Rais Samia akutana na Baraza la Maaskofu (TEC), Kilaini aelezea Historia yake na utaifishaji wa mashule 1970

Sijakuzwa na dini yoyote,mama akiwachekea hao atavuna mabua,hapo wanajaribu kumchokonoa Ili awaachie wasilipe kodi na leseni za biashara zao.

Shule na hospital zote za dini zinafanya biashara na sio kwamba zinatoa huduma kama wanavyosingizia, gharama huko ni kubwa karibu mara mbili ya taasisi za umma afu eti wanajisemesha.

Magu alikataa huo ujinga wa kutaka kutembelea visingizio ,lazima walipe kodi,wakate leseni na masltakwa mengine ya biashara za huduma.

Kiufupi hata sadaka zinatakiwa kulipwa kodi sasa hawa wanajificha kwenye maeneo kama vituo vya huduma za watoto yatima,wazee,walemavu nk nk..Huko ndiko kinaweza kupewa special treatment na sio kwingine
 
Yaani Hawa TEC wanashangaza,kwanza kwenye hospital zao wanaihujumu bima ya Afya kwa kuandika madawa lundo na kulazimisha vipimo.

Pili Hawa jamaa walikuwa wanaendesha taasisi za mafunzo ambazo hazikukidhi vigezo vya ubora sasa eti wanamwomba mama azifungue? Kwani mama ndio mdhibiti ubora wa Elimu na mafunzo?

Yaani wao wanaangalia tuu kupata pesa bila kujali matakwa ya ubora,naomba ieleweke kwamba si kweli kwamba kila kitu alochosimamia Magu kilikuwa kibaya,binafsi Sikuwahi mkubali kwa mengi ila kuna mengi mazuri lazima sheria isimamiwe.

Hii biashara ya ku lobby kwa Rais sio sawa na yote hii ni matokeo ya kuwa na Katiba mbovu kwamba kauli na utashi wa Rais ndio kinachosimamiwa,hili jambo halikubaliki
 
Ellen G White katika ubora wake [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yesu yupi mkuu,yule wa chato?
 
Inaonekana hujui kama ni biashara au siyo biashara.
Kwa hiyo tafuta ukweli ulivyo kwanza ili ujiridhishe, halafu ulete mada tuijadili.
Haiitaji uwe na degree kujua hilo? Leo shule zao ambazo wanaomba au wanapewa msamaha wa Kodi, bado Ada zao ni za juu kwa waumini wao,alkadhalika hospital zao pia zipo juu sana
 
Jibu ni kuwa Wao ndio walikuwa 'vilainishi' vya wakoloni kupora!

Ulitegemea TAG au KKKT au Kanisa la Kakobe liwe na shule nyingi wakati halikuwa sehemu ya Agents of Colonialism?, Hizo shule ni sehemu ndogo sana ya resources zilizokuwa zinaporwa chini ya usimamizi wao
Sasa mmesikia wenyewe kwanini kanisani lina shule nyingi
 
Uko sahihi kiongozi wangu [emoji120]
 
Acha kulia lia......
kumbe una akili ndogo kiasi hiki

usiwe maskini wa akili ndugu baraza hilo ndilo lililomuomba aende kukutana nao ktk makao yao makuu pale kurasini ili wazungumzie changamoto zao. kwani kuna dini yeyote iliyomuomba akutane nayo akakataa? mbona kwenye baraza la Eid alikubali kwenda mbona pia alikutana na viongozi wote wa dini pale dodoma hata hivyo amesema huo si mwisho wa kukutana na viongozi wa dini so tegemea pia next time atakutana na wengineo shirikisha akili kabla ya kuchangia ndugu
 
Hakukua na haja ya kuniquote. Hujaelewa kabisa hoja yangu!!?
 
