Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Hapo nimeongea na mtumishi mmoja wa umma anasema hiyo nyongeza ya 23% ipo hivi.
Kama Kima cha chini cha mshahara ni laki tatu itakuwa hivi
300,000 × 0.23 = 69,000.
Kwa hiyo watumishi wote wa serikali wataongezewa 69,000 kwenye mishahara yao.
Kwa aliyekuwa analipwa
500,000+ 69,000 =569,000
600,000+69,000=669,000
700,000+69,000=769,000
1,000,000+69,000=1,069,000
Hivyo hivyo kwa mishahara ya ngazi zote.
Sio kweli,iko hivi mshahara huongezwa kwa kuzingatia kima cha chini,maana yake mtu wa kima cha chini anaongezewa asilimia kubwa ili kupunhuza gape kati yke na kima cha juu,kwa hiyo kama kima chini anapewa asilimia 23.3 wa juu yake atapunguziwa asilimia fomula inaenda hivyo hivyo hadi wa daraja la mwisho.
Kwa mantiki hii ni kwamba mtu anaepokea let us say 250,000*0.233 =58,250 then wa juu yake asilimia itashuka kidogo lakini pesa itakayoongezeka itakua kubwa kiasi kutogautisha na wa kima cha chini mfano anapokea 350,000*0.183= 64,050 na kuendelea
Kwa mantiki hii watumishi wote lazima wataona badiliko katika mishahara yao,na nyongeza haiwezi kua flat rate!
 
Kweli kabisa hapo inahitaji ufafanuzi..

Itakua sio nyongeza ya mshahara bali nyongeza ya kima cha chiini kwa mshahara wa serikali na sekta binafsi nchini.
Potelea mbali,lkn amejitahidi.Tusubiri mwezi wa Saba tuchungulie kwenye akaunti zetu ndipo turudi hapa kujadili Ongezeko hilo.
 
Na je ongezeko hili litahesabika kama salary step?
Mfano D1 aende D2?
 
Mama ni Mama, yaani hapa ndio utajua, JPM alituua sana watanzania, yaani Mama katika mwaka mmoja kapandisha 23.3% yaani Watumishi wa umma wataandamana kumpongeza Mh. Rais Samia.

Mama Samia, watumishi wa Umma watakuombea kwa Mola na miaka yako iwe utakavyo duniani. Hii ni kazi kubwa sana Mama yetu kaifanya. Hakika Serikali ya CCM chini ya Mama yetu Samia imetenda makubwa hapa. Mungu ambariki Mama Samia sana.
Bado ni ndogo sana, ila ndio hivyo tena
 
Kweli kabisa hapo inahitaji ufafanuzi..

Itakua sio nyongeza ya mshahara bali nyongeza ya kima cha chiini kwa mshahara wa serikali na sekta binafsi nchini.
Soma vizuri ongezeko la mshahara ikiwemo kima cha chini
 
Kama kima chani ni 180,000, maana yake ongezwko ni Tsh41,400 ambayo jumla ni 221,400; bado kidogo sana na mfumko wa bei
 
Kama kima chani ni 180,000, maana yake ongezwko ni Tsh41,400 ambayo jumla ni 221,400; bado kidogo sana na mfumko wa bei
Sasa hiyo 41,400 ndo itaongezwa kwa kila mtumishi haijalishi yeye anapata kiasi gani cha mshahara, ko ongezeko itakua ni 41,000 ikiwa figure uliyoweka ndo kima cha chini
 
Ila
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akubali ongezeko la 23.3% kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma.

View attachment 2224213View attachment 2224214
TUCTA kupendekeza mafao ya wastaafu walipwe asilimia 33 ni usaliti mkubwa kwa wafanyakazi. Jambo zito kama hilo TUCTA walipaswa waendeshe zoezi la kupata maoni ya wafanyakazi kila sehemu ya ajira ( taw) ndipo wawasilishe kikokotoo kinachotokana na wafanyakazi wenyewe. Kwa kikokotoo hicho kuna wafanyakazi wengi wataambulia sh milioni saba mpaka 25 badala ya kati ya shilingi milioni 40 hadi mia walizokuwa wanapata awali kwa wale waliostaafu bila cheo. Ninamaanisha malipo ya mkupuo.

Kupunguzwa kwa rate ya kikokotoo ni suicide rope kwa wafanyakazi
 
Na je ongezeko hili litahesabika kama salary step?
Mfano D1 aende D2?

Kupanda madaraja ni tofauti na ongezeko la kima cha chini ambapo hilo huongezwa kwa wote na ongezeko hilo linakua na utofauti kulingana na basic salary yako unayopata
 
Hongereni watumwa wa serikali ila mkumbuke izo ni hela za kukusaidia kukabilia na ugumu wa maisha sio mwende kununulia magari halafu mwanze tena kuisumbua serikali ya sisiemu
Endelea kuinamishwa upate mkate wako
 
Back
Top Bottom