Rais Samia akutana na Baraza la Maaskofu (TEC), Kilaini aelezea Historia yake na utaifishaji wa mashule 1970

Rais Samia akutana na Baraza la Maaskofu (TEC), Kilaini aelezea Historia yake na utaifishaji wa mashule 1970

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kukutana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) leo Juni 25, 2021

Rais atakutana nao katika Makao Makuu ya TEC, Kurasini



==========

5:30 Asubuhi: Rais Samia Suluhu ameshafika na kuimbwa wimbo wa Taifa, kinachoendelea kwa sasa ni utambulisho wa maaskofu

KILAINI AELEZEA HISTORIA YA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA
5:45 Asubuhi:
Anaeongea kwa sasa ni Askofu Method Kilaini na anaongelea historia ya baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Kilaini amesema Baraza la Maaskofu ndio uongozi wa Kanisa Katoliki na lilianza na ujio wa Kanisa Katoliki mwaka 1860.

Askofu Kilaini amesema Wamisionari walikuja na mambo matatu muhimu ambayo ni kueneza dini, kutibu wagonjwa na Elimu.

Kilaini amesema waingereza walikuwa wanaitawala Tanganyika kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa hivyo hawakutaka kuwekeza. Ndipo Kanisa lilipoamua kujaza Ombwe lililobaki ambapo mwaka 1928 waliwekeana sera kwamba msisitizo uwe Shule. Kilaini anaendelea kwa kusema maaskofu waliweka sera endapo fedha ni kidogo na inabidi kuchagua kujenga shule au Kanisa, ni bora kuchagua shule na kuacha kanisa na ndio umekuwa msimamo wa kanisa hadi leo.

Kilaini: Mwaka 1956 wakaunda Rasmi umoja wa baraza la maaskofu linaloitwa TEC na kati ya waliounda, askofu mwafrika alikuwa mmoja, Laurian Rugambwa akiwa askofu wa Rutabwa na polepole waliingia mpaka sasa unaona nyuso za waafrika pekee.

Baraza hili liliendelea na sera hiyohiyo mpaka tulivyofika Uhuru mwaka 1961 na wakaunga mkono juhudi zote alizokuwa anazifanya Mwalimu Julius Nyerere.

Alivyofika mwaka 1969/70, Nyerere alisema naona mna shule nyingi lakini nataka ziwe za watu wote, akazitaifisha. Mwaka 1970 wakati anataifisha, Baraza la Maaskofu Tanzania lilikuwa na shule za msingi 1,420. Shule za sekondari 44, vyuo vya ualimu nane halafu shule za ufundi ambazo hazikutaifishwa za wavulana 15 na wasichana 48.

Na hizi zilizotaifishwa, mama utakumbana na hii historia katika utawala wako kwasababu mashule mengine yako katikati ya mission, mbele ni kanisa, nyuma ni nyumba ya mapadri na kushoto nyumba ya kanisa, sasa tukotuko lakini tunaenda vizuri, miaka mingi tumekwenda kwenda lakini kila mara inabidi kutia nguvu sana ili kuweza kukaakaa kwasababu hiki cha katikati hiki ni kiserikali serikali na kilichozunguka ni kimisheni misheni, imekuwa ni changamoto kila mara.

Tunakushukuru mama, unapoongea Lugha yako tunaipenda, usione tumevaa mabarakoa wote hapa, maaskofu wanatabasamu sana hapa, ni kwasababu ya matamko yako unayatoa, wote wanafurahi.




Askofu Mkuu(Gervas Nyaisonga)-Rais wa TEC: RISALA YA MAASKOFU

  • Hiki ni chombo cha juu kabisa cha uongozi wa kanisa katoliki Tanzania hivyo ujio wako kwetu na uwepo wako hapa, wewe ni kiongozi mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni heshma kubwa sana kwetu sisi wanabaraza pia ni ishara ya wazi kwamba unathamini baraza hili na mchango wake kwa maendeleo ya watanzania wote.
  • Tunamshukuru Mungu kukubali wewe kuwa kiongozi wa Taifa letu na tunakuombea hekima, afya na mshikamano, Mungu akuwezeshe kutimiza majukumu yako vyema. TECL linakuahidi ushirikiano katika kusimamia ustawi wa watanzania.
  • Tunakuomba uimarishe utawala wa sheria na ujenzi wa Taasisi imara za kidemokrasia ambazo ndio msingi wa utawala bora.
Mheshimiwa Rais tukiwa tunakupongeza na kukushukuru kuwa nasi hapa, hatuna budi tukushirikishe masuala kadhaa kwa ajili ya kutuwezesha sisi kama taasisi inayoshughulika na maendeleo ya kiroho na ustawi wa Watu.
  • Katika utekelezaji wa majukumu yetu, hatuna budi kushukuru ushikiano mzuri uliopo kati ya didi kama taasisi na serikali
  • Mheshimiwa Rais mwaka 2016 sera mbalimbali zilibadilika na kutukwamisha kutoa huduma za kijamii hasa elimu bila kujali uwekezaji mkubwa uliofanywa na kanisa kabla ya hapo hii imesababisha hasara kubwa kifedha na hata rasilimali nyingine pamoja na rasilimali watu
  • Lengo la Shule zetu sio kufanya biashara bali kutoa huduma bila kujali uwezo wa wazazi wanaotaka kueleimisha watoto wao kama ilivyo Sera ya Serikali yako ya Awamu ya Sita



RAIS SAMIA SULUHU
  • Niwashukuru kwa pongezi mlizonipa kwa kushika wadhifa huu mzito na kweli niwaambie ni mzito na mwanzo ni mgumu sana. Lakini mwa ushirikiano na maombi yenu nina imani tutavuka salama,"- Rais Samia Suluhu Hassan
  • Nawashukuru kwa kuwa pamoja na Serikali katika kipindi kizito tulichompoteza kiongozi wetu Hayati John Pombe Magufuli, kwa umoja wetu tuliomba na kushirikiana tukamaliza msiba kwa amani na utulivu na Taifa letu likabaki salama
  • Serikali inawapongeza Kanisa Katoliki kwa mchango wenu kwenye jamii, kwani mmewalea wanadamu kiroho, kiimani, kimaadili, kudumisha amani, kustawisha maisha ya wananchi, kupambana na umaskini, kupunguza tatizo la ajira na kuchochea maendeleo
  • Lengo langu ni kukutana na dhehebu moja moja la dini ili kujua mema na changamoto mlizonazo ili Serikali iweze kujua jinsi ya kuzifanyia kazi
 
... baadhi ni wanafiki sana hao maaskofu! Hapo askofu ni Niwemugizi na Ruwa'ichi tu wengine chenga linapokuja suala la kuwaonya watawala. Wanageuka na kushiriki nao karamu za dhuluma!
 
... baadhi ni wanafiki sana hao maaskofu! Hapo askofu ni Niwemugizi na Ruwa'ichi tu wengine chenga linapokuja suala la kuwaonya watawala. Wanageuka na kushiriki nao karamu za dhuluma!
unafiki wao ni sasa uuseme hapa tuujue.tatizo nyinyi mnataka mkubaliwe kila kitu hata kama ni cha hovyo.tusilazimisha watu kukubali hoja ya kila mtu na hiyo siyo demokrasia.
 
Back
Top Bottom