Tunakuomba uimarishe utawala wa sheria na ujenzi wa Taasisi imara za kidemokrasia ambazo ndio msingi wa utawala bora.
Hii ni pointi muhimu mno na inaashiria kuwa serikali ya Magufuli haikuwa ikiongoza kidemokrasia wala kufuata misingi ya haki. Hata serikali yenyewe iliingia madarakani kwa kubaka uchaguzi mchana kweupe. Ni afadhali mwenda angefariki kabla ya uchaguzi na mama Samia aongoze nchi. Kama mwenda angefariki hata mwaka 2016 sasa hivi nchi ingekuwa imepiga maendeleo makubwa sana. Lakini Mungu mwenyewe anajua muda na wakati wa kuingilia kati ndio maana akatenda muujiza mwanzoni kabisa mwa awamu yake ya pili ya uongozi. Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo. Amina🙏🙏
 
Samia tupe katiba mpya . Na Mungu atakupa pepo yake amrikiama. INSHAALLAH..!

Mimi nilivyoona anakutana na Catholic leaders akilini kwangu ikanijia kuna siku nyingine hapo mbele atakutana na Waislamu.
Swali je, wewe umewaza hivyo??? Kwani mama Samia siku za kukalia kiti zimeisha mpk ulalamike??? Why always negative guys.
mwambie huyo
 
UKWELI ni nini?

Kweli ni NENO la MUNGU na hilo NENO limeandikwa kwenye Biblia. Sasa kipimo cha "uongo" ni KWELI.

Kanisa katoliki linafundisha kinyume kabisa na KWELI ya NENO la MUNGU.
Soma Wagalatia 1:6-9
Son of Gamba asante sana kwa kuwa na ufahamu ambao wengi sana hawanao na kuwa macho kiroho.
 
usitupotezee muda ndugu kwa vifungu vyako vya agano la kale wakatoliki hawaongozwi kwa sheria bali kwa imani kama Yesu mwenyewe alishasema kama agano la kale lisingelikuwa na mapungufu hakungelikuwa na haja ya agano jipya. amri mpya ya mapendo inakamilisha yote yaliyoko kwenye amri kumi za Mungu pendelea kusoma agano jipya itakusaidia kuiamsha imani yako haba.

 

YESU KRISTO alisema hivi :
"Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au manabii, la sikuja kutangua bali kutimiliza. Kwa maana amini nawaambia mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja, wala nukta moja ya Torati haitaondoka hata yote yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja Amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Ball mtu atakayezitenda na kuzifundisha huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni". Mathayo 5:17-19

"Mkizishika Amri zangu mtakaa katika pendo langu kama vile mimi nilivyozishika Amri za BABA yangu na kukaa katika pendo lake". Yohana 15:10

Ukisoma Maandiko utaona kuna mahali BWANA YESU anasema tujifunze kutoka kwake (Mathayo 11:29). Sasa jiulize ujifunze nini kutoka kwake kama siyo kujifunza kuzishika Amri za BABA yake kama yeye alivyozishika?

Na Je, hujasoma wewe kuwa Yakobo 2:14-17 anasema "imani bila matendo ni bure"? Yakobo anafundisha kuwa imani ili iwe hai ni lazima iambatane na matendo na sehemu moja wapo ya matendo ya imani ni kuzishika Amri. Watakatifu wote wa MUNGU wanazishika Amri.

Malizia kwa kusoma Ufunuo 14:12
"hapa ndipo penye subira ya Watakatifu hao wazishikao Amri za MUNGU na imani ya YESU KRISTO".

Alaaa kumbe! Watakatifu ni hao wazishikao Amri za MUNGU na imani ya YESU KRISTO. Kumbe "imani ya YESU" pamoja na "kuzishika Amri za MUNGU" ndiyo humkamilisha mtu kuwa Mtakatifu!!!

Kama ndiyo hivyo ni Ibilisi gani huyo anayetudanganya kuwa Amri za MUNGU zimepitwa na wakati na hatuna haja ya kuzishika?
Ibilisi huyo ndiye kanisa katoliki, anafundisha uongo na udanganyifu ili kuwapoteza hata wateule wa MUNGU.

Nami nawakumbusha tena, "tokeni kwake enyi watu wangu msishiriki dhambi zake wala msipokee mapigo yake". Ufunuo 18:4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…