Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Waajiriwa 1,000,000 v/s watanzania 59mil waliopo katika mfumo usio rasmi,na ambao kilio chao hawafahamu pa kukipeleka.
•Magu aliangalia sana hapa!
Ni kwasababu tu ya ubinafsi wake,na roho mbaya. Hakuna mtu haitaji masilahi juu ya shughuli yake anayoifanya.

Wafanyakazi wakiongezewa mshahara ni moja ya kuingiza pesa kwenye mzunguko.
Mkulima naye anapigania masilahi ya kazi zake za shambani na Kila mtu anaunga mkono iweje Kwa watumishi?

Magu ameacha kizazi Cha roho mbaya Sana.
 
Mshahara kadiri unavyopanda na KODI huwa kubwa lazima mtambue hilo.
Hivyo hiyo nyongeza ni flat rate kwa wote ila sasa utaona umeopata % chache kutokana na nyongeza ya makato ya kodi ambayo hutokea kutokana na viwango vya mshahara.

Sio kwamba 23.3% inaenda kuongeza kwenye take home yako NOOOOO. Inaenda kusogeza Basic Salary yako, kisha Kodi inafuata na hapa lazima muelewe kodi inatofautiana kati ya kiwango cha mshahara mmoja na wingine.
Hii ni post ya ikulu, wameweka wazi ili baadae msianze kulalama
Screenshot_20220514-154241_1.jpg
 
Ngoja nimtafute Mathematician na Economist anidadavulie na anichambulie Kisomi na Kimantiki hii 23.3% ina maana gani katika Vichwa vya Watanzania wengi wepesi wa Kuridhishwa na maneno matamu matamu yenye Uwongo na Ukweli mwingi tu.

Nilipoiona tu hii 23.3% ghafla nimemkumbuka Mchumi Mbobezi Marehemu Profesa Honest Ngowi kwani kwa alivyokuwa Mtaalam nina uhakika hii 23.3% angeikosoa na Kutuelewesha tusio Wachumi na wenye Upopoma mwingi jinsi isivyo na 'direct inpact' kwa Mtanzania na Ustawi wake.

R.I.P mno Profesa Nguli Honest Ngowi.
 
Na kima cha juu ongezeko shs ngapi
Kima Cha juu hawana shida Sana hata wakiongezwa kwa asilimia 10 tu Hilo ni ongezeko kubwa sana!! Mfano: Anayepata mshahara wa 350,000/= atapata nyongeza ya 81,550/= akiongezewa asilimia 23.3. Lakini Anayepata mshahara wa 3,500,000/= atapata nyongeza ya 350,000/= akiongezewa asilimia 10.
Ila hili ongezeko lingekuwa na tija Kama lingefanyika kimya kimya!! Kwa sasa Kila kitu kitapanda!!
 
Kwamba kwa mfano aliekua anapokea 200,000 sasa atapokea 280,000 JE ALIYEKUA ANAPOKEA 280,000 ataendelea kupokea 280,000 ?!
Tatizo kuna watu humu hata maana ya asilimia 23% hamjui ni vichwa panzi mnashangilia tu kama mazuzu! Serikali imepandisha kwa wale wanaopata kima cha chini kwa asilimia 23% Ila kwa wengine haijaweka wazi! Hesabu ni mhimu sana maishani!
 
Kweli kabisa hapo inahitaji ufafanuzi..

Itakua sio nyongeza ya mshahara bali nyongeza ya kima cha chiini kwa mshahara wa serikali na sekta binafsi nchini.
Wakiongeza kwenye hizo AGGREGATE BUDGET, hapo sasa kwenye kugawana inategemea utaongezewa Tsh ngapi, kuna wengine watapata nyongeza hadi ya Tsh elfu moja moja [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom