Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Mimi nalipwa mil 4.125 Ila mpaka Sasa sijajua naongezewa kiasi gani, nimemuuliza afisa muajiri ananiambia yeye hajui anasubiri muongozo kutoka utumishi
 
Fomula ya kukokotoa asilimia 23 ya kima cha mshahara ipo hivi:
Kima Cha chini Cha mshahara Tanzania ni 300000/=
23/100x300,000=69,000/=
Hivyo 69000-18% ya makato yote utaona umeongezewa sh.ngapi?
18/100x69,000=12,420/=
Sasa 69,000-12,420=56,580/=
Hivyo basi nyongeza ya mashahara ni 56,580/= kwa kila mtumishi.
Hivyo tegemeeni nyongeza ya 56,000/= kwenye mshahara.
Ndugu zangu msije pigia 23%ya basic eti ndio nyongeza mtakuta Julai ni tofauti kabisa.
Upo Sawa Makati mengine yanakuja by default except PAYE
 
Mkubwaa...

Hatujui hesabu ila jua kuwa hicho kima ni kwa mtu anae lipwa laki tatu pekee...
Na je...??? Anae lipwa laki nane na nusu...???
Nae anaongezewa 56k...??

Au ndo unavyo fikiri...?
Ameeleza vizuri, hiyo fedha ni mfano ukitaka kupata chukua mshahara wako kama laki 4,5,6 yoyote tumia hiyo formula
 
Mara zote sekta binafsi pia wanasetiwa viwango, hawajipangii mishahara hovyo.
Kikubwa serikali inaweza ku-set ni minimum... lakini haiwezi kuiambia sekta binafsi wapandishe kwa sababu serikali imepandisha. Ila kitakachoweza kutokea ni waajiriwa kutaka nyongeza kwa sababu wana option ya serikali yenye maslahi mazuri zaidi.
 
Kuna watu mnataka kutugombanisha na mama.Mimi nishajipigia hesabu zangu July nasubiri ongezeko la 23.3%ambavyo ni sawa na laki 223000.Maana mpaka sasa Zuhura Yunus hajatoa mchanganuo
Kuna baadhi ya Makato ni by default mfano Ada ya Chama chako ya wafanyakazi na hifadhi ya jamii
 
Nikajua ni 23% ya basic ya kila mtumishi.😁!
 
Mimi nalipwa mil 4.125 Ila mpaka Sasa sijajua naongezewa kiasi gani, nimemuuliza afisa muajiri ananiambia yeye hajui anasubiri muongozo kutoka utumishi
Samahani mkuu, unafanya kazi TCRA? Maana niliona wajuvi humu wakisema huo ndo mshahara wa afisa wa kawaida huko TCRA.

Kama ni serikali kuu, kwa hilo lifiga, unapaswa kuwa unajua kinachoendelea au utumbuliwe tu, hamna namna.
 
Hakuna kitu hapo ni ujinga mtupu...habari ya chini ya kapeti ..serikali kuanza kuchapa pesa ili kuongeza mishahara ni upuizi wa hali ya juu sh inakwenda kuanguka vibaya hadi mwezi wa 12 bei ya mafuta itakuwa sh3600 hadi 4000 kwa lita moja
Roho ya korosho!
 
Kinaongezeka kile kima cha chini na sio mshahara wote. Hahaha serikali wametumia lugha tamu kuonesha wazembe wanaongeza 23.3 kwenye basic salary
 
Mtakutana saa ngapi kwa Space 🎙 mjadili hii au mmenuna wafanyakazi kupewa shavu? 🐒😁

Tafuteni ajira sasa, sio maisha ya ujanja ujanja kupiga Porojo kwenye mitandao.
 
Duh waajiliwa wapya wa TRA wameenda kula sana maisha

Maana mshahara wanaanza nao ni 2,534,000/= hapo hapo wanakutana na nyongeza ya asilimia 23.3 yaani wanakutana na (23.3/100) x 2,534,000 = 590, 422

Yaani sasaivi ni: 2, 534,000 + 534,000 = 3,124,422

3,124,422 (yaaaani ni milion tatu, laki moja ishilini na nne elfu, na Mia nne ishirini na mbili)


Makato yakitembea hapo awezi kosa milion 2.5


Hapo bado marupu rupu ya hapa na pale.
 
Back
Top Bottom