Rais Samia alikosea Mwanzo hawezi kurekebisha kwani tayari ameshaharibu

Ingekufa 2020.
 
Mataga muda wenu umekwisha, move on badala ya kuendelea kulia lia tu.
Hilo ndiyo kosa lenu kubwa kuona eti Make Tanzania Great Again mnaona eti ulikuwa mpango mbaya kiasi kwamba mnamwaminisha Mama eti hao ni wafuasi wa falsafa mbaya wakati wananchi waliipenda Tanzania mpya. Na mkamdanganya Mama achome masoko (kariakoo, mwenge, mbeya etc) eti akija kujenga watu wataona kawajali wakati inajulikana mpango wa Mliomuambia wa kuwavuruga wananchi then atafute suluhisho yeye mwenyewe, juzi kasikika eti anaongea na wafadhili waje wajenge miundombinu wa machinga, yaani akope ili kujenga masoko ya machinga??? Kila machinga anamuona Mama hayupo sahihi kwa sababu tulishaambiwa na Dkt Magufuli nchi hii tajiri na hakuna haja ya kuwatoza watu tozo, ila yeye kadanganywa
 
Lini Tanzania ilikuwa Great?
 
Ni maoni yako ila yote ni nadharia ukiambiwa uthibitishe huwezi. Muache raisi afanye kazi hata kama ana mapungufu yake tumsahihishe sio kukosoa tu, tukubali Magufuli ame rehemika tuendelee na kazi. Hakuna kita kacho tokea we zoea tu. Ni heccups.
 
Reactions: Ame
Hatimaye umerudi mwimba pambio wa enzi zile, mini kemekuibua, au hatua za kupambana na wanahujumu enzi mpya🤔.
 
Ni maoni yako ila yote ni nadharia ukiambiwa uthibitishe huwezi. Muache raisi afanye kazi hata kama ana mapungufu yake tumsahihishe sio kukosoa tu, tukubali Magufuli ame rehemika tuendelee na kazi. Hakuna kita kacho tokea we zoea tu. Ni heccups.
Sawa....ila maoni yako inaelekea siyo nadharia isipokuwa yangu...interesting
 
Papara zake baada ya kuchukua kiti ndiyo zitamgarimu, na kama kweli CCM huiba kura basi ili mama abaki 2025 wajipange kuiba kweli kweli, la sivyo hali si nzuri. Kibaya zaidi mama hakubaliki hadi vijijini.
 
Mama Samia aliianza kutawala vizuri kwa haki, alikosea baada ya ama kwa kutaka, au kulazimishwa kutawala kwa mfano wa Magufuli. Matokeo yake amejikuta hawezi kutawala kama Magufuli maana yeye sio muovu kama Magufuli, na hawezi kutawala kama yeye maana amekubali kuiga tabia asizoziweza. Bado hajachelewa, atawale kwa haki maana serekali hii haiko madarakani kwa ridhaa ya umma, bali kwa kiburi cha madaraka cha Magufuli
 
kwa mara ya kwanza siendi kupiga kura 2025, akismama tu huyo mama bora nilale

Kama CCM ingekuwa inatagemea kura yako au kura halali, leo hii isingekuwa madarakani.
 
Kama CCM ingekuwa inatagemea kura yako au kura halali, leo hii isingekuwa madarakani.

ccm chini ya JPM ilikua inaungwa mkono na wananchi wengi sana, hata mngepiga kura mwaka mzima kulikua hamna namna mnashinda ule uchaguzi, mengi yalitokea lakini bado kulikua hamna namna mnashinda, CCM ya mkapa pamoja na JPM ndo ccm nlizojivunia sana kua mwana CCM, Japokua kuitoa ccm hata mkiungana vyama vyote hamtaweza kuitoa sio kwa sababu wanaiba kura ila ccm wapo wengi sana nadhan ni chama cha 8 ama 7 duniani saaahv
 
Nadhani kuna washauri wanaompa ushauri wa ajabu ili kumpoteza, tatizo la wabongo
 
Nani ana shida na kura za machinga na nyie wapiga Domo wa mijini?

Huku Vijijini watu wanamshukuru Rais kwa barabara,madaraja,vituo vya afya ,shule nk

Ukienda Vijijini story ni tofauti na za kwenye mitandao na mijini.Hivi mtoa mada ukifuatilia logic ya Jenerali Ulimwengu aliposema alikataa kuwa DC mjini bali alitaka Wilayani,ulimielewa?

Rais hana haja ya kuhangaika Sana na nyie machinga na wapuuzi wengine wa mjini yeye ana deal na watu wa Vijijini na wanawake, watumishi na watu wanaopenda biashara na wasanii..

Haya makundi yatamfanya apite kilaini tuu 2025,hutaki acha.
 

Ule uporaji wa uchaguzi haukufanyika kwa bahati mbaya, bali uwezekano wa CCM kushinda kama alivyotaka Magufuli haukuwepo na wala haitakuwa uwepo tena. Ni kweli Magufuli angeweza kushinda kihalali, lakini ungekuwa ni ushindi mwembamba sana, na huko bungeni ccm haikuwa na uwezo wa kufikia 2/3 ya wabunge ya kuwafanya kupitisha chochote watakacho. Na sio wakati huo tu, ni kuwa kwa sasa uwezo wa CCM kushinda zaidi ya 50% haupo tena maana ccm sio chama cha kizazi hiki. Hutaki jinyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…