Mambo mazuri tusifie na kwenye kudhani kuna makosa tukosoe kwa kujenga ili kuboresha. Ukichukulia hali ya kiuchumi hili ni jambo zuri litasaidia kidogo na kuwashauri serikali tu wasiongeze budget kiujumla hii pesa itoke sehemu ipunguzwe kama matumizi ya kawaida ya serikali moja ya sehemu ya kungalia sana ruzuku ya vyama vya siasa ni wakati wa kukata hii vyama vijiendeshe kwa pesa zao za ndani maana vyama vimekuwa miradi sio siasa tena. lingine bunge kuna pesa nyingi zinalipwa hivyo huko wakate hii itasaidia kugombea ubunge isiwe sehemu ya kupata riziki bali sehemu ya kupigania maendeleo na siasa.Watanzania walivyo WAPUMBAVU wapo ambao watapinga na kutoka kejeli hata kwa hili la kuongeza mishahara kwa 23.3% tena TZ ikiongoza kwa nyongeza kubwa zaidi ya Mishahara EAC.