Rais Samia akutana na mjomba wake ambaye ni Mwarabu

Rais Samia akutana na mjomba wake ambaye ni Mwarabu

Rais Samia amekutana na mjomba wake Oman ambaye ni mwarabu
View attachment 2260683
Kuna historia ambayo watanzania wengi hawajui! Oman mpaka miaka ya 70 hivi, ilikuwa masikini na ilikuwa na watu wachache-mara baada ya kuanza biashara ya kuuza mafuta (1967) na uchumi kuanza kupanda, ilijikuta haina watu wa kuendesha shughuli za maendeleo. Ndipo ika fanya operation ya kuwaita watu kutoka Africa Mashariki hasa Tanzania wenye damu ya uarabu hata kama ni tone tu! Wengi walikuwa wamemaliza form 4&6 na hata la saba! Walikwenda kwa mamia na maelfu kutoka Zanzibar na Bara. (ndiyo maana Kulikuwa na Sheikh Tigusikanilwa'Omugisha al Khatoum - aliezaliwa Katoma Bukoba, wakati wa ufunguzi wa msikiti wa Bukoba). Hivyo tunao ndugu zetu wa damu huko Oman. Wengi walipofika kule walipewa scholarship mpaka ulaya na nchi nyingi za nje mpaka PhD. Lugha yao huko ughaibuni walikuwa wanaongea kiswahili fasaha kuliko hata sisi watanzania wa bara. Pia wengine walikuwa wanaongea kiha, kisukuma, kisambaa, kichanga, kihaya etc.
Point yangu hapa ni kwamba siyo Samia tu mwenye ndugu huko, huenda na wewe ila hujui.
 
Hivi hii nayo ni habari??lakini sishangai hata Leo kumuona MTU au media kubwa wanamuhoji amber rutty...juu ya umaarufu wake
 
Hakuna cha uarabu hapo. Hao ni watoto wa nje waliozaliwa na housegirls wahudumu wa familia za kiarabu enzi hizo.......wamekulia kwa embe za kuokota.
Wapo vizazi na vizazi wote waarabu pure. Siongelei shombeshombe
 
Haya tena, wataalamu wetu wa mambo ya uhamiaji wana kauli gani? Huko magharibi kauli za "wewe sio raia" zimetawala kwa miaka mingi..... Ningependa kusikia ufafanuzi wa kamishna wa uhamiaji angalau kwenye hili. 🤔
 
Natumaini sasa ule unafiki wa CCM Zanzibar kuhusu “machotara wa Hizbu” na kelele za “mapinduzi matukufu; mapinduzi daima” vitaanza kuzikwa taratibu awamu hii.
 
Haya tena, wataalamu wetu wa mambo ya uhamiaji wana kauli gani? Huko magharibi kauli za "wewe sio raia" zimetawala kwa miaka mingi..... Ningependa kusikia ufafanuzi wa kamishna wa uhamiaji angalau kwenye hili. 🤔

Uhamiaji useme kwa nini Nyerere alipeleka majeshi ya uvamizi Zanzibar na kuhamishia watu wa bara ili abadilishe demographics na Uislam wa Zanzibar.
 
Kuna historia ambayo watanzania wengi hawajui! Oman mpaka miaka ya 70 hivi, ilikuwa masikini na ilikuwa na watu wachache-mara baada ya kuanza biashara ya kuuza mafuta (1967) na uchumi kuanza kupanda, ilijikuta haina watu wa kuendesha shughuli za maendeleo. Ndipo ika fanya operation ya kuwaita watu kutoka Africa Mashariki hasa Tanzania wenye damu ya uarabu hata kama ni tone tu! Wengi walikuwa wamemaliza form 4&6 na hata la saba! Walikwenda kwa mamia na maelfu kutoka Zanzibar na Bara. (ndiyo maana Kulikuwa na Sheikh Tigusikanilwa'Omugisha al Khatoum - aliezaliwa Katoma Bukoba, wakati wa ufunguzi wa msikiti wa Bukoba). Hivyo tunao ndugu zetu wa damu huko Oman. Wengi walipofika kule walipewa scholarship mpaka ulaya na nchi nyingi za nje mpaka PhD. Lugha yao huko ughaibuni walikuwa wanaongea kiswahili fasaha kuliko hata sisi watanzania wa bara. Pia wengine walikuwa wanaongea kiha, kisukuma, kisambaa, kichanga, kihaya etc.
Point yangu hapa ni kwamba siyo Samia tu mwenye ndugu huko, huenda na wewe ila hujui.
Mimi jirani yetu ana mtoto Oman na ana wajukuu. Kila mwaka huwa anakwenda kuona familia. Yeye mme wake ni wale waarabu waliokuwa wanafata pembe za ndovu au watumwa, wanaamua kuzamia na kupata vimwana wa kibantu. Wengi waliokuwa na pua ndefu halafu weupe. na wowowo .
Siyo Oman tu hata Saudia watu wana ndugu ila Oman sababu waliitawala Zenj tunasahau kuwa wareno waliacha vizazi pale, waspanish nao hivyo. Zanzibar ni kama Mauritia, na nchi nyingi za visiwa ambazo wageni wa kwanza walifikia na kuvitangaza kuwa mali yao.
 
Serikali isiposhugulikia suala la vivuko kigamboni na kutumia vya Azam mwezi hauishi tutazika ndugu zetu waishio kigamboni
 
Si mnasemaga Hayati JPM ni mrundi Mara sijui muhutu! Origine does not matter but the performance!! Hata Obama ni mkenya ameongoza taifa kubwa USA! Sisi watanzania wavivu na wanafiki tunaangaika na origine ya mtu hasa akiwa serious na taifa lake.Big shame.
 
Kwa hiyo waoman wana haki zadi kwenye ardhi ya Tanzania kuliko wamasai?

Mwenye haki ni serikali, siyo mtu wa Oman, siyo muEmirati, siyo Mtanzania. Kesho anaweza akaingia Rais mwingine akawapa Ngorongo Warusi. Hao Waemirati watakula chini.
 
Back
Top Bottom