Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Hapa kwa kima cha chini ni 23. Ila kwa waliovuka kima cha chini wamepugiwa hesabu zingine.
Yaani 1.9 trillion iwe imeongezwa kwa waliokuwa wanalipwa laki 3 kamili tu inakuja?
Wewe ndo umeelewa kama mimi! Mfano mtu analipwa lakini tatu kima cha chini cha watumishi wa umma! Huyu ndo ameongezewa kwa asilimia 23% Ila pia wengine kuna ongezek ambalo halijawekwa wazi! Ili kufikia ongezeko la tril1.9 kwa mshahara lazima kila mtumishi ambaye sio wa kima cha chini atapata ongezeko laweza kuwa halifikii 23% kama ilivyo kwa wale wa kima cha chini!
 

Rais Samia aridhia nyongeza ya mishahara kwa asilimia 23.3​

Saturday May 14 2022​

Samia pc

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3, ambapo Sh1.59 trilioni itatumika kwa ongezeko hilo.

Taarifa iliyotolewa leo Mei 14 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus inasema mapendekezo hayo ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichokifanya hivi karibuni mkoani Dodoma na kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu ongezeko la mishahara.

Taarifa hiyo imesema Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.

“Bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/23 inaongezeko la Sh1.59 trilioni sawa na asilimia 19.51 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22,” imesema taarifa hiyo.
 
Anahusikaje hapa? Kwani yeye asingepandisha? Mbona alishusha PAYE mkuu!
Mnaumia sana Sukuma gang.
Bahati nzuri niliajiriwa 2015 July kwahiyo hunielezi chochote kipya kilicholeta unafuu wa mtumishi kutoka kwa Ibilisi wenu marehemu.
Mama kuingia tu miezi 3 madaraja hayo tukavuta pesa benki.
Na sasa tunasubiri kidogo tu tuvute tena pesa.
Asiye na nyumba atajenga, asiye na gari atanunua sasa.
Na ambao tumeshaoata hivyo vyote tutafungua business Kariakoo
 
Rais Samia kwenye masuala mengine anajitahidi, yupo fast to act, which is good.

Ila kwenye mambo ya siasa anakuwa mgumu sana kuelewa mpaka pawepo na vikao vya maridhiano, tena hata kwenye masuala yaliyo wazi kisheria, ajabu sana; sijui wakina nani wanamdanganya, hajiamini.
Mambo ya siasa Kama yapi?
 
Watanzania tuna shida gani?

Hilo tangazo mmesoma vizuri kabla ya kuanza kubishana kuhusu kima cha chini?

Nanukuu " NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA IKIWEMO KIMA CHA CHINI KWA 23%"

sasa kuna wengine mmeonna KWA KIMA CHA CHINI tu.
Wanakurupuka tu hawasomi vizuri taarifa! Nilitaka kufafanua hili, umeeleweka mkuu!

Sent from my itel A16 Plus using JamiiForums mobile app
 
Wale waliokuwa nawakejeli sasa vipi hapo wekeni video za Kenya tena
Bila Nguvu ya Wananchi usingeona Vitu kama Hivi! Huu wote ni msukumo kutoka Kwa Wananchi! Hata Mafuta watu wasingepiga kelele usingeona Serikali ikichukua Hatua yoyote! Jitambue kijana
 
Back
Top Bottom