeko kubwa lisipoambatana na kutunza thamani ya pesa Kwa kudhibiti mfumuko wa bei basi hzi jitihadi naweza kuwa kama kukojoa hewani Yan matokeo kidogo kwenye uchumi wa mfanyakazi Mmoja mmoja.maendeleo hayana chama,naomba kuwasilisha
 
Hebu ngoja hapa:-
23.3/100=0.233
0.233×270000/= =62,910
KWA hiyo:-
270000+62910=332,910/=
KWA kima cha CHINI hicho!!
Nakaribisha masahihisho kama yapo!!
Mimi Raisi ajaye nimeona hivi KWA lima cha CHINI ya wewe je!!?
Kima cha juu ni kipi
 
Back
Top Bottom